Nimeenda sehemu na baiskeli nikaisahau nikarudi na mguu

Nimeenda sehemu na baiskeli nikaisahau nikarudi na mguu

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Hii hali sio maramoja imekuwa ikinitokea Mara kadha ya kusahau vitu sasa leo nikaenda mgahawani kula baada ya kumaliza kula nikarudi zangu ofisini na mguu.

Baada ya kufika ofisini ndo nagundua kwamba nimeisahau nilipokuwa nakula sasa ikabidi niirudie.

Kama wiki mbili hivi zimepita nilifika ofisini kwa mtu nikawakuta watu wazima wawili baada ya kuwasalimia mimi nikaitikia marahaba.

Wale wazee wakacheka sana na kuniambia ndo ukubwa ulivo.
 
Hiyo hali imekuwa ikinipata sana mimi.
Kuna siku nilibeba dumu la maji na kuingia nalo bafuni kuoga, sasa Ile nimefika bafuni kwa kuhangaika kulibeba ndiyo kwa mbaali nilikuwa nafikiria mbona kama ndoo nzito sana?

Ndo nakuja kugundua kuwa nimebeba dumu.
 
Hii hali sio maramoja imekuwa ikinitokea Mara kadha ya kusahau vitu sasa leo nikaenda mgahawani kula baada ya kumaliza kula nikarudi zangu ofisini na mguu.

Baada ya kufika ofisini ndo nagundua kwamba nimeisahau nilipokuwa nakula sasa ikabidi niirudie.

Kama wiki mbili hivi zimepita nilifika ofisini kwa mtu nikawakuta watu wazima wawili baada ya kuwasalimia mimi nikaitikia marahaba.

Wale wazee wakacheka sana na kuniambia ndo ukubwa ulivo.
Mbonaa kama ndo wale wa kupokea simu afu unabisha hodiiiiii badala ya halooo.... 😂😂😂😂😂
 
Mm shida yangu nikifunga ghetto langu nikifika kituo cha basi nakuwa nimesahau km nilifunga au niliacha wazi inanibizi nirudi nikahskikishe

Mpaka nikanunua solex ili nikiona ninafunguo najua nilishafunga
 
Zipoje hizo
Screenshot_20240803_234241_Chrome.jpg

Disclaimer:
Mimi siyo daktari. Kamuone dr wako kwa ushauri juu ya tatizo lako
 
Aisee mkuu unachekesha sana, matatizo kama haya huwa ni kwa mabachelor, keep bachelorism🤝
 
Back
Top Bottom