SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

SoC02 Nimefanikiwa kuwa Daktari kwa msukumo wa mama ambae ni kichaa, alibakwa akanizaa mimi

Stories of Change - 2022 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwezi januari mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi,ambae ni mtoto wa kipekee kutoka katika familia hii masikini.

Mama huyu alininyonyesha, akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua kwa kupewa maziwa ya ng'ombe kwa kuwa hawakuwa pia na uwezo wa kuninunulia maziwa ya kopo (lactogen),baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona alishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi. Kiukweli kipenzi mama yangu aliumia na kuteseka sana kwa maisha aliyopitia.

MAISHA YA SHULE
Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza, mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.Na kila wakati mama alipokuwa akiniona alinikumbuka na hali yake kidogo kubadilika lakini ni kwa muda mfupi,hali iliyonifanya kuzidi kupambania ndoto zangu ili ziweze kutimia.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7, nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto"(nyumba za kupanga) waliopitia shule za kata wanayajua maisha haya. Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana , mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo Dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .5 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na akasema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

Kumbuka wakati huo tunaenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hatukwenda na vyeti,hivyo ilinilazimu kuwasiliana na shule nilyomaliza kidato cha nne ambapo kulikuwa na mwalimu aliekuwa karibu yangu sana,kiukweli alinisaidia sana mpaka nikapata vyeti(cha kuzaliwa na kidato cha 4),kuhusu cha kidato cha sita(6) niliprint matokeo kwa sababu yalikuwa tayari yametoka.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine ambayo ilidumu kwa muda wa miezi 6 tu,na kufanikiwa kumaliza nakufaulu vizuri tu,,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masomo ya udaktari,kiukweli kwa mliopita muhimbili mnapajua maisha ya pale ni magumu sana,ilikufaulu inakubidi kusoma kwa bidii sana ,mimi pia ilinilazimu kusoma kwa bidii sana, ndipo nilipofanikiwa kumaliza masomo yangu kwa ufaulu mzuri tu kwa sababu niliamini penye nia pana njia, nilitunukiwa udaktari wangu ambao niliusotea kwa miaka 5 pale lengo ni kumsaidia mama yangu kipenzi ambapo muda wote huo nilikuwa namuomba Mungu azidi kumpa afya ili nije kumtibu salama salimi,na sasa ni daktari nimeajiriwa katika hospitali ya Arusha(Mount Meru)

SAFARI YA KUMTIBU MAMA
Baada ya tu ya kuwa daktari, nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi, nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India(hapa nilipata wafadhili kwa maana nilikuw atayari nimejuana na kufahamiana na madaktari wengi niliosoma nao chuoni, na tukahitimu pamoja) ,Nilifika India na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu, tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
 
Upvote 252
Hii ni stori nzuri ila nina ulakini ndani yake kwa sababu zifutazo
1.Umesema wewe sasa ni daktari ila nikipiga hesabu ya mtu wa mwaka 1997 probably alimaliza kidato cha sita 2017 kwahyo
MD1-2017/2018
MD2-2018/2019
MD3-2019/2020
MD4-2020/2021
MD5-2021/2022
Internship-2022/2023
sasa dada yangu Amina68 huo udaktari wako umeupataje mapema hivyo na unasema upo hospitali ya Arusha wakati kwa hesabu za haraka haraka unatakiwa uwe mwaka wa 5 (MD5)
Nawasilisha
[emoji23][emoji23] na amesema kamaliza la saba 2009 hii inamaana form 4 kamaliza 2013 na six 2016 si 2015 kama alivyosema [emoji23][emoji23] kweli wahenga hawakukosea walivyosema

"Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu".
 
kwani wote huanza std 1 with 7 years?
 
Hii ni stori nzuri ila nina ulakini ndani yake kwa sababu zifutazo
1.Umesema wewe sasa ni daktari ila nikipiga hesabu ya mtu wa mwaka 1997 probably alimaliza kidato cha sita 2017 kwahyo
MD1-2017/2018
MD2-2018/2019
MD3-2019/2020
MD4-2020/2021
MD5-2021/2022
Internship-2022/2023
sasa dada yangu Amina68 huo udaktari wako umeupataje mapema hivyo na unasema upo hospitali ya Arusha wakati kwa hesabu za haraka haraka unatakiwa uwe mwaka wa 5 (MD5)
Nawasilisha
Kadanganya kwenye field ambayo anaonekana haijui hata kidogo,ndiyo maana story imekuwa na mgongano.Angefanya utafiti kabla ya kupost story ili mambo yaendane
 
nashukuru sana Istone
Habari wana jukwaa wote!

Kwa majina naitwa Amina kama nilivyojisajili kwa forum hii.

Mimi ni mtanzania ambae nimetokea katika familia maskini sana kule SIMIYU kijiji cha itilima. Nilizaliwa mnamo mwaka 1997 katika mazingira ambayo sio salama na mama yangu ajulikanae kwa jina la Minza, ambae alibakwa ndio nikazaliwa mimi.

mama huyu alininyonyesha ,akanilea na kunipenda sana japo ndugu zangu walimnyang'anya baada ya kufikisha miezi 6 tu wakaamua kunilea mpaka nakua,baba yangu simfahamu lakini mama yangu nilimfahamu baada ya bibi yangu alienilea kunifahamisha na siku moja kwenda kunionyesha.

Mama aliponiona laishtuka japokuwa ni kichaa,lakini alinitizama na kunifata mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikumbatia kwa nguvu sana,alinidondosha chini na kuning'ang'ania sana,nami sikupenda kuondoka katika mazingira yale lakini,ndugu walionipeleka kunionesha walikuja kunichukua kwa nguvu alipokuwa mama.

mama alikuwa haogi ,anakula barabarani na majalalani alikuwa pia akibakwa na kila mpita njia asie na maadili ambae alitaka hamu zake azimalizie kwa mama yangu kipenzi.

MAISHA YA SHULE

Nilipofikisha miaka 7 nilianza darasa la kwanza ,mjomba wangu ambae ni mdogo wake mama alinipeleka shule, wakaniandikisha ,kiukweli tangu nipo darasa la kwanza ,kila siku nilikuwa namuwaza mama yangu tu.kuna wakati niliwahi iba chakula ofisini kwa walimu (ulikuwa mkate) nikampeleka mama maana mitaa aliyokuwepo niliifahamu fika.

Nikafanikiwa kumaliza darasa la 7,nikachaguliwa kujiunga shule ya sekondari iliyopo huko itilima bariadi, Nilianza masomo yangu nikiwa sina hata daftari wala kulipa mchango wowote lakini darasani nilikuwa ninajitahidi sana kusoma kwani nilikuwa ninawaongoza wenzangu kwa kushika nafasi ya kwanza,nilipofika kidato cha pili. Mkuu wa shule yetu aliniita ofisini na kuniuliza kwanini sijawahi lipa chochote tangu nimefika pale? Kwani alitaka kunipa barua kwapelekea wazazi wangu nyumbani ndipo nilipoamua kumpa historia ya maisha yangu.

Mkuu wa shule, aliumia sana na kuamu kunilipia kila kitu na kuniamishia nyumbani kwake kwa sababu hapo shule nilikuwa nikitoka naenda kuishi "gheto". Pia nilimweleza mkuu wa shule kwamba ninahitaji kusoma kwa bidii lengo niwe daktari bingwa nimtibu mama angu, pia nilitamani sana mpaka namaliza kusoma mama awe hai.

Nilisoma kwa bidii sana ,mtihani wa kidato cha nne nilifanikiwa kuijunga na shule ya wasichana msalato iliyopo dodoma mchepuo wa PCB.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kuchaguliwa JKT ambapo nilienda bila kuogopa katika kambi ya RUVU iliyopo Pwani.

wakati nipo mafunzoni, matokeo yalitoka na nilifanikiwa kupata DIV.I .5 tukaendelea a mafunzo wakati tukifanya maombi ya mkopo na chuo kikuu. Wakati nipo jeshini kuna afande mmoja alikuwa anapenda sana kutupa elimu kuhusu mambo ya kusomea chuo na maisha yalivyo mbeleni, haswaa nikamuona huyu ndio muhusika na sahihi katika kumfata.

Nilimfata na kumueleza kuhusu historia ya maisha yangu na ninachokihitaji, lakini nikamuuliza kwamba nimesikia jeshi wanataka madaktari sana akasma ni kweli, nikamwambia kwamba napenda sana kazi ya uanajeshi lakini niwe daktari wa jeshi.Tuliongea sana kutokana na nilivyomweleza historia yangu,basi kesho yake asubuhi alinifata akaniambia nimfate akanipeleka kwa mkuu wa kambi ofisini kwake,nilimweleza pia Mkuu wa kambi.

Mkuu wa kambi alifurahi sana na akasema anapenda watu majasiri kama mimi,basi akaniambia kwamba kuna usaili unakuja siku sio nyingi hivyo niandae vyeti vyangu na taarifa zangu kwa ajili ya usaili kwa sababu alinipa nafasi ya upendeleo.

Kumbuka wakati huo tunaenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hatukwenda na vyeti,hivyo ilinilazimu kuwasiliana na shule nilyomaliza kidato cha nne ambapo kulikuwa na mwalimu aliekuwa karibu yangu sana,kiukweli alinisaidia sana mpaka nikapata vyeti(cha kuzaliwa na kidato cha 4),kuhusu cha kidato cha sita(6) niliprint matokeo kwa sababu yalikuwa tayari yametoka.

nilifanya usaili na taasisi moja inayohusiana na ulinzi walinichukua ,tulikwa 12 kambini kwetu ,baada ya mafunzo pale tulienda kozi nyingine na kumaliza,ndipo nilipojiunga na chuo kikuu MUHIMBILI kwa masmomo ya udaktari,na kufanikiwa kumaliza na sasa ni daktari nipo hospitali ya Arusha.

SAFARI YA KUMTIBU MAMA

Baada ya tu ya kuwa daktari,nilienda kumtafuta mama yangu kipenzi,nikamchukua na kumpeleka hospital nchini India, na kufanikiwa kumtibu kabisa ugonjwa kichaa alichokuwa nancho, na sasa ni mzima wa afya na nina ishi nae.

FUNZO: Tujitahidi kuziishi ndoto zetu,tusikatishwe tamaa na changamoto za dunia, tutumie changamoto kama fursa katika kufanikiwa katika maisha.

Mimi Dkt.Amina (Arusha)
Nina maswali:
1. muhimbili ulisomea udaktari wa nini?
2. India, ulimpeleka mama kwa gharama za nani?
3. Wakati unampeleka mama India alikuwa bado kichaa?
4. Karibu nyumbani Njiro H77 tubadilishane mawazo
 
nimeanza drs la 7 mwaka 2003
nimemaliza drs la 7 mwaka 2009
nimeamaliza kidato cha 6 mwaka 2015,
nimemaliza intern 2021,kazini nimeingia 2021
Hongera, kumbe ma dr mnalipwa vizuri, umeanza kazi 2022 ushapatq hela ya kumpeleka mama india ndani ya miezi?, God is good.
 
Wewe ni liongo liongo umetunga uongo. Huo ukichaa mara nyingi huwezi kutibu eti India. Halafu kingine eti ulipata nafasi ya jeshi mara eti chombo cha ulinzi, mara eti interview mara unafanya kazi arusha, yaani utunzi wako wa kitoto.
Ana Mungu wake wa pekee inaonesha hakuna alipo kwama chekechea hadi kazini na ndani ya miezi 7 akiwa job akaweza kwenda mpaka india. Ma dr wameanza lipwa vizuri.
 
Kuna kitu sijaelewa hapa. Umezaliwa 1997, shule umeanza ukiwa na miaka 7 hapo ni mwaka 2004. Ukijumlisha miaka 7 ya shule ya msingi inakuwa shule ya msingi umemaliza 2011. Ongeza miaka minne ya O-level inakua 2015. Jumlisha miwili ya A-level inakua 2017. Degree ya udaktari inatolewa miaka mitano ambapo kwa hesabu mwaka huu 2022 ndo ulitakiwa uwe mwaka wa mwisho wa masomo yako ya udaktari. Hapo bado hujafanya internship kwa mwaka mmoja. Naomba nifafanulie hapo Mkuu.
Mambo ya data statistics n connecting dots! Watu mko makini! Hakuna kulishwa matango pori
 
kuwa mkweli basi?
wewe ni Manka au Amina?

katika uzi huu post #4 ulikiri kuwa wewe ni Manka na ulikuwa kahaba na ukabahatika kuwa dereva wa Ikulu.
huku unajiita Amnina wa Itilima.
Ukiwa muongo jitahidi iwe una kumbuka kuwa jana uliongopa kitu gani mdada
Fukua babaa! makaburi ya kalee! Maana hayanuki! Kuna mtu alikuwa anaandaliwa kupigwa hapa!
 
nashukuru sana
Kama kitu hakikuhusu andika umecopy sehemu, au uliandika uonewe huruma? Mara dr amina mara manka kahaba, jf sio sehemu ya kutupia ujinga ujinga kuna watu wengi wanasoma hapa. Na ukiwa muongo kuwa na kumbukumbu, sasa umejisikiaje watu wanavyofukuwa uongo wako?
 
Unapigilia misumari mirefu mama🤣
 
Kitu alisahau ni kuwa jf makaburi ya kale huwa hayafutiki, jf inatunza kumbukumbu. Alipaswa kusajili I'd mpya, japo kufikia hadhi ya jf expert member ingemchukua muda. Na kwenye jukwaa la stories of changes hufuatilia mada zako za nyuma,hushindi kirahisi tu kwa uongo wa kutunga
 
na kumbuka pia,sio kila aandikacho mtu humu humuwakilisha yeye,vingine huwakilisha wasiopo humu

nashukuru kwa kushiriki mjadala.
 
Back
Top Bottom