Nimefanikiwa kupunguza uzito, zifahamu mbinu zangu na changamoto zake!

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Takribani miaka 8 nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la kuongezeka uzito wa Kg 2.125 kwa mwaka. Uzito wangu wa kawaida ulikuwa ni Kg 75, hadi kufikia April,2013 nilikuwa na Kg 92 ambazo ni ongezeko la Kg 17. Urefu ni Sm 178 na umri wangu ni miaka 31.

Nimekuwa nikitumia asali mbichi kwa kuitia kwenye maji ya moto yaliyochanganywa na Tangawizi iliyo pondwa pondwa asubuhi kwenye kifungua kinywa na jioni kabla ya mlo wa jioni. Nilipunguza kiasi cha chakula nilichokuwa nakula na asubuhi nilikuwa natembea Km 4, 2 wakati wa kwenda na 2 wakati wa kurudi. Tangu April -August, 2013 nimepunguza Kg 8 na sasa nina uzito wa Kg 84 tu na bado naendelea kupunguza.

Ingawa kitambi bado kipo, naamini kitakwisha kabisa. Suruali zote zimepwaya na sasa nanunua nguo zingine.

Natoa shukrani zangu kwa Mzizi mkavu na wadau wengine wote , haya ni matunda ya michango yenu hapa JF Doctor!
 
Hongera sana. Hiyo asali na tangawizi ndo ulikuwa unatumia kama chai ama na chai ulikuwa unakunywa?
 
asali na tangawizi inasaidia sana kupunguza uzito.mi huwa nakunywa tu asubuhi na jioni bila mazoezi but nimefanikiwa kupunguza uzito despite of lack of exercise..
 
Deal hapo umepunguza intake ya msosi (carbs) na kuongeza matumizi ya calories (mazoezi).
Kupungua carolies in lazima iwe ndogo kuliko burnt carolies.
Kumaintain ni carolies in iwe sawa na calories burnt.

Hongera, ukifikia uzito unaouhitaji tafuta balance ya intake na carolies burnt.
 
Asali na tangawizi mm haitonifaa kwa sababu ya tumbo langu. Sijui asali tupu inafaa?
 
Hongera sana. Hiyo asali na tangawizi ndo ulikuwa unatumia kama chai ama na chai ulikuwa unakunywa?

Nashukuru Mkuu! Chai nilikua sinywi kabisa, sababu sukari ya kawaida nayo huchangia kwa kiasi fulani kuongezeka kwa uzito hasa kwa wanaofanya kazi za ofisini ambazo hazitumii nguvu za mwili.
 

Mkuu nashukuru kwa maelezo yako ya kitaalamu, ukifika uzito ninaouhitaji itabidi ni-maintain intake na carolies itakayokuwa released from the body!
 
Asali na tangawizi mm haitonifaa kwa sababu ya tumbo langu. Sijui asali tupu inafaa?

Kuanywa glasi ya maji ya moto yaliyotiwa asali kijiko kimoja asubuhi, mchana na jioni kabla hujala milo ya kawaida. Kuna thread humu za Mzizi mkavu zinaelekeza vizuri, zitafute uzipitie na uzingatie maelekezo, hakika tatizo lako litakwisha! Mbona mimi nimeweza?
 
Hongera saaaaaana ila mie nina 100kg nam nikifanya hivyo nitapungua???
 
Mkuu ulitumia mbinu gani kuongeza uzito?plz

Kuongezeka kwa uzito kunaendana na kunenepa. Kunenepa kunategemeana na mwili wako jinsi ulivyoumbika au kurithi kutoka kwa wazazi au ukoo wako. Kuna wengine miili yao haina shukrani hata uilishe nini na hata umiliki dunia nzima iwe chini yako lakini huwezi kubadirika. Hapa nilitaka kukueleza kuwa, kilichonifanya mimi kunenepa na kuongezeka uzito si kwamba na wewe itakuwa hivyo la hasha! Hivyo basi, ni jambo ambalo halina formular. Unataka unenepe ili iweje? Usiombee tafadhali ni shida tupu!
 
Pia kuna majani ya chai yanaitwa slimatee kama sija kosea jina lake, yanauzwa elfu 30 nakuendelea. Nimazuri kwa kupunguza uzito na unene.
 
Mkuu Mshua's Umejitahidi Hongera zidi kutumia dawa upunguwe mpaka ufike kilo 70.

Hongera saaaaaana ila mie nina 100kg nam nikifanya hivyo nitapungua???
Mkuu gondolwa Jaribu kufuata ushauri wa mkuu Mshua's usipofanikiwa hebu pitia hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doct...to-wa-mwili-na-unene-na-mafuta-mwilini-5.html

Mkuu Bujibuji habari yako? Nawewe una kilo ngapi? unataka kupunguwa?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…