Uchaguzi 2020 Nimefurahi Msigwa kupigwa chini

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Nimefurahi sana aliyekuwa mbunge wa Iringa, Msigwa Peter kuangushwa chini, Alikuwa na dharau sana ukimfata Kumueleza Shida akusaidie kama Mwananchi. Aliutumia ubunge kama Kitega uchumi cha kujinufaisha yeye binafsi.

Jimbo lingine la Ubungo. Alilokuwa analitumikia Kubenea, alilitelekeza mwisho wa siku akalikimbia aliyekuwa meya Boniface Jacob na yeye ilikuwa ukimfata akusaidie kama mwananchi anakukimbia.

Kifupi Wapinzani waligeuza ubunge sehemu ya Kujinufaisha wao binafsi.

Ni wabunge wachache wa upinzani Walikuwa kwa ajiri ya Wananchi.

Heche John , huyu kazi yake ilikuwa ni kupinga tu kila kinachofanywa na serikali.

Mwisho nashukuru Msigwa kupigwa chini, akatulie sasa kwenye Car wash yake aliyowekeza, pia arudi kanisani kwa Waumini aliowatelekeza, Akajifunze sasa na Kauli nzuri.
 
Msigwa kawe mchungaji sasa
 
Ukitaka kujua akili za watu wa CCM angalia wanachoposti humu ndani kinafanana na walichokuwa wanachangia wabunge wao bungeni. jiulize sasa bunge linaenda kutawaliwa na akili kama hizi tunalipeleka wapi Taifa
Kabisa, na hawa sio mashabiki ni viongozi wakubwa tu wanaandika mavi kama haya
 
Msigwa anarudi. Uchaguzi huu utafutwa tu. Mark my words.
 
Watanzania wameamua
Wakolosai 3:2

Nanyi watumwa,watiini mabwana wenu Wa hapa duniani katika mambo yote:

Fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu,wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatizama.
 
Wakolosai 3:2,
Nanyi watumwa,watiini mabwana wenu Wa hapa duniani katika mambo yote:
Fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu,wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatizama.

1Petro 2: 13-17


13Basi, jiwekeni chini ya mamlaka yote ya kibinadamu, kwa ajili ya Bwana: utii kwa mfalme aliye mtawala mkuu,
14utii kwa wakuu wa mikoa ambao wameteuliwa naye kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema.
15Maana Mungu anataka mweze kuyakomesha maneno ya kijinga ya watu wasio na akili kwa matendo mema mnayofanya.
16Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu.
17Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme.
na, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
 
Lofa tu wewe mijitu mipuuzi ya Iringa hasa mizee ndio mishabiki ya huyo bibi
 
Msigwa kawe mchungaji sasa
Yaani unafurahi Msigwa kushindwa ubunge kwa sababu tu hakukusaidia! Kwani hapo ulipo huna miguu na mikono ya kufanyia kazi?
Huna ndugu wa kuwaomba huo msaada? Wewe ni yatima? Au ni mtoto aliyeokotwa jalalani?

Na akili yako hiyo ya kuwaza kusaidiwa tu, unategemea huyo Msigwa atapungukiwa nini kwa kuukosa huo ubunge alioutumikia kwa miaka 10 mfululizo! Na kwa kuukosa tu huo ubunge, unatarajia hizo shida zako zitafikia tamati sasa?

Kijana, jifunze kujitegemea na pia kutafuta kwa jasho. Hata ningekua mimi ndiye huyo Msigwa, ningekufuzia mbali. Muda wote unashinda kijiweni, halafu unataka mwanaume mwenzako akusaidie! Hovyo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…