Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

“Naelekea Bungeni”

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ‘’Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)’’ yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni ukaguzi na udhibiti mzuri wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge na DED

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la “Naelekea Bungeni” linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata

Hongera sana, thats the spirit, keep it up, usirudi nyuma. Tunahitaji viajana kama wewe kuwakwamua wa Tanzania toka kwenye dimbwi umasikini ulio kithiri, uliosababishwa na viongozi mafisadi na serekali dhaifu
 
Mkuu CV yako kwa upande mkubwa inaonyesha utumishi wako wa Chadema. Mimi nina swali moja tu. Ningependa kujua CV yako outside chadema. Kitu gani amabacho unajivunia umeki accomplish na kina social impact kwa jamii yako iwe ni mtaa unaoishi au kijijini ulipotokea. Maana hiki ndo kitakuwa kipimo halisi cha uzalendo wako. Umeshawahi kujaribu kuwatumika wananchi kwa namna moja au nyingine nje ya siasa? Je una rekodi yeyote ya kazi za kujitolea katika jamii?

kwanza unajaza server kwa kunukuu mhabari wote. Pili ulitaka achimbe barabara na wananchi?
 
Teh teh teh

So anawaongopea ana phd??

Teh teh teh

Yale yaleee kama yule mwehu yericko eti anasema ni CEO wa kampuni

Teh teh teh

Kumbe ni mchumia tumbo tuh na mpiga ripu.

Teh teh teh

Wachaga wa chadema kweli wamevurugwa.

ukiambiwa uvae bomu ukajilipue kwenye mkutano wa cdm utafanya hivyo? Fanatic!
 
Kabla hujagombea ubunge,umewafanyia nini wananchi cha kuwashawishi wakuchague?
 
Hongera sana comrade Ben Saanane kwa uamuzi sahihi Kwa muda mwafaka ninakufahamu long time and am certain u can.
Kupitia uzi wako huu niwaombe wanachadema pamoja na mashabiki wake punguzeni jazba, kejeli, umbea na maneno ya mtaani. % kubwa ya wanachadema ni vijana sasa kijana ukiwa na tabia za kinafiki za kuropoka vitu usivyokuwa na uhakika navyo ni dalili ya kuwa mchawi uzeeni. Angalizo hili nalitoa kutokana na tangazo lako kupitia ule uzi mwingine kama umepitia pole ndo changamoto za siasa uchwara. Ukisoma ule uzi unapata picha kwamba kuna uwezekano hata Zitto anasingiziwa tu.

Otherwise all the best

Bwana mdogo, bezikale nikupongeze kwa kuungana na maamuzi ya mate yako.
Ben yuko humu muda mrefu na alikuja mwenyewe akakili kuwa alikuwa anaisaliti CHADEMA akiwa chini ya kiongozi wao zitto, alivoona usalti ule ungempeleka kubaya akaenda kuomba msamaha na apewa na uongozi halali wa chama.

Lakini kikubwa, niungane na wewe kumpongeza kwa dhamira ya hiyo kuwatumikia wananchi.

Kuhusu zitto, ufahamu tu kuwa hajaonewa, alichokifanya ni usalti usiovumilika, binafsi nilianza kupata wasiwasi tangu alipoacha kuonekana majukwaani katika operations kadhaa.

Kule CCM kuna vijana wazuri tu japo wanapelekeswa na mfumo uliopo, yupo Mpina, Deo etc. Tunaposema ccm haifai ni kwakuwa viongozi wake wapo too corrupt and selfish, ccm ingekuwa inatimiza wajibu wake ipasavyo kwa nchi nani angipinga?

Go Ben go.
 
Last edited by a moderator:
ukinyimwa hiyo fursa ndani ya chama utaendelea kukijenga chama kiroho safi na kutumikia wananchi kupitia fursa nyingine??
 
well said shardcole...hebu muulize tena kuyu habari ya mujini wakati wenzake kina Sanane wanaandika proposal wakafanye PhD yeye anakuwa anafanya nini??? kwani hizo fursa haziwahusu wao wazee wa buku saba saba?

tanzania mpya tuitakayo haina room ya kulipa wanamipasho kama huyu anayejiita habari ya mujini...tunataka kila mtu anayepokea mshahara na awe na mchango kwa taifa....hawa kina habari ya mjini ndio hasa wanaodidimiza uchumi...mnakuwa na kundi kuuubwa la matapeli hawafanyi uzalishaji wa aina yoyote ile....[h/QUOTE]

Ni sawa na kumtukana baba yako baada ya kukusomesha eti kisa umeshaelimika....
 
nakukubali na niko tayari kuchangia hela taslimu ili kuwezesha mchakato wako , sina mashaka na wewe .
 
Kila la kheri kamanda, wasaliti walisema unahamia kwenye lichama lao la m@shoga
 
Yericko Nyerere naye anataka akagombee ubunge? naamini chadema kuna wazee wenye busara hawataruhusu jambo hilo. huyu bwana ambaye siku zote ana desa materials ya watu anafanya plagiarism anakuja kubandika hapa akijifanya ya kwake na kuandika hbr za uzushi uzushi kila wakati kuchangamsha JF anataka akawe mbunge? huu ndo mwanzo wa yeye kuhama cdm maana wakimtaka tu jina lake anahamia ACT au CCM na mtakuja kunambia hapa. ila ki ukweli mwaka huu wananchi msichague wabunge aina ya ya ashumpta,kibajaji,sugu,yule aliyekuwa mtangazaji,yule wa morogoro et al. hawa ndio kikwazo cha maendeleo ya taifa hili. yericko wachen awe anakuja hapa jf anapiga porojo zake siku zinaenda. muda si mrefu utasikia na said mohamed anataka kugombea urais au ubunge wakati hawa ni waburudishaji wa JF.... hata yule KJ malecela naye atataka ubunge.
 
Last edited by a moderator:
Bwana mdogo, bezikale nikupongeze kwa kuungana na maamuzi ya mate yako.
Ben yuko humu muda mrefu na alikuja mwenyewe akakili kuwa alikuwa anaisaliti CHADEMA akiwa chini ya kiongozi wao zitto, alivoona usalti ule ungempeleka kubaya akaenda kuomba msamaha na apewa na uongozi halali wa chama.

Lakini kikubwa, niungane na wewe kumpongeza kwa dhamira ya hiyo kuwatumikia wananchi.

Kuhusu zitto, ufahamu tu kuwa hajaonewa, alichokifanya ni usalti usiovumilika, binafsi nilianza kupata wasiwasi tangu alipoacha kuonekana majukwaani katika operations kadhaa.

Kule CCM kuna vijana wazuri tu japo wanapelekeswa na mfumo uliopo, yupo Mpina, Deo etc. Tunaposema ccm haifai ni kwakuwa viongozi wake wapo too corrupt and selfish, ccm ingekuwa inatimiza wajibu wake ipasavyo kwa nchi nani angipinga?

Go Ben go.

Naona ukisikia tu jina la zitto unachanganyikiwa tulia siasa siyo ugomvi, umemtuhumu kuwa msaliti kwa maneno ya mtaani lakini anaendelea na harakati zake tena kwa spidi kali. Kwa taarifa yako hoja yangu kubwa haikuwa zitto ila lugha za kejeli toka kwa wanachadema zisizokuwa na vyanzo vya uhakika, watu hawatafuti ukweli ila wanafuata upepo na uzi niliokuwa nauzungumzia ni huu https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=832543 . Fanya ulinganishi wa michango ya wadau kwenye huo uzi na huu unaoendelea. Kama Ben alikosea 2012 akasamehewa je hizi lugha kumwita tena msaliti 2015 zinatoka wapi?

Picha mnayotoa ni kwamba kuna uchafu mwingi ndani ya chadema ila hausemwi hadi mtu atangaze kuhama.
 
Back
Top Bottom