Mkuu, Sheria yetu ya Ardhi inatambua haki ya njia( Public Right Of Way) katika kundi la haki za muhimu( siyo lazima) yaani Easement Rights. Msingi wa haki hizi ni utambuzi wa kisheria kwamba thamani ya ardhi inategemea matumizi kwa hivyo kama kuna kitu kinachozuia matumizi ya Ardhi hiyo bila sababu za msingi sheria itakiondoa. Kwa ishu kama yako ni lazima kwanza ithibitishwe kwamba nyote mna haki juu ya vipande hivyo vya ardhi maana easement right haitolwewi kwa mvamizi, pili itabidi kuthibitisha kwamba hakuna namna nyingine ya kupata njia nyingine ( accessibility to land) kama ipo njia nyingine ambayo haitaathiri matumizi basi mahakama itaamuru njia hiyo nyingine itumike la kama hakuna na njia ya awali imetimika toka awali basi mahakama itaamuru aliyefunga njia kuifungua kwa gharama zake. Angalizo muhimu ni kua lazima ujihakikishie kuwa njia hiyo ipo toka awali siyo umeanzisha wewe na kama eneo limepimwa (surveyed land) mahakama itatumia maelekezo ya ramani kutoa maamuzi yaani kama hapo pamepangwa kuwa barabara ataamriwa kuvunja mara moja .