nimechoka na huyu mume msaada

Nilidhani hujui 'capacity' ya mmeo
Kumbe unaijua???

Mwanawake huwa anaolewa na mwanamme akitegemea mwanamme atabadilika na HABADILIKI
Mwanamme huwa anaoa mwanamke akitegemea mwanamke hatabadilika na ANABADILIKA

GROW UP
Huyu mtu ana matatizo lizzy yani akiwa na kazi anaweza kuchanganyikiwa kabisa sas ntambadilishaje aondokane na hii hali nahis hana uwezo wa kumanage mambo mengi kwa wakat mmoja
 
Kujali I mean anajali familia kwa mahitaji yoote lakini kimawasiliano ndo anakiwa mgumu

Davina mama why are you behaving like that my dear? Kumbe hana tatizo kama anacare kwa mahitaji yote ya family isipokuwa ni kujisahau tu kwenye simu kwa ubusy wa kazi. Nahisi wewe uliolewa bado mdogo sana hivyo hujakua. Sababu unazonipa hapa ni za kitoto sana kwa wewe kutaka kufikia hayo maamuzi.

Tulia mtoto mzuri mumeo anakupenda sana na anamenyeka kwaajili yako na watoto. Wanaume kukumendea hilo lisikudanganye coz wao huwa na hurka ya kutamano. Kumbuka kutongozwa siyo uzuri au siyo ndo kupendwa coz hata vichaa au walemavu hutongozwa na kuzalishwa tena na watu wa maana huwezi amini.

Kunamigubeli humu haijawahi bahatika kuolewa itakushauri uachane na mumeo mzuri na wamaana, au itakwambia utafute wa pembeni weee koma kabisa mamangu dunia hii imeharibika vibaya sana, utakuja kufa ungali mbichiiii..kuna watu wanapesa na mvuto na miili safi ilojengeka, wenye magari, elimu na kazi nzuri but wanaishi kwa vidonge na wanapendeza sana kwa macho. Kuwa mwangalifu mama kondom siyo ya kuiamini, we hayaaaa weeee utajakumbuka haya maneno nikufundayo mama.

Tulia tuliii ktk ndoa yako mtoto mzurii mumeo hana shida ila wewe ni wivu unaota unaibiwa kumbe siyo. Kumbuka wakupendao hukwambia ikweli daima, we have enough experience ktk ndoa thats why twakuonya mama. Usiache kuomba daima Mungu akupe amani.
 
Asante ushaur mzuri ntazingatia
 
Kuna mahali niliwahi kusikia huu msemo; "WASIWASI NDIYO MARADHI YAKO". Kwani nini unafikiria mabaya juu ya mwezako?
Hili ni tatizo la watu wasiojiamini, anajiona hana elimu ya kutosha na sasa anataka kwenda kwa baba yake akamwendeleze kielimu.

Naomba ujiamini, huyo ni mumeo.
 

AshaDii;
Hongera sana kwa ushauri wako kwa huyu dada. Siku zote umekuwa na mawazo mazuri sana. Hongera and keep it up!
 
pole sana dada yangu kwa yote yaliyokukuta lakini yote hayo ni mitihani ya kimaisha. Kumbuka kuwa uliapa kanisani/msikitini kuwa mtapendana katika shida na raha, katika mateso na uchungu hadi kifo kitakapowatenganisha. Ki ukweli watu wengi huwa haelewi nini maana ya hiki kiapo na ndio maana watu wengi hukifanyia mzaha.

Cha kufanya dada yangu kabla ya kuamua kufanya chochote naomba ujaribu kuongea na huyo mume wako umueleze jinsi unavyojisikia pale anavyokufanyia kitu flani na pia umueleze ni kitu gani ambacho yeye angependa akufanyie huwezi jua pengine anaweza kubadilika kama hiyo hali likuwa ni tabi yake na is vinginevyo.

na kama hali ukiona bado inaendelea kuwa hivyo hivyo jaribu kufanya uchunguzi pengine inawezekana akawa na mwanamke mwingine au pengine inawezekana akawa ni shoga au basha na ndio maana hana mapenzi kwako
 
Kumbe Davina na Mankaa ni mtu mmoja!
Mama jaribu kucontrol ID zako humu.

Naona manka nae kaguswa tu na tatizo langu.nashukuruni sana kwa ushauri mzuri mloonipa nahisi ni utoto unanisumbua nmeamua kutulia tu
 

dahh..umenistua cna haiwezekan hiv dia usiende mbali hivyo
 
Kujali I mean anajali familia kwa mahitaji yoote lakini kimawasiliano ndo anakiwa mgumu

kama hapo juu ni sawa, basi wewe una lako jambo na si swala la mawasiliano tu. wewe una motives zingine zaidi ya mawasiliano na ndiyo maana kuna sehemu umesema wapo wengi wanaume wanakutaka.

Ushauri wangu; ithamini ndoa yako na ipende familia yako. Achana na hao wanaokudanganya, kwani I can assure you that siku ukimwacha mmeo na kuhamia kwake huyo anayekudanganya kwasasa, ndipo utakapojua kwamba kuna wanaume wengi sana wanapenda kuwa na wake za watu na sababu kuu ni kuhusu suala la gharama. Lkn, siku ukimwambia nimeachana na mme wangu na mimi nitakuwa wako jumla kuanzia leo ndipo utakapojua ni kwanini kuna wanaume wanapenda wake za watu.

Achana na uongo wanaokuambia ohooo mimi nakupenda na nipo tayari kukuoa kama ukimwacha mmeo, sasa jaribu uone matokeo yake. Yaani miaka 7 kwenye ndoa, then leo simu inataka kuvunja ndoa? je mna watoto? hivi unapata hata muda wa kuweza kufikiria role anayoplay mmeo kwenye nyumba?

Mimi nahisi huyo mwizi anakuchanganya kwa mapenzi motomoto na labda ni vitu ambavyo unavimisi kutoka kwa mmeo na sasa unaona giza tu mbele kwa udanganyifu unaofanya dhidi ya mmeo. Davina, si ajabu kwasasa hao wanaume kibao wanaokutokea wanafanya hivyo kwasababu umependeza sasa na hii ni kutokana na care anayotoa mmeo na si ajabu hata sehemu ya hizo care ndiyo unatumia kutimiza tamaa zako. Hii inakuwa na negative impacts kwenye ndoa.

Tafadhali achana na mawazo hayo ya kuona unatongozwa na wengi na hivyo kumwona mmeo hafai na UMPENDE MMEO NA FAMILIA YAKO. Ebu ishindi hiyo roho chafu inayotaka kuvuruga ndoa yako na future yako.
RDI.
 
dahh..umenistua cna haiwezekan hiv dia usiende mbali hivyo

usikatae dada yangu. Mume wako kuwa shoga au basha inawezekana kabisa. Mimi nimeshafuatwa na waume za watu kibao ambao ni mashoga wakitaka niwananihii na hata ukitaka proof nitakupa. Sikwambii kuwa mume wako yuko hivyo ila kuna uwezekano mkubwa kuwa yuko hivyo. Jaribu kufanya uchunguzi. Umdhaniae ndiye kumbe siye
 
kama unataka kuachana naye na kwenda kwa hiyo minjemba mingine inayokumendea si uondoke tu? kwa taarifa tu, kila mtu ana weaknesses zake; so, get prepared!
 
heeee davina mme kuzima simu tu unataka kurudi kwenu,yaani ukimpa baba yako hiyo sababu atakurudisha kwa mmeo mapeeeeeeeeeema, vuta subira atakutafuta na muulize kwa nn alizima simu,kuna mazito zaidi ya hayo kwenye hizi ndoa
 
miaka saba bado tu inshu ya simu inatishia usalama wa ndoa yako?

Hatukujiandaa kukabiliana na changamoto za teknolojia mpya, ni wazi simu , facebook ni vitu vinavyotesa mahusiano mengi katika dunia yetu sasa, kumbe kama walizoeshana kupigiana simu kila wakati na pale mtu asipopiga mashaka kibao, basi huu ni ukweli juu ya hayo anayosema ILA itakuwa ni ajabu kuchukua uamuzi anaozungumzia kama hakuna sababu nyingine, wakati mwingine tunatakiwa kuzoea haya mambo!
 

Swali zito sana kwa kwa ma lovey wa kisasa yani hawa ni full pasua kichwa. Yani huyu wa kwangu anataka tuwasiliane kila saa yani mpaka kero sometime anaweza kuniita ofisini kwao bila sababu yoyote ya msingi huku akijua wazi kuwa mimi pia nimeajiriwa na huwa nipo na boss karibu muda wote. Nisipokwenda sasa huwa ni kesi ya kuvulia shati. Yani haya mapenzi haya karibu nta resign
 
Dawa Yake na wewe Mzimie Simu tu na siku akirejea halfa wivu ukimshika mwambie nilikuwa kwa Duduwasha huwa hapendi niwashe simu! akikomaa mwambie hupendi tabia yake ya kuzima zima simu! hapo atajirekebisha!
 
Achana na ushauri wa saluni. Kumejaa manungayembe yasiyofugika.
 
Kama wanaume wangekuwa hivi basi wote wangekuwa wameachana na wake zao zamani sana. Duniani kuna mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…