Nimefanikiwa kuanzisha kikundi cha maendeleo

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Napenda kuleta mrejesho hapa jamii forum maana ni sehemu ambayo nilipata wazo la kuanzisha kikundi cha maendeleo.
Nilisoma uzi wa mkuu mmoja unaohusu vicoba. Nikavutiwa na namna vicoba vinavyoendeshwa hivyo nikaamua kuchukua idea na kuwapa baadhi ya watu wangu wa karibu.
Ninachofurahi ni kuwa walipokea wazo lile na kwa pamoja tukaamua kuanzisha kikundi ambacho mwanzo tulipanga tukiendeshe kwa mfumo wa vicoba lakini baadaye nikaamua kubadili maamuzi na kukifanya kuwa kikundi cha kudumu cha kusimamia miradi mbalimbali.

Kikundi kina wanachama 10. Ambao tumejiwekea kutoa mchango kwa mfumo wa hisa. Hisa yetu moja tunaiuza sh 10,000 ambapo kila mwanachama lazima anunue kila wiki. Pia kana atahitaji kununua hisa nyingi kwa wiki, zisizidi 3.
Pia tunakopeshana wenyewe kwa riba nafuu kabisa.
Tumepanga kufungua mradi wa kwanza mwezi wa sita mwaka huu.

Lengo la kuanzisha uzi huu ni kuomba ushauri namna ya kuweza kusajiri kikundi ili kitambulike na tuingie kwenye mikopo nafuu inayotolewa na taasisi mbalimbali.
Ni hatua zipi inatupasa kuzifuata ili tuweze kusajiliwa bila vikwazo.

Ahsanteni sana
 
Kwanza mnapaswa kuwa na shughuli maaalumu ya Kikundi ambayo ndiyo Core Function, Pili kuwa na Katiba ya Kikundi, Tatu kikundi kiwe na Bank account.
Baada ya kuwa na document hizo utaenda Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa au Jiji ya eneo mnapofanyia kazi zenu Ukiwa na nyaraka hizo. Utaingia Idara ya Maendeleo ya Jamiii kuomba kusajili kikundi chako na Gharama za Usajili ni Tshs.30,000/= Elfu thelathini. Kama yapo marekebisho ya Katiba utarekebisha na kama hakuna tatizo la Katiba utapewa Usajili bila shida.
 
Mkuu kindly share mrejesho wa taratibu za kufungua kikundi hasa ktk vipengele vifuatavyo...

1. Nyaraka za kuambatanisha ni zipi..
2. Ofisii ya Msajili ni ipi..
3. Gharama za kusajil na gharama endelevu ni kiasi gani..
4. Idadi ya chini kabisa ya wanachama wanaoweza kuanzisha kikundi ni ngapi..
5. Matakwa mengine ambayo ni muhimu sana kuzingatia..


Natanguliza shukurani.
 
Kwanini msisajili kampuni mkuu?, kwa sababu kikundi mtabaki local sana ila kampuni mtaweza kutanua mipaka.

Tafuteni mtaji wa kama milioni 5 hivi mfungue kampuni yenu hao hao watu 10 kama mpo siriazi.

Nimesema milioni 5 sababu ni kiasi kizuri kuanzia kama mtaji wa kampuni ila hata chini ya hapo mnaweza kusajili vizuri bila tatizo.

Kwa haraka haraka hapo mtasajili kwa gharama isiyovuka Tsh. 150,000 Brela na ni wiki tu mnapata cheti cha usajili

Fikirieni tena vizuri mkuu, kampuni ni best move mkuu trust me, achaneni na kikundi sijui kikoba.
 
Hello, Naomba nikusaidie kwa ninayoyajua;
Mimi sijamaliza miez miwili toka nifanye usajili wa kikundi changu, Kuna mambo muhimu ya kuzingatia ukitaka kuanzisha kikundi kama ifuatavyo;
Katiba ya kikundi, Hii ndo huwa inabeba lengo la kikundi pamoja na taratibu zake, Mnatakiwa kuwa wana kikundi wasipungue 10, Na mkishakamilisha hayo ili kuanza taratibu za kusajili kikundi chenu, mnatakiwa kuandaa muhtasar pamoja na Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa, ambayo itapitia kwa mtendaji wa kata na kupigwa muhuri hapohapo itapitishwa na afisa maendeleo wa kata yenu.

Baada ya hapo, Unapswa kuwa na kiasi cha Tsh 50,000 kama ada ya usajili, sijui kama hicho kiwango kinatumika kwa mikoa yote ila kama uko Arusha hiyo ndo ada. Hatua inayofuata ni usajili utaambatanisha hizo nyaraka hapo juu (Katiba, barua ya maombi ya usajili, Muhtasari, na Barua kutoka serikali za mitaa) na utaenda kwa mkurugenzi wa Jiji sehemu unapoishi office zake, hapo wa watapitia nyaraka zako kisha watakupatia Acc no ukalipie ada, halaf watakupa maelezo ya lini kuja kuchukua cheti chako cha usajili.

Baada ya kupata cheti cha usajili sasa unaweza kwenda kuanza taratibu za kufungua account; Bank nzuri kwa account ya kikundi nakushauri Equity, Haina mlolongo mrefu na pia hakuna makato ya mwezi wala ada ya kufungulia tofauti na bank nyingine

Aina ya kikundi CBO ( Community based Organisation )
 
Ahsante sana Mkuu kwa maelezo makini kabisa..

Roughly, mchakato mzima ulikuchukua siku ngapi kukamilisha..

Pia, nalenga kufungua kikundi cha kijasiriamali, nacho kinaangukia category ya CBO....

Natanguliza shukurani.
 
Ahsante sana Mkuu kwa maelezo makini kabisa..

Roughly, mchakato mzima ulikuchukua siku ngapi kukamilisha..

Pia, nalenga kufungua kikundi cha kijasiriamali, nacho kinaangukia category ya CBO....

Natanguliza shukurani.
Mchakato ulinichukua kama wiki Mbili kwani, taratibu za Barua na kulipia nilitumia siku mbili, baada ya hapo week ya kwanza ikapita inayofuatia Tukapata cheti chetu.

Nadhani itaangukia huko kwani vikundi vingi naona huwa wanatumia CBO kujisajili....
Pia Mnapokuwa mmepata usajili ni rahisi pia kupata Mikopo ile inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya VIkundi vya kijasiriamali na pia Hata kama mtahitajia kupata bima ya afya Mkiwa na usajili ni rahisi kupata Bima kwa gharama ndogo tofaut na mtu mmojammoja.
 
Ahsante sana kwa ushirikiano big boss..

Unastahili kabisa kuwa na kikundi,kwa sbb ya roho nzuri sana ya ushirikiano uliyonayo..

Mungu azidi kukubariki katika eneo hilo..

Siku Njema.
 
mtafute afisa maendeleo wa jamii aliyepo karibu nawe muulize kuhusu mkopo wa magufuli usio na riba mkipata hiyo ita boost sana kikundi chenu
 
mtafute afisa maendeleo wa jamii aliyepo karibu nawe muulize kuhusu mkopo wa magufuli usio na riba mkipata hiyo ita boost sana kikundi chenu
Ahsante kwa taarifa..
 
Ahsante sana kwa ushirikiano big boss..

Unastahili kabisa kuwa na kikundi,kwa sbb ya roho nzuri sana ya ushirikiano uliyonayo..

Mungu azidi kukubariki katika eneo hilo..

Siku Njema.
Amina'
Pia kuna jamaa anaitwa kivuyo, nimejaribu kutafuta uzi wake nikuwekee ila sijaupata nilishawahi kuusoma huko aliweka maelezo mengi yanayohusiana unaweza kupitia site yake
https://www.kivuyo.com/taratibu-za-kufuata-katika-kusajili-kikundi-kikoba/ alinipa mwanga sana jinsi ya kufungua
kama jinsi ya kuandaa Muhtasari, taratibu za kufuata nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…