Nimeenda leo kanisani mhubiri akaniita "YESHURUNI" Nikalia Sana.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
NIMEENDE LEO KANISANI MHUBIRI AKANIITA "YESHURUNI" NIKALIA SANA.

Anaandika Robert HERIEL
Yule Shahidi,

Ole wangu Mimi ikiwa nimekuwa Yeshuruni, nitatengwa na Mkono wangu utatupiliwa mbali, ingawa najua wengi wenu hamumjui huyo Yeshuruni ni Nani.

Leo nikalisogelea lango la Kanisa ikiwa ni muda mrefu toka niache kwenda kanisani, kilichonipeleka Kanisani pengine hakikuwa cha muhimu, Ila kikawaida Taikon ninaupata umuhimu wa kwenda kanisani pale Mungu anaposema na Mimi kupitia watumishi wake watakaotoa ujumbe mbele ya madhabahu.

Basi baada ya Aya nyingi kutolewa ndipo Yule mhubiri akatoa Aya iliyoushtua moyo wangu, ukausigina, ukauponda ponda hata ukasagika, Yule mhubiri akatuagiza tufungue Kumbukumbu la Torati 32:15 kisha akaanza kusoma Kama hivi;

"
Kumbukumbu la Torati 32:15
" Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake"

Yule mhubiri hiyo aya alivyoitoa nilihisi ananisema Mimi, au anawasema watu mfano wangu, watu tufananaye na Yeshuruni.
Tulionenepa, tukawa na Shukrani ya punda ambayo ni mateke, tukamuacha Mungu ambaye ndiye aliyetufanya tuwe hivi tulivyo, wengine ni Mataikon, wengine amewafanya hivyo mlivyo Kwa kadiri ya mafanikio yenu. Lakini mwisho wa siku tumemdharau Mungu ambaye ndiye mwamba wa wokovu na mafanikio yetu.

Asilimia 90% tuliosoma mpaka kufikia vyuo vikuu na elimu za juu tulitoka katika umasikini wa kuogofya, Nani ambaye hakumuomba Mungu wakati anasoma kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu.

Ninaoushahidi wa kutosha katika Mazingira yetu, watu wote niliowaona wamefanikiwa shuleni walikuwa waombaji wazuri,
Tena Kwa tulipokuwa chuo kuna Baadhi ya Kozi coursework zilizokuwa zinasuasua zilitufanya tumuombe Mungu kikweli bila kujali Tunasoma Kwa kiwango kipi.

Ni mara ngapi kabla hatujapata kazi, tulikuwa tukiomba Mungu atusaidie tupate bahati kwani ngazi ni chache lakini waombaji tena wenye vigezo tulikuwa wengi, matokeo yake tulipopata kazi tukageuka Yeshuruni.

Hata Watu mfano wa Kiranga wengi wao walikuwa wanamuomba Mungu lakini wamegeuka na kuwa kama Yeshuruni, wamesahau walikotoka, na ni uhakika hawajui waendako.

Mahubiri ya Mhubiri Yule yalinifanya nikumbuke nyuma kidogo nilipokuwa mdogo, nikajikuta nalia machozi,
Machozi ya uchungu, Leo kisa nimekuwa Taikon ndio nimemsaliti Mungu wangu aliyenifanya niwe hivi nilivyo, nikesahau Enzi sina Ada wala pesa ya Tuition lakini Mungu alinifaulisha mitihani,
Nimesahau shule nilizosomea zilikuwa na changamoto lukuki lakini Kwa uwezo wa Mungu nikafika Chuo kikuu. Wala sikuwa na akili kuwashinda wengine lakini Mungu tuu huyu basi acheni tuu.

Nimesahau nilivyokuwa sina nguo za kuvaa,
Nimesahau tulivyokuwa tunalala sehemu mbaya,
Nimesahau jinsi nilivyokuwa tunadharaulika, Yote hayo nimesahau, nimekuwa Kama Yeshuruni.

Ati leo hii kisa chakula hakinisumbui, nguo hazisumbui, makazi hayasumbui ndio maana inafikia hatua ya kumdharau Mungu na kumuacha, loooh!

Kwa wasiomjua Yeshuruni ni jina jingine la Waisrael, Waisrael Musa aliwaita Kama Yeshuruni akiwatabiria Kama watakuja kumuasi Mungu licha ya yote aliyowatendea.
Yeshuruni ametajwa mara nne kwenye Biblia.

Wito: tusisahau tulipotoka,
Nimejitumia Kama kiwakilishi cha waliowengi walio Yeshuruni, ambao Kwa sasa mmefanikishwa katika njia zenu mkamsahau aliyewasaidia.

Mungu mwenyezi anasema; Nitamheshimu atakayeniheshimu, nitamdharau atakaye nidharau.

Yeshuruni nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mwenge, DAR es salaam
 
Huu Uzi nimezamia tu naomba niende huku waje wazee wa upako , SDA n.k
 
Ni kweli mkuu hata watu waliotusaidia tumewasahau!Mungu anatuona
 
Back
Top Bottom