Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Chadema ndiyo chama kinachoongoza kuwa na wendawazimu wengi.

Sasa wewe njaaa kali na mwenzako yericko mdandia nasaba ya nyerere nani awape Ruksa ya kwenda kutia najis bunge la jamhuri ya muungano??

Lakin kwa kuwa chama chenyewe ni cha wehu may be wanaweza kukutizama kwa jicho la kukuzingatia.

Ila inshort huwezi kuingia bungeni we pimbi.

Labda huko huko kwa Bavichaaa wenzako.

wewe pia ulitoka kwenye hiki chama cha vichaa,ulitibiwa wapi ukapona mkuu
 
Huyu jamaa anauwezo mkubwa kujenga hoja. Tumuunge mkono.
 
mbona zitto aliposema kama haya aliyosema ben aliitwa msaliti?
Zitto alipotangaza nia ya urasi akaitwa msaliti ila kwa ben kwa sababu ni mchaga mwenzenu anaitwa kamanda na amefanya maamuzi sahihi!
 
wewe pia ulitoka kwenye hiki chama cha vichaa,ulitibiwa wapi ukapona mkuu

Teh teh teh

Mkuu mimi sijawahi hata siku moja kuwa mshabiki wa hiki chama cha hawa Vichaa wakabila na wadini hata siku moja.

Si unaona wao ubunge wanatangaza nia zao Jamii Forum.

Teh teh teh

Kama sio uwendawazimu tuite nin

Tokea lin nia ya kugombea ubungeni ukaitangaza Jamii forum.

Teh teh teh

Hawa bado kuokota makopo tuh
 
mbona zitto aliposema kama haya aliyosema ben aliitwa msaliti?
Zitto alipotangaza nia ya urasi akaitwa msaliti ila kwa ben kwa sababu ni mchaga mwenzenu anaitwa kamanda na amefanya maamuzi sahihi!

Wachaga wna akili sna.

Lakn hawa wachaga wa chadema ni wendawazimu.

Sijapata kuona.
 
politics.jpg
 
Ben Saanane, nakutakia mafanikio mema you are a great asset but I question myself if you have to be in that parliament now #whoAMI ?

"Be sure you put your feet in the right place, then stand firm."
Abraham Lincoln
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana watu wako tayari kufia CCM. kwa mawazo yako na utaifa ulionao ungesha pewa UKUU WA WILAYA kwani tunashuhudia zinahongwa tu. MAANA SHIDA YAKO WEWE NI HELA ZA FASTA FASTA TU. HUKU CDM UBUNGE MNAENDA PIGANA JUJU TU.

BTW HILO JIMBO UNALOENDA ,,WAMEKWAMBIA WENYE NALO WAMELICHOKA.

DAHHH. KILA LAKHERI BANA BILA SHAKA UKOO WAKO UMEIAFIKI HATARI HII KUBWAA MBELE YAKO.

Pesa za fasta fasta kivipi Mkuu??

Kamaliza his First Degree 2005, Masters 2008. He is on his 30's now kama ni hiyo hoja yako ya pesa huoni ni wakati sahihi wa yeye kupata pesa?? Au unataka azitafute akifika umri wa kina Le Mutuz??

Lakini kwa tunaomtambua Ben tunajua nini ataenda kukifanya Bungeni.. Twende na Ben !
 
Sielewi ni kwanini tunadhani mtu kuwa bungeni ndiyo nafasi ya muhimu sana ili kulisaidia Taifa lisonge mbele! Mie hii haijawahi kuacha kunishangaza. Hivi wajenzi mahiri wa nchi ni wanasiasa tu?

Swali zuri sana hili... Ila nadhani lianze kujibiwa na CCM kwanza. Kwanini Ridhiwani Kikwete ni Mbunge?? Kwanini January Makamba ni Mbunge?? Kwanini Mnauye ana kile cheo pale Lumumba?? Kwanini wanasiasa wengi wakongwe wa CCM wanarithisha watoto wao vyeo vya kisiasa??

Lakini, ni kwanini kwa kijana wa CDM/UKAWA akitangaza nia inakuwa nongwa?? Eti anaenda kuchumia tumbo kwenye siasa?? Ina maana hao wa CCM wao wanafuata nini?? Au hii nchi mnataka muiongoze wenyewe??
 
“Naelekea Bungeni”

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 O'Hara's ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata
Kamanda Ben, nakushukuru sana kwa kujionyesha waziwazi, tupo pamoja kiongozi tumeteseka sana makamanda wenzio kwa uzushi ulioenea juu yako na ACT
 
Hongera sana comrade Ben Saanane kwa uamuzi sahihi Kwa muda mwafaka ninakufahamu long time and am certain u can.
Kupitia uzi wako huu niwaombe wanachadema pamoja na mashabiki wake punguzeni jazba, kejeli, umbea na maneno ya mtaani. % kubwa ya wanachadema ni vijana sasa kijana ukiwa na tabia za kinafiki za kuropoka vitu usivyokuwa na uhakika navyo ni dalili ya kuwa mchawi uzeeni. Angalizo hili nalitoa kutokana na tangazo lako kupitia ule uzi mwingine kama umepitia pole ndo changamoto za siasa uchwara. Ukisoma ule uzi unapata picha kwamba kuna uwezekano hata Zitto anasingiziwa tu.

Otherwise all the best
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa vijana umefika xio vijana taifa kesho wakati wa kumng'oa mkoloni mweusi umefika !
 
“Naelekea Bungeni” Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla. Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo; Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo; Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla. Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo. Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba. Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics). Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi. Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa. Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza! Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu. Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali. Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma. Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili. Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana. Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu. Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie? Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni. Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla. Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1). Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata
Safi Sana..Lumumba wake jadili elimu yake km walivyokuwa akiongea upuuzi kuhusu bavicha.Ndio maana ayatoullah alikuwa akipite hivi kila akiiona hii sura.
 
Back
Top Bottom