Blessingmore
JF-Expert Member
- Jun 14, 2016
- 377
- 394
Sawaa senetor wa mtwiz
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Guest atalipia coz atakuwa ameweka budget ya kugegeda. Ukipanga kugegeda lazima budget yako iwe na;Tatizo ni umasikini ila kibinadamu umekosea sana. Sio kwamba alikua anataka umlipie ila ni utamaduni tuliojijengea. Sasa umeshindwa kulipa 400 gesti utaweza lipia?
Seneta mwenyewe ndo walee ambao ajiraa badoo Magu hajaamuaa....ukutee alikuwa na ileile bukuuTatizo ni umasikini ila kibinadamu umekosea sana. Sio kwamba alikua anataka umlipie ila ni utamaduni tuliojijengea. Sasa umeshindwa kulipa 400 gesti utaweza lipia?
Chinga anamahesabu ya Sh.600/=Huyo nae boya,kumlipia mtu sh 600 kuna ubaya gani?
Fala sana huyo.Chinga anamahesabu ya Sh.600/=
Nili kumiss sana Seneta Wa Mtwiz
kumbe anatokea kskzn......!!!!!!!Wakuu,
Hii ime_happen leo.
Kuna dada mmoja nilisoma na'e ngazi fulani ya elimu,
Tangu tumemaliza umepita muda mrefu hatukuwahi kuonana.
Sasa leo tumekutana kwenye daladala 1 la *t/segerea-simu2000*.
Ingawa hatukuzoeana sana kipindi tunasoma,
Leo huyu dada alionekana kufurahi sana kuniona.
Kwa kuwa tulikaa siti 1
Tukaanza kupiga stori kadhaa za kitambo,
Na kuulizana kuhusu wana wengine ambao tulisoma nao,
"Hivi _masalago_ yuko wapi?"
"Halafu nilidhani kuwa *seneta* umesharejea mtwara."
Na unajua kuwa yule _christopher maila_ wa kigoma anafanya kazi sehemu fulani?
Hivi yule _john nguchiro_ wa kuuza madesa yule huwa namwona fb sana,
Una mawasiliano na'e yule?"
"Ila _*seneta wa mtwiz*_ una mwili ya ajabu,
Yaani bado kamwili kembambaaaaaa!!!!
Hunenepi hata kidogo!!!"
Tukacheka kiutani
Na stori zingine kibao kama hizo.
Akashika simu yake
Akaniambia
"Halafu *seneta* naomba unipe namba zako za simu zote kabisa,
Ya airtel na ya tigo."
_____
Sasa ile naanza kumtajia
"0786 ........."
Kabla sijamalizia,
Kikafika kile kipengele cha *ndugu konda* kuhitaji nauli katika siti yetu.
Pamoja na kuwa miye nilikaa upande wa dirishani kabisa,
*konda* akanyoosha mkono hadi upande wangu kuhitaji hela ya nauli.
Nikajisachi mfukoni nikatoa 1,000/= nikampa konda
Halafu nikanyoosha kidole kimoja ([emoji121])
Kuashiria akate nauli ya mtu mmoja,
Kisha anirudishie 600/= yangu.
Yule konda akaniuliza kwa msisitizo,
"Blaza wangapi?"
Nikaonesha tena kwa kidole ([emoji121]).
Akaniuliza tena
"Au nikate ya wawili?"
Nikamkazia konda,
Nikamjibu,
"Wewe konda
Tuheshimiane!
Nimekwambia kata ya mtu mmoja,
Lete chenji hapa!
Eeeeeeeboh!!!!"
Watu wote wa jirani wakawa kimya wakitucheki kwa kuibia.
Konda akanipa tiketi na 6,00/= yangu,
Nikapokea,
Nikaweka mfukoni!
Nikatulia.
______
Yule dada akionekana kuwa na donge kali limemkaa rohoni,
Akafungua pochi yake,
Akatoa 400/= (ambayo ilikuwa ni sarafu 1 ya sh. 200,
Sarafu 1 ya sh. 100 na
Sarafu 2 za sh. 50) akampa konda,
Konda akapoke na akahamia siti ingine!
*******
Kukawa na kimya kama cha dakika 3 hivi kati yetu,
Zile stori za wana tuliosoma nao na kuniomba namba za simu zikapotea ghafla.
Hapo
Nikimcheki dada amekunja ndita ile mbaya,
Na mashavu yamevimba ghafla mithili ya kobe mwenye mimba!
Nikajifanya kumuuliza kwa upole,
"Hivi unayo namba ya simu ya *ching hyphen* wa _kimara bucha_ yule wa ps yule??"
Dada kimyaaaaa!!!!
******
Muda si mrefu basi likaingia stendi ya *mawasiliano*,
Baada ya kushuka nikamfuata ili tuagane au hata mawasiliano tupeane,
Nikamwambia
"Sasa ndugu naomba namba yako ya ..."
Kabla sijamalizia,
Alisonya kwa nguvu na kunifokea
"Ishia zako kuleee!!!
Tangu lini wamachame na wamakonde wamekuwa ndugu!!
Kwanza usiniharibie siku!!!"
Daaaaaaaaaaaaaaah!!!!
Nikashangaa sana,
Na kila aliye karibu aligeuka kuangalia!
*****
Sasa sijajua nilichomkosea huyu dada nini,
Wakati kabla ya konda kutembelea siti yetu
Tulikuwa na furaha yenye bashasha tele na amani sana!