Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 829
- 1,564
Wakuu habari za mchana,
Nimekuja kwenu kuleta wazo na kuomba ushauri hii ni kutokana na ukweli kwamba nimechoka kuwapa hela vibarua wa kulima shamba langu kwa kutumia jembe la mkono.
Hivyo nikawaza nikiwa kijijini tulikuwa tunatumia jembe la kukotwa kwa ngómbe (Plau) hivi hakuna namna nikatumia hili plau na badala ya kutumia wanyama nikanunua engine ya lawn more au engine ya pikipiki au engine ya chain saw alafu nikamodify hili plau na likaweza kusukumwa kwa engine?
Hii ni kwa ajili ya kulimia eneo dogo kuzunguka makazi yangu lakini pia kwa kuwa ni maeneo mapya nitatumia pia kulima kwenye viwanja vya majirani zangu kwa kivuli cha kuwasafishia viwanja vyao na kupanda vitu vidogo vidogo.
Kwa kawaida napenda kuzalisha na kutumia vyakula ama mboga nilizolima mwenyewe ambazo najitahidi sana kutotumia viwatilifu vya viwandani na badala yake natengeza pia vya kwangu vinavyotokana na majani ya mwarobaini, vinager, maganda ya mayai nk.
Mwenye ujuzi na mambo ya mechanical na umeme naombeni ushauri