Jifunafu
Senior Member
- May 25, 2020
- 182
- 693
Wanajamvi Aslam,
Hama baada ya salamu ndugu zangu Ile safari yangu ya kwenda mji wa Mpanda kuona fursa za kilimo imetimia.
Nilipata nafasi ya kutembelea baadhi ya vijiji tofauti tofauti Kwaajili ya kuangalia maeneo, ni kweli natoa ushuhuda kwamba kilimo kimetajilisha watu wengi hususani Mji wa Mpanda na wengi wao wakiwa ndugu zetu wasukuma na wageni kutoka mikoa mbali mbali wanakuja kuwekeza.
Nilibahatika kupitia vijiji vya wilaya ya Mlele na kutembelea na kisha kwenda hadi wilaya ya Tanganyika inayopakana na mkoa wa Kigoma, vijiji kama Mwese na kuona jinsi mapori yalivyojazana huko na mashamba mazuri na mabonde.
Kweli Tanzania ni kubwa na kuwa masikini ni kujitakia wenyewe, wasukuma wanaivisha huko magunia na magunia ya mahindi. Ardhi unapewa hata bure unaweka watu wanafyeka mianzi unalima bure tu, mahindi yanatoka baraa.
Kijijini kilichonivutia zaidi na kuamua kukodi na mashamba ni Kijiji cha Kapanga, ni center iliyochangamka na magari yanasomba mahindi Kila kukicha na wafanyabiashara wamejaa kutafuta mahindi.Kiujumla mpanda ni mji unakuwa Kwa kasi na mabosi wengi ni wakulima.
Vijana tuamkie kilimo na kilimo kinalipa, mambo ya kuzunguka na bahasha za kaki haina maana, mashamba tele hayajawai kulimwa tangu kuwepo kwa dunia.
View attachment 2339026