RESOLVED Nimefanikiwa kupata huduma lakini NSSF Ilala Boma Watoa huduma waboreshe Customer Care

RESOLVED Nimefanikiwa kupata huduma lakini NSSF Ilala Boma Watoa huduma waboreshe Customer Care

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Nilijisajili na NSSF Mwaka 2017 wakati naanza chuo, wasajili walikosea tarehe yangu ya kuzaliwa, nimekuja kugundua na kuanza utaratibu wa kuomba kubadilishiwa ni baada ya kupata ajira Mwaka huu 2026 Februari.

Nilivyoanza mchakato katika Ofisi za NSSF jengo la Benjamin Mkapa lilipo Posta ILALA, Dar es Salaam waliniomba niende ofisi zilizopo Ilala BOMA, DAR ES SAALAM.

Nimefika na kupewa utaratibu wa namna ya kuomba kuandika barua ya kubadilsha taarifa zangu za kuzaliwa ijapokuwa kulikuwa na changamoto.

Wahudumu wa pale (NSSF Ilala Boma) hawana Customer Care kabisa, kuanzia lugha na maelekezo hadi kwenye kutoa huduma.

Mfano mhudumu anakupa maelekezo nusunusu unaenda kufanya mchakato labda wa kutafuta saini na mhuri wa muajiri unarudi anakuelekeza tena uandike barua, unaandika bado anakuelekeza jambo lingine, eleweni kuwa watu wapo kwenye ofisi za watu, hivyo hawana muda wa kuzunguka kwenye ofisi zenu kila siku.

Baadaye nimefanikiwa kukamilisha michakato yote ya kuweza kujaza fomu, kuandika barua pamoja na michakato.
 
Kuna nssf kibaha,wao kila siku mtandao hawana,halafu hawana msaada wowote,ukienda pale eti wanakuelekeza uende stationery ya nje ukapewe maelekezo..unajiuliza hawa watu wanalipwa mishahara kwa kazi gani wanayofanya?
 
Stationery ya nje ni ya mfanyakazi mmoja wao wa hapo NSSF mjomba.
Michezo ya stationery ya nje ipo sana TRA.
 
Nssf yote uwa wanajiona .sijui uwa wanajikuta nani.
Lakini hilo tatizo hata benki zetu wanalo.
 
Back
Top Bottom