Nimefungua biashara hii week ya tatu tangu tuanze, ila naona imedorora sana

Nimefungua biashara hii week ya tatu tangu tuanze, ila naona imedorora sana

Habari ya mchana wakuu

Nahisi kuchanganikwa hapa, nimefungua biashara hii week ya tatu tangu tuanze, ila naona imedorora sana, pesa iliyopatikan ni ya kulipa watumishi tu,hivi hii ni kawaida kwa biashara yoyote mpya inavyoanza anza au kwangu imenigomea tu.
pambana ndg hapo ndipo unatakiwa kuvuka baadaye utasahau....kama unapata hata ya kuwalipa watumishi wewe umeanza vizuri mnoooo big up
 
Jaribu kutembea kidogo kwa wazee! mjini wachawi wengi nadhani umenielewa
 
Bado mapema Kwa sababu umefungua biashara ambayo ipo tayari na watu walikua wanapata huduma hiyo Kwa watu wengine. Kwa hiyo subili uzoweleke kwanza kama wengine,lakn pia angalia jinsi ya kuongeza thamani huduma unazotoa. Kama akija kunyoa nywele na ndevu wanamtolea bure, weka wadada wazuri wawe wanawaosha vichwa walionyolew na wawapake mafuta,weka na scrubbing maana wanaume nao siku hii wanapenda, .....Kwa hiyo ujibu swali:'kwa nn wateja waje kwangu na si Kwa mengine". Hapo ndo tunaweza kuboresha na kuongeza kipato na sio" na Mimi nimo". Pia biashara yako itakua stable baada ya miezi 6
 
Habari ya mchana wakuu

Nahisi kuchanganikwa hapa, nimefungua biashara hii week ya tatu tangu tuanze, ila naona imedorora sana, pesa iliyopatikan ni ya kulipa watumishi tu,hivi hii ni kawaida kwa biashara yoyote mpya inavyoanza anza au kwangu imenigomea tu.
Una mkataba gani Na wafanakazi wako?
Unawalipaje?
Huduma zinaendana Na bei?

Huduma zilizopo wateja wanazihitaji?
 
Back
Top Bottom