Nimechoka kuwa mwalimu

Nimechoka kuwa mwalimu

jogijo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
260
Reaction score
495
Wakuu habari, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Nimesoma Education (bachelor of education in policy planning and management) nikispecialize kwenye Economics and accountancy kama teaching subjects, Sikuwahi kupenda kuwa mwalimu lkn baada ya kumaliza form six niliona sina option zaidi ya kuomba hiyo.

Sababu zilifanya niombe kwanza ni hali ngumu ya nyumbani na wigo mpana wa ajira na mkopo. Nilivyomaliza chuo nilibahatika kufanya kazi shule kadhaa as private baadhi zinalipa vizuri zingine ndio hivyo tena.

Mwaka 2016 nilibahatika kupata kazi serikalini, mwanzo nilifurahi lkn picha linaanza nilipangiwa shule na masomo ya kufundisha yakawa sawa yaani Economics and accountancy lakini shule niliyopangwa kwanza ni o level pili haina somo la biashara hata moja, nilivyouliza nikaambiwa Bora nikubali nafundisha hata Civics maana shule iliyopo ya biashara ni moja tu na iko kijijini sana. Nilikubali na kuanza kazi mwanzo nilifundisha Civics baadae nikaona siwezi nikahamia kwenye maths hadi sasa.

Changamoto ni nini? Nimechoka kufundisha vitu nisivyovipenda, zaidi pia ualimu ni taaluma nzuri isiyokuwa na shukrani, haina fursa ya kukua au kuongezeka kitaaluma, kiuchumi inadumaza sana.

Msaada kwenu, what is the best, nirudi shule nikasome course mbadala? Au niombe uhamisho na kwa technique ipi ili nipate kulingana na masomo yangu ili nisipelekwe huko kufundisha commerce na bk wakat Ajira yangu ni ya Economics na account?

Kama ni shule je fursa ziko wapi kati ya kozi hizi nilizozipenda?
1. Insurance and risk management?
2. Social security hii sijui kirefu sana lkn inadeal na mifuko ya hifadhi za jamii.
3. Kama ipo nyingine in relation to business niambie.

Natanguliza shukrani, na samahani kwa uzi mrefu.
 
Bachelor of education in policy planning and management ?? Chuo gani hio ?
Unataka kunikumbushia enzi za Magu, kuna Mwamba alisema alimaliza Chuo na Hana ajira Hivyo anaitaka Serikali itoe ajira. Jiwe akamuuliza maswali Matatu tu, La kwanza ulisoma Chuo kikuu kipi Tz?, La pili ulisoma kozi gani?, La tatu Ulipata GPA ya ngapi?.

Ninachokumbuka hadi leo ni kwamba yule Jamaa alisema alipata GPA ya 32, maswali mengine usiniulize jinsi alivyojibu.
 
Unataka kunikumbushia enzi za Magu,kuna Mwamba alisema alimaliza Chuo na Hana ajira Hivyo anaitaka Serikali itoe ajira.Jiwe akamuuliza maswali Matatu tu,La kwanza ulisoma Chuo kikuu kipi Tz?,La pili ulisoma kozi gani?,La tatu Ulipata GPA ya ngapi?.Ninachokumbuka hadi leo ni kwamba yule Jamaa alisema alipata GPA ya 32, maswali mengine usiniulize jinsi alivyojibu.
Jamaa aliua
 
Fursa hata kwenye ualimu zipo tatizo ulishajikalilisha kuwa haupendi ualimu. Kuwa positive na mazuri yatakuja.

Ila upande mwingine nakuelewa ni vigumu kufanikisha usichokipenda. Tumia salary Kusoma ukipendacho
Kama zipi mkuu, kilichopo kwenye ualimu ni kwamba una muda mwingi lkn hauna pesa, na kwa hapa nilipo nakosa hata fursa ya kutunga wala ku mark maana sina somo rasmi.
 
Unataka kunikumbushia enzi za Magu,kuna Mwamba alisema alimaliza Chuo na Hana ajira Hivyo anaitaka Serikali itoe ajira.Jiwe akamuuliza maswali Matatu tu,La kwanza ulisoma Chuo kikuu kipi Tz?,La pili ulisoma kozi gani?,La tatu Ulipata GPA ya ngapi?.Ninachokumbuka hadi leo ni kwamba yule Jamaa alisema alipata GPA ya 32, maswali mengine usiniulize jinsi alivyojibu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mwamba tutamkumbuka kwa mengi aise, yaani jamaa hakutegemea kuulizwa vile.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Kama zipi mkuu, kilichopo kwenye ualimu ni kwamba una mda mwingi lkn hauna pesa, na kwa hapa nilipo nakosa hata fursa ya kutunga wala ku mark maana sina somo rasmi
Kama kuna mashamba karibu Lima sana! Vitu vingine havihitaji complications.
 
Back
Top Bottom