Nimefungiwa njia msaada wa kisheria tafadhali.

kamsongole

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
111
Reaction score
15
Habari ndugu, mimi nilinunua eneo ambalo lilikuwa na barabara ya kufika kwenye eneo hilo. badae akaja akanunua mtu mwingine mbele yangu pembezoni mwa barabara. cha kushangaza huyu jamaa aliyenunua mbele yangu ameziba hadi barabara akidai kuwa ameuziwa kote. nikimuuliza aliyetuuzia kwa nini ameuza hadi barabara anasema yeye hakumuuzia njia na anasema wazi ila jamaa hasikii nifanyeje?
 

wanasheria mko wapi? msaada tafadhali.
 
Njia ni haki ya mtu katika ardhi anayomiliki,nenda mahakamani kwa hilo shauri litasikilizwa na maamuzi yatatolewa ya kumwamuru akufungulie njia aliyoziba
 
Asanteni kwa maoni yenu ngoja niende serikali za mitaa nikashughulikie fasta.
 
Mkuu, Sheria yetu ya Ardhi inatambua haki ya njia( Public Right Of Way) katika kundi la haki za muhimu( siyo lazima) yaani Easement Rights. Msingi wa haki hizi ni utambuzi wa kisheria kwamba thamani ya ardhi inategemea matumizi kwa hivyo kama kuna kitu kinachozuia matumizi ya Ardhi hiyo bila sababu za msingi sheria itakiondoa. Kwa ishu kama yako ni lazima kwanza ithibitishwe kwamba nyote mna haki juu ya vipande hivyo vya ardhi maana easement right haitolwewi kwa mvamizi, pili itabidi kuthibitisha kwamba hakuna namna nyingine ya kupata njia nyingine ( accessibility to land) kama ipo njia nyingine ambayo haitaathiri matumizi basi mahakama itaamuru njia hiyo nyingine itumike la kama hakuna na njia ya awali imetimika toka awali basi mahakama itaamuru aliyefunga njia kuifungua kwa gharama zake. Angalizo muhimu ni kua lazima ujihakikishie kuwa njia hiyo ipo toka awali siyo umeanzisha wewe na kama eneo limepimwa (surveyed land) mahakama itatumia maelekezo ya ramani kutoa maamuzi yaani kama hapo pamepangwa kuwa barabara ataamriwa kuvunja mara moja .
 

Nashukuru sana mkuu, ki ufupi ni kwamba njia ilikuwepo siku nyingi na ilitumiwa na wanakijiji ha hapo. hivi sasa kila mtu anajiuliza imekuwaje afunge njia. but kila kitu kitakuwa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…