Nimedhamiria Huu mwaka najenga

Hiyo ya kulipa day kwa fundi ni kama daily uko site kusimamia Kazi mwenyewe vinginevyo hakuna kipimo maalumu cha kwamba leo utajenga hadi hapa.

Watu sasa tumetoboa projects kadhaa effectively kwa style hyo (Goba Areas). Tunaenda site mapema asubuhi na jioni pia tunapanga kazi na kutoa maagizo site mtu 3 tu….Fundi na Vibarua Wawili au Sumtyms Watatu na Ujenzi Unaenda Bila Shida Na unakuta una save hela kibao.

Uraiani kuna nguvu ngazi nyingi sanaa alaf bei chee sanaa na fundi anajiona don maana kazi yote anakimbiza mwenyewe (unacheza na akili yake tu) and u end up saving a lot of money effectively.

Mfano mimi nyumba yangu ya mwisho kupiga plasta ilikua kazi ya watu wawili tu fundi na kibarua nyumba yote 3 bedroom, dining, living room, kitchen na store na jiko la nnje…ilikua kazi ya siku 8 unajua nilitumia bei gani ?? Nyumba nzima ndani na nnje. Na watu huko sijui wanapigwa mabei gani ??

Akili Kichwani.

Mimi plan yangu ni kuwa strongly based in Goba nishaona potential ya haya maneneo miaka ya mbele sasa nina team ya vijana wangu kama wa 5 hivi yani hawa siwatupi labda wazingue wenyewe. Hadi Fundi Sibadilishi.

Huyo fundi ujenzi kichwa sanaa hadi kupaua anajua, blandering, tiles na bomba za choo zote anaweka yeye……style ni ile ile tu ya kulipana kazi yote nimemuambia anafanya mwenyewe….umeme, welding na decor ndio nachukua mtu mwingine nao kuna namna nishawaset kisaikolojia mwanzo hawakunisoma vizuri.

Na sasa nikuchane kama madirisha ya welding nenda manzese mashine kule kanunue ready made vipimo vyako tu either 6 x 6 au 5 x 5 na baadae unayaremba vizuri tu yote yanafanana bei moja chee sanaa mnooo…..nachukua pick up ya mzee wangu natia wese napeleka site na drive mwenyewe…na kijana wangu wa site.

Na mjue hizi idea inabdi mnilipe mjue maana nawapa maisha basi tu HaHaHa [emoji1787]
 
Hujasema hio plaster ndani nyumba nzima umetumia bei gani? Grill moja unapata kwa bei gani? Tuwekee bei tuone tunavyopigwa.
 
Hujasema hio plaster ndani nyumba nzima umetumia bei gani? Grill moja unapata kwa bei gani? Tuwekee bei tuone tunavyopigwa.

Plasta mafundi kama nlivyosema awali nawalipa day job 20,000 - 25,000 (kama ni 20,000 nimempa fundi namtia 2000 ya nauli hakai mbali na goba) ina range humo siku zingine nampa 25,000

Kibarua alikua anakula 15,000 anaishi goba huko huko…..vijana wapo wa kutosha sana and cheap labor….na wanakuwa na adabu cz mtu ana uhakika wa kila siku kula 15,000 sibadilishi vijana wengine wa akiba nlikua nao wawili incase wakiwa na udhuru kikubwa wawe waaminifu tu.

Ma grill ya madirisha chuma tupu sio dirisha za mbao na nondo (80,000 - 90,000) manzese tu hapo
 
Fundi 8days 200,000
Kibarua 8days 120,000
Total 300,000
Haina tofauti na rate ya 70,000 per room ambapo nyumba ya kawaida kama hio yako nawapa 300,000/-
Grills nimenunua 100,000 bila kujali size
 
Fundi 8days 200,000
Kibarua 8days 120,000
Total 300,000
Haina tofauti na rate ya 70,000 per room ambapo nyumba ya kawaida kama hio yako nawapa 300,000/-
Grills nimenunua 100,000 bila kujali size

Safi, Basi nawe uko exposed kuna watu humu wanapigwa mahela mengi unasoma posts unacheka tu behind the screen.

Grills umenunua wapi ??

Hyo rate yako ya 70K kwa vyumba vyote nlivyotaja hapo inazidi na sumtyms huenda ukapigwa cement ujue unaeza ukawa unalipa bei ndogo as labor charge ila ukiwa hujui mambo yalivyo wanakuliza materials. Mimi nanunua kidogo kidogo na na monitor materials zote 24 / 7 /365.
 
Kuna fundi amenitengenezea. Kuhusu material huwa nanunua mwenyewe kiasi kinachotosha siku hio,nasimamia mwanzo mwisho
 
Tumefanana kila kitu hadi mpango wa ramani ya nyumba hapa nina laki 7 mimi yangu vyumba 2 kimoja self choo cha public jiko dining stoo naweka under ground maana najenga msingi mrefu sababu ya maji.

Fundi ni mm mwenyewe wa kila kitu nitakua na mafundi wa day waka usafiri ninao power tiller bati 54 zinatosha najenga temporary
 
Shukrani sana
 
Usimdanganye, mshikaji wangu kapoteza huko usd 11000 na utaalam wake
 
Hizi nyumba zinamudu vizuri masika ikiwa utapata mafundi wazuri japo miongoni mwa CHANGAMOTO ni upakaji wa rangi baada ya muda flani maana kuta zinakutana na maji kuanzia juu, pia ikiezekwa vibaya kwenye junction ya bati na ukuta nyumba inaanza kuvuja.
Ungesema na hizo complication mkuu ingesaidia wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…