nimechoshwa na hawa majembe auctioneers.

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,692
Kwa mwana jf aliyebahatika kupita njia ya mandela maeneo ya taraza siku ya leo atakuwa amekutana na vijana waliovaalia mashati meupe yenye mikono mirefu ambayo kifuani kwenye mfuko yamechorwa herufi M na kisha kuandikwa kwa maandish madogo ya blue majembe auction mart.

vijana hawa walionekana kuleta kero sana kwa watumiaji wa njia hasa kwa waliokuwa wanaelekekea temeke wakiwa kwenye mataa hapa NMC. walichokuwa wanakifanya ni wanasogelea gari sehem ya kwenye kioo kisha wanamwambia dereva paki pembeni ili wakague. sijui kwann nimeshindwa kuelewa maana ya kitendo kicho kwan nimewaza kwan huyu majembe ni badala ya traffic polisi? na je TRA hawana uwezo wa kukusanya mapato toka kwa wamiliki wa magari hadi watumie mtu kati ambaye inabidi alipwe?

haya kama ilinekana basi kunasababu ya kuwa nao hawa majembe kwann bas wasipewe elimu juu ya usalama barabaran? kwani inaelekea kabisa kwamb hawajui, ingekuwa wanajua wasingeweza kauondoa gari kwenye folen na kulipaki pembeni katika mdomo wa mataa, pia wangejua kabisa kwamba eneo wanalotumia ni risk areaa sana kwani ni karibu sana mna njia ya reli kias kwamba ukidelay magair kwa muda kidogo tu unasababisha kero si tu kwa magari bali hata njia ya reli.
 
kwa nini mtu anapaki wakague?

Je kisheria wana uhalali wa kukagua? Kwa kutumia sheria ipi? Wanasheria mje hapa mtueleze kina Ruttashobolwa

na wanavyotaka usimame what if ni majambazi ndani ya kivuli cha majembe?

Tazara na veta ni maeneo wanayopenda kusimama.... Binafsi nitasimama kama tu trafiki kanisimamisha, wanasimamisha watu kwa kibali gani?

Angalau tra naweza simama....ila napo kama wapo na trafiki mji umeharibika huu, ajira milioni moja zinaweza kukuketea upotevu wa mali
 
Last edited by a moderator:

hawa ni Agent wana tumika kukusanya hasa madeni sugu na muda mwingine wana tumika kufanya minada kwa wateja wanao shindwa kulipa madeni mfano ya bank, pango la nyumba n.k, na kabla ya kufanya hivyo lazima muhusika upewe taarifa na barua una sign na wana kuwa na vitambulisho na barua ya utambulisho kutoka kwa shirika wanalo lifanyia kazi husika!

Hivyo basi inawezekana wamepewa tenda la kukamata magari ambayo hayajalipiwa TRA lakini lazima wawe na vitambulisho na barua na pia kuna kuwa na mfanyakazi mmoja toka shirika husika ana ambatana nao!

Na hii inafanyika sababu watu wana kwepa kulipa kodi na watu wana kwepaa vilivyo!

Lakini muwe makini hata wezi utumia huo mwanya

updates
Nimesikiliza na kutazama habari jioni hii kupitia kituo cha ITV huko shinyanga kama sijakosea afisa TRA wametoa angalizo kwa wateja kuwa kuna watu wapita barabarani na sehemu za biashara wana sema wana kusanya madeni ni matapeli na wakatoa angalizo kuwa watu wasitoe pesa kwa hao watu!

Kwa hiyo be care!
 
Hawa wanaweza tambulika na wana haki "under law of Agent"
na wana tumika kufanya kazi kwa niaba ya mtu fulani au shirika fulan lakini lazima wawe wameidhinishwa(Authorised) kufanya hivyo na wana ingia mikataba na hayo mashirika au watu!

Unacho takiwa ni kujua ya kwamba lazima wawe na vitambusho si t.shirt tu na barua ya kufanya ukaguzi!

Na unatakiwa uwaombe kitmbulisho na pemmit ya kufanya ukaguzi na huwa wana ambatana na wafanyakazi wa TRA!
Be wanned

nimesikiliza taarifa ya habario ya ITV kuna afisa wa TRA amesema kuna utapeli unaendelea kwamba kuna watu wana kusanya pesa barabarani na kusema wametumwa na TRA lakini ni huko shinyanga na amesema msitoe pesa kwa mtu yeyote lakini hawakutaja watu hao kwa hiyo kuweni makini msije kutoa pesa barabarani!

 
Last edited by a moderator:
Huu ni ulaji wanaopeana bila ya aibu..! Hivi wanaweza kuhalalisha malipo kwa kampuni kama hii ya majembe..? Jee wanasaidia kukusanya kiaci gani cha mapato TRA ambacho kitahalalisha malipo kwa kampuni hiyo ya majembe..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…