SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

Stories of Change - 2022 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwezi januari mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi,ambae ni mtoto wa kipekee kutoka katika familia hii masikini.

Mama huyu alininyonyesha, akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua kwa kupewa maziwa ya ng'ombe kwa kuwa hawakuwa pia na uwezo wa kuninunulia maziwa ya kopo (lactogen),baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona alishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi. Kiukweli kipenzi mama yangu aliumia na kuteseka sana kwa maisha aliyopitia.

MAISHA YA SHULE
Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza, mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.Na kila wakati mama alipokuwa akiniona alinikumbuka na hali yake kidogo kubadilika lakini ni kwa muda mfupi,hali iliyonifanya kuzidi kupambania ndoto zangu ili ziweze kutimia.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7, nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto"(nyumba za kupanga) waliopitia shule za kata wanayajua maisha haya. Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana , mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo Dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .5 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na akasema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

Kumbuka wakati huo tunaenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hatukwenda na vyeti,hivyo ilinilazimu kuwasiliana na shule nilyomaliza kidato cha nne ambapo kulikuwa na mwalimu aliekuwa karibu yangu sana,kiukweli alinisaidia sana mpaka nikapata vyeti(cha kuzaliwa na kidato cha 4),kuhusu cha kidato cha sita(6) niliprint matokeo kwa sababu yalikuwa tayari yametoka.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine ambayo ilidumu kwa muda wa miezi 6 tu,na kufanikiwa kumaliza nakufaulu vizuri tu,,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masomo ya udaktari,kiukweli kwa mliopita muhimbili mnapajua maisha ya pale ni magumu sana,ilikufaulu inakubidi kusoma kwa bidii sana ,mimi pia ilinilazimu kusoma kwa bidii sana, ndipo nilipofanikiwa kumaliza masomo yangu kwa ufaulu mzuri tu kwa sababu niliamini penye nia pana njia, nilitunukiwa udaktari wangu ambao niliusotea kwa miaka 5 pale lengo ni kumsaidia mama yangu kipenzi ambapo muda wote huo nilikuwa namuomba Mungu azidi kumpa afya ili nije kumtibu salama salimi,na sasa ni daktari nimeajiriwa katika hospitali ya Arusha(Mount Meru)

SAFARI YA KUMTIBU MAMA
Baada ya tu ya kuwa daktari, nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi, nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India(hapa nilipata wafadhili kwa maana nilikuw atayari nimejuana na kufahamiana na madaktari wengi niliosoma nao chuoni, na tukahitimu pamoja) ,Nilifika India na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu, tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
 
Upvote 252
Dokta Amina,
Mm naomba unitibu Korodani zangu nipo hapa Ngaramtoni,Arusha.
 
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
Hongera sana habari yako itaenda badirisha maisha ya wahanga wa ubakaji na ukatili wa kijinsia nashauri isiishie hapa jf tafuta namna jamii ipate funzo hili muhimu ,hakika umemfuta mama machozi wewe ni shujaa !
 
M naomba kuuliza kuna kipindi ulileta uzi ukasema ww ni Mwalimu naomba ufafanuzi hpa
Tena alisema kuna mabinti wawili wanaomba ushauri kwake, mabinti hawa walichaguliwa kusoma kidato cha tano ila hawakutaka kusoma. Walichotaka ni kwenda vyuo vya kati kama sijakosea.
 
Ndugu yangu ni wa 2000 na alianza shule mapema na miaka 7 saivi yupo MD 2 anaingia MD 3 sasa huyu yeye katupiga changa la macho umri huo anakua bado ajamaliza ata internship apate leseni ya udaktari
😀😀😀😀😀
Anatupiga kamba sana, kuna mdau huko juu kasema hii stori iliwahi kutolewa na mwanamke wa Kinaijeria ila huyu kaibadilisha kidogo(hachomoki kwenye plagiarism sasa)
 
Mimi nikianza kumuhoji huyu mahakamani nita muonea bure ngoja niwaachie wajumbe wa shindano hili.

Kwanza uandishi wake tu, inaonesha ni mtu wa namna gani, wewe kama ni daktari unafanya nini humu badala ya kuhudumia wagonjwa kwenye hospital uliyo pangiwa ??

Hiyo hospital unayo fanyia kazi mshahara ni mdogo ? Sins mengi ya kuongea ngoja nikae kimya tu.

nikianza kumchambua sitamtendea haki yani dogo amesoma vizuri moja kwa moja na kupata ajira alafu moja kwa moja kaenda India alafu moja kwa moja yupo anafanya kazi arusha ?????
 
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .4 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na aksema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
Hongera sana dr. Amina, hakika Damu ni nzito kuliko Maji. Mama kichaa lkn alimtambua mwanae baada ya miaka mingi.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Kuna kitu sijaelewa hapa. Umezaliwa 1997, shule umeanza ukiwa na miaka 7 hapo ni mwaka 2004. Ukijumlisha miaka 7 ya shule ya msingi inakuwa shule ya msingi umemaliza 2011. Ongeza miaka minne ya O-level inakua 2015. Jumlisha miwili ya A-level inakua 2017. Degree ya udaktari inatolewa miaka mitano ambapo kwa hesabu mwaka huu 2022 ndo ulitakiwa uwe mwaka wa mwisho wa masomo yako ya udaktari. Hapo bado hujafanya internship kwa mwaka mmoja. Naomba nifafanulie hapo Mkuu.
Na amepata hela ya kumtibu mama yake India. Anyways, ni shindano watu wanajaribu bahati zao. 😁
 
Mimi nikianza kumuhoji huyu mahakamani nita muonea bure ngoja niwaachie wajumbe wa shindano hili.

Kwanza uandishi wake tu, inaonesha ni mtu wa namna gani, wewe kama ni daktari unafanya nini humu badala ya kuhudumia wagonjwa kwenye hospital uliyo pangiwa ??

Hiyo hospital unayo fanyia kazi mshahara ni mdogo ? Sins mengi ya kuongea ngoja nikae kimya tu.

nikianza kumchambua sitamtendea haki yani dogo amesoma vizuri moja kwa moja na kupata ajira alafu moja kwa moja kaenda India alafu moja kwa moja yupo anafanya kazi arusha ?????
Kwani udokta kuusomea ni miaka mingapi? Maana alizaliwa 1997 alipofikisha miaka 7 akaanza shule ( sijui primary au pre ) ko 2004 la 1 -2010 la 7. 2011-14 o'level, 2015-17 advance 2017-21 udokta km ni miaka mi4 au 2022 km ni miaka mi5. Hapo ajira na matibabu India
 
Mimi namjua Dr. Mariam daktari intern wa vichaa pale muhimbili🤗
 
Uzalendo huanzia pale binadamu anapotafakari kwa kina juu ya Upendo wake halisi kwa nchi, kazi, jamii, familia na yeye binafsi. Kama hakuna Upendo katika nyanja zote hizi ndipo FIKRA HASI zinapozaliwa sasa, fikra za kutokujipenda mwenyewe na kujivalisha maisha ambayo si halisi. Fikra za kutoithamini jamii kwa kuirithisha fikra zisizo na tija. Fikra za kulifikirisha taifa kwa hadithi za abnuasi nk.
Kikubwa tujitahidi kuwa tayari kujifunza na kurithishana fikra CHANYA kwa Upendo na si kutengeneza hisia ambazo inawezekana si halisi kwa mujibu wa tafiti za wapembuzi wa makala hii.
Hongera kwa uthubutu wa kuandika naamini ukweli na uhalisia wa andiko hili mpaka sasa upo nafsini mwako.

Tuendelee kujifunza kwa Upendo
 
Woow hongera kwa jitihada zako binafsi na kumtibu mama yako. Wewe nj mwanamke jasiri sana. Kila lenye Baraka likafunike maisha yako
 
Back
Top Bottom