Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Kipimo gani ofsa?

Unazungumzia kitu kama hiki?

View attachment 2985797

Hicho kipimo cha milion 10 ni level za GMT (pichani) ambacho sio mchongo kabisa na siku hizi hakifai hata kwa survey.

Uchimbaji wa madini wa mdau ni wa karasha wa kudili na mawe maana yake hayo mavipimo kwa shughuli yake ni useless

View attachment 2985798

View attachment 2985799

Sawa mkuu, any idea sehemu pa kuanzia?
Niko Chunya nina mchongo mkali Sana umenyooka hakuna pressure ni check 0655745533 yeyote mwenye mtaji kuanzia ml 3
 
Una chimba chunya sehemu gani?
Maana mimi nafanya shughuli hizo pia huku na nina site zaidi ya 2 ninazoendesha. Kwanza unatakiwa ujue nature ya eneo unalochimba je lina dhahabu ya vikole au ya vumbi, pili unatakiwa ujue nature ya eneo unalochimba sampo yake huwa inaanza ndogo kwenda kubwa au kubwa kwenda ndogo Kadri unavyoshuka chini, je eneo lina miamba mikubwa au midogo, je mwamba wenye dhahabu nyingi kwa eneo husika ni mwekundu, mweupe au wa zinc.
Je eneo unalochimba lina asili ya mbuga au minima, kiwango cha maji vipi n.k
Kikubwa loss kwenye uchimbaji ni kawaida zaidi fanya tafiti kabla hujaamua kuwekeza kwenye eneo husika na usiamue kwa mihemko.
Chunya bado kwa eneo kubwa ina dhahabu ya kutosha ni vile tafiti kwa kina hazijafanyika. So usikate tamaa hela ya dhahabu ni tamu sana siku ukiipata unasahau changamoto zote na unatimiza malengo yako mengi.

Ila ukiona kabisa umeshindwa ni heri huo mtaji ukawekeze kwenye KILIMO maana huku kunahitaji ngozi ngumu
Kilimo ni uti wa Mgongo wa Taifa
 
Nimepigwa mueleka huko itumbi chunya. Nimepoteza zaidi ya milioni 89 kuanzia mwaka 2020 mpaka 2023. Mtindo ulikuwa huo huo. Unapima nakutana na Ppm 6. Lakini mwisho wa kupeleka prant na elution kidogo nizimie. Nilitoa hela zote za duka nikahamishia huko. Nimerudi dukani najikongoja. Japo nitarudi tena kwenye madini
Inaonekana hakuna mawe chunya yaani unakusanya lundo tokea 2020 mpaka 2023😅 hapo gharama lazimabzikuuwe....maximum ni miezi sita lakni kama mawe ni ya kutosha na mtaji upo huwa tunasaga miezi miwili tu
 
Jiwe lipo vizuri tu mkuu. Kilichoniangusha ni uzoefu tu na kukurupuka kwa story tu unaingia mkenge kwa haraka. Hiyo milioni 89 sio kwamba ni mkupuo mmoja kwa miaka hiyo. Ni mara 2 hapo. Ni story ndefu jamaa yangu mpaka naingia hasara hiyo. Halafu kumbuka haiwi kwa mkupuo. Ksbb tunaandika siku za mwisho mwisho ndio unakutana na hasara hizo.

Kikubwa ni uzoefu tu. Kama sasa nipate milioni 30 tu naweza kurudisha hasara yote hiyo.

Chunya ni mpya mkuu ina hifadhi kubwa sana ya dhahabu mkuu. Ni mitaji tu na sana sana uzoefu. Basi
 
Ni kweli mkuu tuna clem huko matundas lakini ni ppm ya 3 hapo tilopofika, ppm nzuri ipo chini sana na uchimbaji ni gharama sana tumeshafunga winch na reli tumevuta umeme kama tukipata muwekezaji tunaweza kupiga kazi ya kueleweka, sema dhahabu zikalipuka kahama mwabomba ikabidi tuamishe kambi...kikubwa kwa biashara hizi za makarasha ni ppm tu na msimamizi wako awe mwaminifu kutoboa ni mapema sana. Usikate tamaa hapo kwa hiyo miaka miwili najua umejifunza mengi. Ebu nipe moja na mbili za eneo ulipo maana ppm ya sita ni nzuri sana tu kwa sasa, hapo tank kumi zinatosha sana..system ikoje huko?? Mnasubiri wateja au mnamaduara?? Au mnanunua mifuko?? Binafsi naogopa maduara sana.
 
Ni ukweli mchungu, lakini mafanikio mengi huanzia spiritual.... Biashara ya madini ni moja ya center za utajiri wa Dunia 🤝
Kuna usemi unasema ukitaka kumcontrol mtu mshike kwenye uchumi... Hii formula inatumiwa sana na Ibiris pamoja na mashetwani!!!!

Kwahyo sehem karibu zote zenye utajiri asilia kutoka kwa Mungu wametawala wao kiwiziwizi.... Lengo ni kuwatawala wanaadam🤝
Kwa mashart ukitaka wakupe mali ufanye wanavyotaka wao.... Mwisho wakupoteze mazima

Sasa solution hapa sio mganga bali ni mchamungu mwenye spiritual power ya kunyang'anya power ya hao viumbe wabaya kwa nguvu... Baada ya hapo kila kitu kitakaa mahala pake

Haya uje Pm kupata msaada.... Tena bure kabisa 🚶🚶
(Ukihisi ni tapeli,,,, nenda kwa kina kalumanzila wakakupigie ramli🤝🤝
 
Pole boss, wengi wame kushauri vema. Kikubwa usikate tamaa, kila kazi inachangamoto zake. Hasara ya 40mil kwenye madini ni hasara ndogo sana, ni kugusa tu. Inshort bado haujapata hasara ingawa haitakiwi upate hasara.
Tafuta wazee ambao ni wenyeji na ulipo, watakupa muongozo wa wapi uende / ufanye nini / umuonenani. Hiyo biashara ni kama biashara zingine tu. Cheza miguu yote. Kila pori na mizimu yake usiende hovyo kutafuta code bila muongozo wa wenyeji.
 
Nitakutafuta tupige kazi

Back
Top Bottom