Nimefuatilia utendaji kazi wa Rais Samia, PM Majaliwa na VP Mpango, huwezi kuamini awamu ya tano walikuwa wamoja na Hayati Magufuli

Nimefuatilia utendaji kazi wa Rais Samia, PM Majaliwa na VP Mpango, huwezi kuamini awamu ya tano walikuwa wamoja na Hayati Magufuli

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Ukilala ukiamka, ukafuatilia uteuzi, utendaji na miradi mkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano, utaona wazi viongozi niliowataja walikuwa wanasali na kuomba JPM atakufa lini ili wafanye yakao.

Ila hawakumbuki kuwa wanaongoza wananchi 60m ambao hawajawahi kuwaomba kura wala kupigiwa kura.

Sasa upepo uliopo mitaani ni tofauti na uliopo maofisini, na hali ya leo bora na jana.

Hayati Magufuli alifanya yake mema na kujenga mifumo dhabiti ya ukusanyaji mapato ya Serikali , awamu hii haijali wala haifuatilii mifumo hiyo na matokeo yako wanyonge wameanza kuishi kama dikidiki ndani ya Tanzania.

Ili kuweka kumbukumbu sawa hata makatibu wa CCM wilayaveasa wanalima hoho makwao kwa kufukuzwa baada ya kufikisha mabox ya kura za wizi kulikotakiwa na watubkupata uongozi.

Umeme na maji vimekuwa bidhaa adimu kuliko kupata bia.
 
Wewe hiyo kodi unayoona hawakusanyi, kipindi cha jiwe ulilipa shilingi ngapi ndugu yangu?.

Wafanyabiashara tulinyanyasika sana kipindi cha rafiki yako mwendazake, tulilimbikiziwa kodi bila hata uhalisia wa biashara tunazofanya ndugu. Alitengenezea wafanyakazi wa TRA sehemu ya kupiga kwa wafanyabisahara.

Mama anafuata utendaji halisi wa serikali na siyo mihemko ya mtu mmoja kuwa ndo sheria ya nchi.

Mbona Meko alikuwa kwenye serikali ya awamu ya nne lakini alituongoza kama ni mgeni serikalini.

Mlikuwa na msemo maarufu ambayo mlikuwa mnautumia '' KILA SHETANI NA MBUYU WAKE" Kila Awamu na mambo yake ila sasa ndo mnaongoza kwa kulalamika kila siku.
 
Kila awamu kuna wanaofaidika na ikija awamu nyingine ndio wanaolalamika.
 
Wewe hiyo kodi unayoona hawakusanyi, kipindi cha jiwe ulilipa shilingi ngapi ndugu yangu?. Wafanyabiashara tulinyanyasika sana kipindi cha rafiki yako mwendazake, tulilimbikiziwa kodi bila hata uhalisia wa biashara tunazofanya ndugu. Alitengenezea wafanyakazi wa TRA sehemu ya kupiga kwa wafanyabisahara.
Mama anafuata utendaji halisi wa serikali na siyo mihemko ya mtu mmoja kuwa ndo sheria ya nchi.
Mbona Meko alikuwa kwenye serikali ya awamu ya nne lakini alituongoza kama ni mgeni serikalini.
Mlikuwa na msemo maarufu ambayo mlikuwa mnautumia '' KILA SHETANI NA MBUYU WAKE" Kila Awamu na mambo yake ila sasa ndo mnaongoza kwa kulalamika kila siku.
Kodi gani ulibambikiwa, sema mmezoea magendo
 
Mnyonge anataka mtoto wake asome elimu bure,maji yapatikane,barabara zijengwe,usalama uwepo na gharama hizo walipie matajiri..wakati hata uzalishaji hamna anaofanya wa kulipa kodi hamna na akiwekewa tozo kidogo analialia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu, awamu hii tunawatumikia wenye mali.
Ukishaanza kuwatumikia wenye mali, hakika huwezi kukusanya kodi.
Ndiyo maana sasa tunakopa kwa kiwango cha kimataifa. Tusipokopa, tutapata wapi fedha za kuendeshea serikali?
 
kwaufupi hakuna waziri mkuu anaefanya kazi kwa raha kama majaliwa.
 
Unaonekana ninamna gani ulivyo mjinga na kutojua ninachokisema, tumepitia magumu mengi sana hadi kusababisha kutamani kwenda nchi nyingine kufanya biashara.
Mungu ametusaidia sana katika hili.
Ndugu kukuza mtaji siyo jambo dogo kama unavyofikilia.
Kodi gani ulibambikiwa, sema mmezoea magendo
 
Ndugu yangu, awamu hii tunawatumikia wenye mali.
Ukishaanza kuwatumikia wenye mali, hakika huwezi kukusanya kodi.
Ndiyo maana sasa tunakopa kwa kiwango cha kimataifa. Tusipokopa, tutapata wapi fedha za kuendeshea serikali?
Mungu ameweka hili wazi.
Kuwa binadamu wote tumeumbwa na Mungu ila Masikini atamtumikia tajiri.
Hata leo uwanaogopa Wamarekani kwa sababu ya utajiri wao.
Yani wewe ambaye huna pesa, mwenye pesa akutumikie? Huko ni kuota ndoto za alinacha
 
Back
Top Bottom