Nimefuta na kublock namba 50 kwenye simu yangu za wanaojiita marafiki zangu

Ila na wewe ulikuwa na marafiki wengi sana aisee.

Wachache tu wanatosha kabisa tena saa ingine unaangalia wale wanaofanya kazi idara ambazo unajua ipo siku utahitaji msaada kwao tena usipende sana uwe wa kifedha mfano Hospitali na kwingineko.
 
Kwa hio unawapima wanaume🤔 Kama hawana wafanyaje afu nilijua tu unatupima haikuwa issue ya serious
 
Hao ndo wale wa save for save unadhani kuona status ya mtu wasap ndo anakuwa kashakuwa rafiki yako
 
Kabla ya tarehe 31 nilifuta zaidi ya contacts 600 na kufanya tathmini upya ya marafiki wote na watu wa karibu.
Kwa hiyo walibaki marafiki wawili tu kwenye inner circle.
 
Mimi nadhani kuna kitu kidogo umekosea umehukumu watu kwa kushindwa kukusaidia pesa lakini kumbuka kuna siri nyingi kwa watu hata hao unaotaka kwao kitu hujui wako katika hali gani inawezekana mtu hana kitu anaona hata aibu kukwambia sina ila ningekuelewa kama hukupata hata msaada wa mtu kutaka kujuwa umefikia wapi je umeweza kupata sehemu mimi kwa kweli sina lakini naamini utapata sehemu au kufuatilia issue yako hata kwa kujali tu kukupigia simu lakini kama yote haya umekosa hata mtu kukupigia siku ya pili vipi yameisha vipi jana sikuwa na amani nafikria issue yako tu la kufanya sina... msaada au rafiki sio lazima pesa kuonesha kujali tu ina umuhimu sana. Kukwambia hivi ume wa block lakini unajuwa na wao shida zao?
 
Uamuzi wa busara refer ule wimbo unaitwa "mpunguze" (sijui hata aliyeimba au kama unaitwa hivyo kweli)
Ngoja weekend hii na mimi nijifungie ndani ila ntaanza na wadada nliowahi kupita nao na bado wananipiga mizinga kama bado nipo nao.

Wiki ile nyingine napita na washkaji nliowahi kufanya nao kazi au kusoma nao na wapo mbali tena hawana msaada.

Halafu mwisho wa mwezi huu namalizia na hawa washkaji ninaowanunulia bia hapa Dodoma ila wakipata hela wanahama viwanja
 
Makosa nayoyaona mimi;
1. Kuwa na marafiki wengi, huwezi kuwa na marafiki wote hao. Labda useme ni watu tu mnawasilina lakini marafiki kama marafiki huwa ni idadi ndogo sana, labda watano tu.
2. Kufanya huku ukisubiri fadhila, kama ni mtu wa kusaidia huna haja ya kuangalia nimemsaidia nani kwa ajili gani na atanipa nini nikipata majanga.
3. Unasaidia kupitiliza, watu wengi hivyo unajitoa kwao? Ni wengi mno...
 
Sijawahi kuwa namarafiki ila kuna watu wengi nafahamiana nao na tunasaidiana kukiwa na uhitaji.

Huwa naona watu wanasema Wana best friends nashangaa inatokeaje hiyo?
 
Kiukweli umenena vyema ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…