rantheb
Member
- Jun 27, 2018
- 86
- 45
Ualimu hauna kasoro hasa serikalini, chenye kasoro hapo ni ubongo wako kutokuziona fursa za kufanya ili hali bado upo kwenye ajira. NawasilishaWakuu habari, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Nimesoma Education (bachelor of education in policy planning and management) nikispecialize kwenye Economics and accountancy kama teaching subjects, Sikuwahi kupenda kuwa mwalim lkn baada ya ukimaliza form six niliona sina option zaidi ya kuomba hio.
Sababu zilifanya niombe kwanza ni hali ngumu ya nyumbani na wigo mpana wa ajila na mkopo. Nilivomaliza chuo nilibahatika kufanya kazi shule kadhaa as private baadhi zinalipa vizuri zingine ndio hivo tena.
Mwaka 2016 nilibahatika kupata kazi serikalini, mwanzo nilifurahi lkn picha linaanza nilipangiwa shule na masomo ya kufundisha yakawa sawa yaan Economics and accountancy lakin shule niliyopangwa kwanza ni o level pili haina somo la biashara hata moja, nilivouliza nikaambiwa Bora nikubari nafundisha hata Civics maana shule iliyopo ya biashara ni moja tu na iko kijjn sana. Nilikubar na kuanza kazi mwanzo nilifundisha Civics baadae nikaona siwez nikahamia kwenye maths hadi sasa.
Changamoto ni nini? Nimechoka kufundisha vitu nisivovipenda, zaid pia ualim ni taaluma nzuri isiyokua na shukrani, haina fursa ya kukua au kuongezeka kitaaluma, kiuchumi inadumaza sana.
Msaada kwenu, what is the best, nirudi shule nikasome course mbadala? Au niombe uhamisho na kwa technique ipi ili nipate kulingana na masomo yangu ili nisipelekwe huko kufundisha commerce na bk wakat Ajira yangu ni ya Economics na account?
Kama ni shule je fursa ziko wapi kati ya kozi hizi nilizozipenda?
1. Insurance and risk management?
2. Social security hii sijui kirefu sana lkn inadeal na mifuko ya hifadhi za jamii.
3. Kama ipo nyingine in relation to business niambie.
Natanguliza shukrani, na samahani kwa uzi mrefu.