Nimefiwa na Mama yangu usiku wa kuamkia 19.11.2011 na kuzika jana.

Nimefiwa na Mama yangu usiku wa kuamkia 19.11.2011 na kuzika jana.

Pole uporoto01! Mungu akupe moyo wa subira ktk kipindi kigumu. RIP mama uporoto01! Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
 
Pole sasa Uporoto,Mungu aliye mwingi wa faraja awape amani na awatie nguvu.
 
Kiongozi wangu Broda,
Pole sana mkuu!
Natuma salamu zangu za pole nyingi kwa familia yako kwa kuondokewa na mama yetu!
Naujua uchungu mnaoupitia kwa sasa, lakini Mungu ndiye mfariji wa kweli!
Ndani ya siku kadha atawafuta machozi, na zaidi sana kwa sasa na mnatakiwa kulibariki jina la Bwana, na kukubali aliyoyaamua!
Poleni tena mkuu!
 
Pole mkuu, sote tusafari moja.
Mungu akupe nguvu!
 
Wakuu nimefiwa na mama yangu mzazi aliyekuwa mgonjwa wa kitandani(bedridden) kwa muda wa mwaka na nusu.

A%20S%20cry.gif
Pole mkuu, tunajua una masikitiko na majonzi mno, pole sana.
Ilandio maisha, mzike mama yako nasi tutamuombea, na wewe ujuwe maisha lazima yaende.
RIP mama.
 
Pole sana kwa msiba Uporoto...
Mungu ampumzishe salama mama yako!!
 
Wakuu nimefiwa na mama yangu mzazi aliyekuwa mgonjwa wa kitandani(bedridden) kwa muda wa mwaka na nusu.

Mungu ailaze Roho ya Mama yetu mahala pema peponi.... Amen

Poleni wafiwa wote, Mungu awape faraja
 
Pole sana dia wangu! Nawaombea kwa Mungu afanye wepesi ktk kipindi hiki kigumu cha majonzi na maumivu makubwa. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, tunalihimid jina lake. :grouphug:
 
mkuu tuko pamoja katika wakati huu mgumu....Bwana ampe raha ya milele na mwanga wa milele amuangazie mama yetu na apumzike kwa amani!!!!letu jukumu ni moja nalo ni kumuombea kwa Mungu kwa kuwa alishiriki kifo cha kristo kwa ubatizo basi atashiriki na ufufuko wake nae Kristu ataufananisha mwili wa mama yetu na mwili wake Mtukufu....tusisononeke maana mama yetu amelala usingizi
 
Pole sana ndugu, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.
 
Back
Top Bottom