Nimeenda sehemu na baiskeli nikaisahau nikarudi na mguu

Kuna jamaa mmoja nae akienda kariakoo akishapaki gar katika mitaa kadhaa,baadae anasahau kapaki wapi

Ila ishawahi kunitokea mara chache sana napiga simu halafu ikiwa sikioni nasahau nilikuwa nampigia nani

Ikawahi kutokea simu ikiita nashtuka balaa

Alhamdulillah hizo mambo ziliisha zote

Evelyn Salt nipo home now,,tusiulizane niko wapi
 
Sawa upo home, ndio usipokee simu 😹
Pokea umpe mkeo nimtakie usiku mwema.
 
Msongo wa mawazo mda mwingine
 
Ushawahi kutoka sebuleni unafuata kitu chumbani ukifika hukumbuki ulifuata nini? Au unasikia simu inaita ukiiangalia iko kimya? Unatoka nyumbani ukiwa njiani huna uhakika ulifunga mlango au hukufunga, ulizima feni au hukuzima?
Karibu uzeeni.
 
Aisee hizo ni stress kuna kipindi stress zilizidi nikasahau password ya simu nilikaa siku mbili nimeshindwa kufungua password ambayo naitumia kila siku
 
Jana jioni Kuna jirani yangu nilimsalimia nikamwambia habari za jioni akaniambia salama za asubuhi mke wake akamwambia ni asubuhi saa hizi!? afu ni mstaafu!
 
Nouma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…