SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

Stories of Change - 2022 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwezi januari mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi,ambae ni mtoto wa kipekee kutoka katika familia hii masikini.

Mama huyu alininyonyesha, akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua kwa kupewa maziwa ya ng'ombe kwa kuwa hawakuwa pia na uwezo wa kuninunulia maziwa ya kopo (lactogen),baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona alishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi. Kiukweli kipenzi mama yangu aliumia na kuteseka sana kwa maisha aliyopitia.

MAISHA YA SHULE
Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza, mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.Na kila wakati mama alipokuwa akiniona alinikumbuka na hali yake kidogo kubadilika lakini ni kwa muda mfupi,hali iliyonifanya kuzidi kupambania ndoto zangu ili ziweze kutimia.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7, nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto"(nyumba za kupanga) waliopitia shule za kata wanayajua maisha haya. Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana , mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo Dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .5 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na akasema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

Kumbuka wakati huo tunaenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hatukwenda na vyeti,hivyo ilinilazimu kuwasiliana na shule nilyomaliza kidato cha nne ambapo kulikuwa na mwalimu aliekuwa karibu yangu sana,kiukweli alinisaidia sana mpaka nikapata vyeti(cha kuzaliwa na kidato cha 4),kuhusu cha kidato cha sita(6) niliprint matokeo kwa sababu yalikuwa tayari yametoka.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine ambayo ilidumu kwa muda wa miezi 6 tu,na kufanikiwa kumaliza nakufaulu vizuri tu,,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masomo ya udaktari,kiukweli kwa mliopita muhimbili mnapajua maisha ya pale ni magumu sana,ilikufaulu inakubidi kusoma kwa bidii sana ,mimi pia ilinilazimu kusoma kwa bidii sana, ndipo nilipofanikiwa kumaliza masomo yangu kwa ufaulu mzuri tu kwa sababu niliamini penye nia pana njia, nilitunukiwa udaktari wangu ambao niliusotea kwa miaka 5 pale lengo ni kumsaidia mama yangu kipenzi ambapo muda wote huo nilikuwa namuomba Mungu azidi kumpa afya ili nije kumtibu salama salimi,na sasa ni daktari nimeajiriwa katika hospitali ya Arusha(Mount Meru)

SAFARI YA KUMTIBU MAMA
Baada ya tu ya kuwa daktari, nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi, nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India(hapa nilipata wafadhili kwa maana nilikuw atayari nimejuana na kufahamiana na madaktari wengi niliosoma nao chuoni, na tukahitimu pamoja) ,Nilifika India na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu, tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
 
Upvote 252
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
hii story umeibadilisha baadhi ya vitu ila kuna mwanamke wa kinaijeria ambae alitoa hii story bhna kma upo mount meru watu wapo tutawauliza waje kuthibitisha hpo
hlf ata mm nimezaliwa 97 ila f6 unatkiwa umalize 2017 au 2018 punguza uongo bhna
 
Bado taarifa hazipo sawa, umesema ulizaliwa 1997 na ulianza darasa la kwanza 2003 ukiwa na miaka 7, lakini kimahesabu mtu aliyezaliwa 1997 hadi kufikia 2003 anakuwa na miaka 6 na siyo 7 kama ulivyosema.

Pia, kwa mtiririko huo, ulitakiwa umalize kidato cha 6 mwaka 2016, ilikiwaje wewe ukamaliza 2015?
Dah watu mmemkomalia hahah!
Lakini nadhani ujumbe wake umefika japo data zake amezichanganya.
 
Huyu toka shindano la mwaka jana anatunga uongo ambao "Hauleti Changes Zozote Kwenye Jamii".

Hizi ni fantsy stories ambazo hazina applications yoyote kwenye jamii, ni hadithi kama zile za Alfu Lela U Lela, Esopo nk.

IMG_20220809_141506.jpg
 
Kuna Uzi kawaombea ushauri wanafunzi wake waliochaguliwa kujiunga advance iringa girls yeye akiwa kama madam hapo shuleni,Leo kawa doctor wa vichaa[emoji16]huku Jf Uhuru umezidi sana
Bila kusahau alishawahi kuwa kahaba ila akapambana akaachana na biashara hiyo na kufanikiwa kuwa dereva ikulu.
 
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)

Nasoma kwanza comments, baadaye nitaamua either kukupongeza au otherwise
 
Nahitaji kukuoa,
mi niko single,
sina historia ya ndoa,
Nyumbani Kwetu NI Malambo bila Shaka unapajua,
 
Back
Top Bottom