Nimechoshwa na maisha ya upweke

Nimechoshwa na maisha ya upweke

Pole!!

Nimewahi kuona mdada hapa akitafuta mwenza ambae ni mwathirika.Inawezekana!!
 
pole sana,
usikate tamaa kwakuwa umelifikisha hapa ngoja tusubiri wenye ushauri na walengwa waweza pata hapa jf
 
Pole sana

Usikate tamaa......kwani hakuna lisilowezekana.....hapa ulipolileta naamini hitaji lako limefanikiwa....kila la heri
 
Pole sana
kila mtu anawake, na wako yupo. Kaza mwendo..
na ninakusifu sana kwa kuwa mkweli ..HONGERA SANA..
 
pole sana.

Mtangulze mungu, atakupatia mwenzi wako!
Kila la kheri.
 
mkuu pole sana
nakushauri uwe mwangalifu sana kwenye hili,tayari wewe ni mwathirika na unapenda kuwa na mwenzi,tahadhari usije chukua kitu cha kukumalizia maisha yako,unaweza pata mwenza akakumaliza na mapresha ya maisha,nakushauri endelea kutulia na jiunge kwenye vikundi mbalimbali vya kukufanya uwe busy,kama wewe ni mristo jiunge na kwaya itakusaidia sana ule muda wa kwenda kufanya mazoezi utajumuika na watu na utachukulia maisha po
japo mimi sijapima lakini tupo nyuma yako mkuu
 
Mkuu pole sana. mw/mungu akutie nguvu.
Naami utapata tu mwenzi ambaye naye hali zenu zitalingana yani wote matakua na hitajio linalofanana.

Nakuombea kwa Mungu akufanikishie hili.
 
inawezekana sana mkuu...Mungu akujalie upate haja ya moyo wako.
 
daaaaah! Pole sana mkuu. Upweke sio kwako ni kwa kila mtu hata kwa wale ambao hawajaathirika. Hata hivyo inabidi uwe makini katika kuchagua, isije ukachukua mtu ambaye ndio akakuzidishia matatizo zaidi. Mtu sahihi hayuko mbali, subira itakufanya umpate atakayekufaa. Endelea kujitunza mkuu ili uendelee kutoa mchango wako katika jamii.
 
Dah!Pole sana,usijali natumai Mungu atakusikia bro,usijali!
 
Waungwana naomba msaada wenu, naishi na virusi vya ukimwi yapata miaka 7 sasa,mwenzi wangu ametangulia mbele za haki miaka 4 iliyopita.<br />
Nahitaji kuowa tena, nitampataje atakaye nikubali na hali yangu?
<br />
<br />......maisha ya upweke kwel yanachosha,umejtahd sn kuwa pekee.utampata ucjal
 
pole sana kaka. usijali,jiweke wazi.unaweza kushangaa ukapata mwenza asiye na hiv na mkapendana kiasi cha kuamua kuwa pamoja. kila la kheri
 
pole sana, Mungu ni mwema, endelea kumuomba nasi tupo nyuma yako. usijekupaparika ukapata mwenza akakupa magonjwa ya moyo bure. taratibu utapata sabuni ya roho yako!
 
pole sana kaka, kwa mungu kila kitu kinawezekana utampata tu atakae kufaa.
 
Mzelokotwa nadhani kule mnakoenda kuchukua dawa is the best place to find a partner. Nadhani pale ndio utakutana na wadada ambao na wao wameathirika basi mkaongea na kujenga uhusiano Mkuu
 
Back
Top Bottom