Nimefanya ujinga jana ambao hadi sasa najilaumu

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Salute guys.

Wakati mwingine mtu unaweza fanya upuuzi halafu kila ukikaa kutafakari uliwaza nini inabaki majuto.

Usiku wa jana nikiwa eneo moja na jamaa kadhaa wakati nimeegemea meza kwa nyuma kuna mbaba wa kituruki nafikiri, alikuwa anapita. Unajua ile mtu anapita nyuma yako wewe umeegemea meza umeangalia mbele. Nilichokifanya nikasogeza mguu wangu kidogo kwa nyuma makusudi ili nimkwae(nimpige kangwara.) Aisee baba wa watu aliyumba kidogo aende chini.

Ni eneo ambalo watu walikuwa wengi. Jamaa zangu wote walicheka. Fasta nilijifanya kumuomba radhi. Ili hali kabisa kiakili ya kawaida kila mtu alijua nimefanya kusudi. Mbaba wa watu alisepa tu kinyonge akiwa hana la kufanya.

Kiukweli naonekanaga mstaarabu sana. Sasa kwa ule upuuzi yaani ni kama bado najuta. Nawaza nimtafute nimuombe radhi tena.
 
Upo katika crew ya attention seekers na bullys.

Unatamani upate approval ya crew yako.

Umekua tayari kuhatarisha another individual's welfare ili kupata approval kutoka kwa crew yako.

Kicheko chao ni saini ya approval. Ulienjoy for a moment ila the real you anakufanya uwe kwenye dilemma kwa ulichofanya.

Anyway sijala bado probably ni njaa zimefanya nione hivi.
 
Salute guys.

Wakati mwingine mtu unaweza fanya upuuzi halafu kila ukikaa kutafakari uliwaza nini inabaki majuto.

Usiku wa jana nikiwa eneo moja na jamaa kadhaa wakati nimeegemea meza kwa nyuma kuna mbaba wa kituruki nafikiri, alikuwa anapita. Unajua ile mtu anapita nyuma yako wewe umeegemea meza umeangalia mbele. Nilichokifanya nikasogeza mguu wangu kidogo kwa nyuma makusudi ili nimkwae(nimpige kangwara.) Aisee baba wa watu aliyumba kidogo aende chini.

Ni eneo ambalo watu walikuwa wengi. Jamaa zangu wote walicheka. Fasta nilijifanya kumuomba radhi. Ili hali kabisa kiakili ya kawaida kila mtu alijua nimefanya kusudi. Mbaba wa watu alisepa tu kinyonge akiwa hana la kufanya.

Kiukweli naonekanaga mstaarabu sana. Sasa kwa ule upuuzi yaani ni kama bado najuta. Nawaza nimtafute nimuombe radhi tena.
Hahahah!! amekuachia laana ya kituruki na haitokuacha daima..
 
Sijaelewa hio meza ilikuwa wapi bar au wapi na huko kuegemea meza kukoje yaani me sijapata picha Bado ya hi scenario
 
Back
Top Bottom