Nimechoka tabia ya watu kuja kwangu na kuniomba kila kitu wanachokiona nimenunua

Kuna wengine wakiona umenunua kitu kikali kama raba au t-shirt utasikia niuzie hii. Yaani wao kwenda kununua hawezi kuchagua au hii mimi naichukia balaa
 
Unaombwa kitu na hauwezi kukataa halafu mwisho wa siku unakuja kulaumu watu kwa kukufanyia jambo ambalo wewe mwenyewe ulilikubali.

Wewe kushindwa kuwakatalia wanaokuomba kisa kuogopa kuonekana una roho mbaya ndo kunakugharimu mali zako, pesa zako, hata amani ya moyo.

bora kuonekana una roho mbaya kuliko kuonekana boya. wewe unaona unawasaidia, wao wanakuona boya, huna uchungu na jasho lako.

wewe ndo wa kubadilika sio wao, jifunze kusema HAPANA.

Uzi wako umetamka maneno mengi ila herufi sita tu zinakushinda kumtamkia binadamu mwenzako.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 

Wana + Ndugu + Mademu = Umaskini

Ukishakuwa maskini Utawaona Kabisa, Acha ukarimu wa Kifala, na ni kwa sababu una cha kuwapa ndo mana unawaona.

Tafuta mke, wana na Ndugu watakaa mbali, ila mke nae adui wa karibu, chagua kwa makini, fuata ushauri wa Imani yako.
 
Acha uchoyo mkuu we wape tu
So far viko store wanakusaidia ku dispose
 
Mkuu huwa unashikiwa panga na watu unaowapaga hivyo vitu???
 
Toa ulichonacho,Mungu anakuona hadi ndani ya moyo wako
 
Umeoa?! Kama haujaoa tatizo linaanzia hapo. Unapokuwa na mke, mojawapo ya majukumu yake ni kulinda mali zako.

Wanawake ndio husaidia kukulindia mali zako dhidi ya watu wanaotaka kukufuja.

Mkiambiwa ndoa huwa mnawaza kugegeda tu. Ukiwa na mke hata mshahara utaona unatumikaje na utaenda vizuri. Ila ukiwa haupo na mke na hauwezi kujisimamia , utashangaa pesa inapotea na haujui imekwenda wapi.
 
Basi nakushauri uoe nduku, utakuja kunambia hapa. Mwambie mkeo awe ndio Procurement officer. Najua watu watamind ila baadae watazoea kuwa fulani mkewe anabana balaa.
 
Ukitoa toa bila kukumbuka, ukitoa na kusononeka siyo vizuri...
 
Mbona wewe hujaoa, umebaki kuwa mshauri wa masuala ya mahusiano wakati huna hata mchumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…