Nimefurahia maamuzi kesi ya Mbowe, Mungu mkubwa atatenda

Nimefurahia maamuzi kesi ya Mbowe, Mungu mkubwa atatenda

Jaji amezawadiwa cheo baada ya kuvurunda kesi , ni maajabu ya Dunia Only Tanzania yanatokea. Haya
 
Acha ujinga wewe,unakremishwa na wazungu maupumbavu nawe unakariri!!
Wewe ukiwa adui wa Mungu je, yeye atakupenda??
Kwanini asikupende na akaishi nawewe paradiso maana yeye anaupendo mkuu kuliko binadamu?
Nikikubaka utanipenda na kuniombea mema daima???
Tumia akili usijazwe upupu kichwani ukaongeza idadi ya mazuzu nchini
Povu jiiingi for nothing. Sasa si ukawaue hao watesi wako ili usiendelee kupata depression mbona unalalamika tu humu. Usipende kutukana bila sababu kwani kutukana ni dalili ya ujinga na kutojiamini.
 
Wewe nafikiri umeingiliwa na ushabiki wa kipuuzi . Umpotezee mtu muda na uelekeo kuwa kama hana hatia ataachiwa !! Seriously ?! . Unyanyasaji kwa wapinzani ktk nchi za ki communist haujaanzia leo na Tz tu. Ni vitu vya kukemewa visiote mizizi. Magu kanyanyasa watu leo yuko wapi ?!. Tunatendeana haya ili tuende nayo wapi ?!

Itikadi zetu zisitupofushe na kulewa madaraka
Mbowe naye alimnyanyapaa Zito, akamnyanyapaa Dr. Slaa na yeye Mbowe leo yupo wapi?
 
Off point
Shusha pressure kijana utazeeka kabla ya wakati wako. Mahakama huwa haipangiwi cha kufanya inafanya kulingana na sheria. Huyo mbowe si Mungu kwamba hawezi kukengeuka na kufanya mambo maovu. Acheni mahakama ifanye kazi yake vinginevyo mtateseka sana na mwishowe mtaambulia vidonda vya tumbo.
 
😁😁😁
AIgmal.jpg
 
Povu jiiingi for nothing. Sasa si ukawaue hao watesi wako ili usiendelee kupata depression mbona unalalamika tu humu. Usipende kutukana bila sababu kwani kutukana ni dalili ya ujinga na kutojiamini.
Kama unaujinga usiambiwe ukiambiwa umetukanwa?
kulipa kisasa ni haki na usipotaka kulipa ukamwachia Mungu akulipie au vinginevyo nihaki pia!!
Kulazimisha kuwa kulipiza kisasi ni dhambi ni ujinga na upuuzi mloambiwa na wazungu wenu ili mnyonywe vizuri. Grow up kimwili na kiakili bwamdogo
 
Sabaya amehukumiwa kwa ukatili alioufanya na ushahidi wa dhahiri upo, Mbowe anakomolewa maana haisujudii serekali. Hakuna anayesema mahakama ni huru. Usidhani hatujui tofauti ya hizi kesi mbili na uhuru wa mahakama.
Sa
wa Sabaya haki imetendeka na mahakama ni huru. Kwa Mbowe haki haijatendeka na mahakama siyo huru. What a double standard!

Wakiguswa wengine mnanyamaza, akiguswa gaidi mnataka sote tumpiganie eti wakimalizana nao watakuja na kwetu!
 
Kwakua Sabaya kafungwa, hata huyu ni lazima atafungwa tu. Mngeonekana wa maana kama msingesema kuwa mahakama inafanya kazi yake vizuri baada ya Sabaya kufungwa ila kwasasa mnaonekana wanafiki, inawezekanaje mahakama hizohizo nzuri (kama mlivyodai) leo zionekane mbaya kwakua zimemshikilia mbowe?
 
Kwahiyo kwakuwa sabaya kafungwa ni lazima na mbowe afungwe hata kama hana hatia?
Ndo msubirie sasa ili tuone kama ana hatia au hana.

Hivi inakuwaje mseme mahakama haifanyi kazi yake vizuri, akati juzi tu hapa mmetoka kuisifia kuwa iko njema baada ya kumfunga Sabaya?

Sheria ni msumeno.
 
Tulianza awamu ya tano tukapiga makofi wapinzani walipofilisiwa na kufunguliwa kesi tukiamini tunakijenga chama. Tulipomalizana nao tuliamia kwa wana CCM nakuwachapa kuanzia kwenye fikra Hadi kwenye akaunti zao. Leo Wana CCM wote waliokuwa na nguvu ya kiuchumi wamefilisika, au wamekufa kwa presha na baadhi wamepoteza madaraka.

Kwanini yamewapata hayo? Ni kwa sababu waliamua kuishi maisha ya Mwenye nchi badala ya kuishi maisha yao. Wapo watu kwa uzembe kabisa bila kujali elimu zao waliumizwa kisa tu wanamwelekeo na mawazo tofauti. Lakini pia wapo watu walitumia nguvu za kibinadamu na dola kutesa wengine wakiamini zamu yao itadumu Sana. Pole kwao maana Mungu alipangalo si la wanadamu.

Tukamaliza harakati za awamu ya tano, walioamini wapo salama wakageuziwa kibao nakuondolewa kwenye nafasi zao Kisha kukalishwa kimya. Kwa frastration wakanzisha Hadi madarasa ya uongozi na wengine kujifanya wataalamu wa afya kupinga chanjo ya COvID19 lakini leo wote wamenyamazishwa na wanatakiw kuongea lugha moja na waliyedhani Hana nguvu.

Lakini ni Jambo kubwa kwamba unapopanga kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake, unapotumika kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake. Akina Rwegamalila waliishi utumwani kwa uvumilivu wakiaminishwa kwamba hakuna namna wanaweza kurudi uraiani lakini Leo wale wote waliokuwa wanawakandamiza awapo kwenye nafasi zao na wengine hata Duniani awapo.

Wapo watu wachache Sana nimeona wanashangilia maamuzi ya kesi ya Mbowe, lakini madhara ya maamuzi haya Ni makubwa Sana kwa wanyonge wa nchi hii. Ninaposema wanyonge simaanishi kwamba watu wasio na fedha Bali namaanisha wale wote ambao maamuzi haya yanawaruhusu kuteswa na dola na bila kuhojiwa. Mfano mkubwa ni utata wa kifo Cha dreva wa kampuni ya Dangote ambapo maelezo ya Polisi yaliyotolewa kila mtu ameyatilia mashaka lakini kile walichotamka Polisi ndicho kinachoishi.

Siyo hayo, tumeshuhudia machinga wakijaribu kufanya fujo karikoo lakini uongozi wao leo wamejitokeza na kusema wale siyo machinga bali Ni wahuni na imepita hivyo. Usidhani Kiongozi wa machinga anappsema Yale aliyoyasema hajui ukweli wake Bali ndivyo amabvyo tunaishi. Kwamba Mwenye kusema hiki ni sawa na si sawa ni serikali.

Niseme wazi kwamba tunaposhangilia maamuzi ya Jaji ambayo hayana hata kifungu Cha sheria kinachoonyesha msingi wa maamuzi yake Basi tutambue kwamba hii siyo huku ya Mbowe. Ni hukumu yakuigwa na mahakama zetu nyingi nchini. Tukumbuke ipo siku Kama ilivyozoeleka kwa miaka mitano viongozi na watu wenye ushawishi ndani ya CCM ambao Sasa hivi wanaona dola na mahakama Wana ndoa nzuri ndoa hiyo itawaathiri wao na famililia zao.

Nimalizie, Makonda aliteuliwa na JK kabla yakuteuliwa kuwa RC na JPM. Lakini ni Makonda huyo huyo wakati anataka kuonyesha ana nguvu alisau mambo yote Jk na familia yake waliyomfanyia na kumtangaza Riz one kwenye skendo za madawa ya kulevya bila hata kutoa ushahidi wowote. Lakini pia wazee wa CCM wasiwe wepesi wa kusahau namna ambavyo wao na familia zao walinyanyasika, mateso waliyopata hayakuzongatia tuhuma zilizothibitika Bali yalijikita kukomoa.

Maamuzi ya Jaji Siyani ambayo yanafuatia uendeshaji wa kesi huku muda wa Azana kesi ikiwa inasimamishwa kumheshimu Mungu itufumbue macho kwamba hawa watu tunaowashangilia ndio hao hao wanaotafuta kututawala wanapokuwa mafichoni au sirini. Tufurahie maana tunamwona Mbowe akiwa anapita mateso lakini naamini vijana waliopo naye kwenye kesi wana wazazi kama ambavyo qatoa maamuzi Wana wazazi.

Tukumbuke Kama baba Riz alivyoumia mwanaye kutajwa kwenye madawa ndivyo wazazi, mke na watoto wa watuhumiwa wanavyoumia wanapogundua muda wakusubiri vijana wao wawahudumie watu wachache ambao Sasa hivi usiku huu wapo wanastarehe na familia zao, wanaitwa Dad na Mom, wanaulizia mshahara utatoka lini wameamua bila sababu yoyote kuakikisha kwamba vijana wale wanateseka na may be wanakufa ili wao malengo yao yatimie.

Mungu aishiye anaweza akanyamaza kwa machozi ya familia hizi kwa muda ila atonyamaza milele. Tunaposherekea ushindi uluotolewa na Jaji leo Ni vyema pia tukaandaa nafsi zetu kupokea maamuzi ya mwenyenzi Mungu dhidi ya watuhumiwa na waliosababisha wapate mateso wanayopitia Sasa.

Niwatakie sherehe njea, bia ziendelee kuwa tamu kwenu lakini pia muda wa majonzi utakapowadia tuwe tayari kuupokea. Hongera wote tunaofurahia ushindi mkuu.
Tulizana wembe una makali sehemu mbili, hata wewe kuna sehemu utaumizwa kufidia uwazayo moyoni mwako ya kishetani
Si.lazima yawe ya serikari hata yako katika maisha yako tu.
Ukihisi una makosa hapa duniani basu ujue wewe sio binadamu.
 
Back
Top Bottom