kama hapo juu ni sawa, basi wewe una lako jambo na si swala la mawasiliano tu. wewe una motives zingine zaidi ya mawasiliano na ndiyo maana kuna sehemu umesema wapo wengi wanaume wanakutaka.
Ushauri wangu; ithamini ndoa yako na ipende familia yako. Achana na hao wanaokudanganya, kwani I can assure you that siku ukimwacha mmeo na kuhamia kwake huyo anayekudanganya kwasasa, ndipo utakapojua kwamba kuna wanaume wengi sana wanapenda kuwa na wake za watu na sababu kuu ni kuhusu suala la gharama. Lkn, siku ukimwambia nimeachana na mme wangu na mimi nitakuwa wako jumla kuanzia leo ndipo utakapojua ni kwanini kuna wanaume wanapenda wake za watu.
Achana na uongo wanaokuambia ohooo mimi nakupenda na nipo tayari kukuoa kama ukimwacha mmeo, sasa jaribu uone matokeo yake. Yaani miaka 7 kwenye ndoa, then leo simu inataka kuvunja ndoa? je mna watoto? hivi unapata hata muda wa kuweza kufikiria role anayoplay mmeo kwenye nyumba?
Mimi nahisi huyo mwizi anakuchanganya kwa mapenzi motomoto na labda ni vitu ambavyo unavimisi kutoka kwa mmeo na sasa unaona giza tu mbele kwa udanganyifu unaofanya dhidi ya mmeo. Davina, si ajabu kwasasa hao wanaume kibao wanaokutokea wanafanya hivyo kwasababu umependeza sasa na hii ni kutokana na care anayotoa mmeo na si ajabu hata sehemu ya hizo care ndiyo unatumia kutimiza tamaa zako. Hii inakuwa na negative impacts kwenye ndoa.
Tafadhali achana na mawazo hayo ya kuona unatongozwa na wengi na hivyo kumwona mmeo hafai na UMPENDE MMEO NA FAMILIA YAKO. Ebu ishindi hiyo roho chafu inayotaka kuvuruga ndoa yako na future yako.
RDI.