Nimegugo dalili zote UKIMWI, ninazo

Nimegugo dalili zote UKIMWI, ninazo

chakula cha watoto

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2023
Posts
539
Reaction score
1,507
Niliamka saa kumi usiku baada ya kuona hizi wiki mbili naumwa Kila siku kichwa, nahara, kitambi chote kwishaaa mkanda nimetoboa matundu sita mpya mpaka sasa.

Nikaona kabisa huu ni UKIMWI, kuchukua simu nikaingia gugo nikaandika dalili za ukimwi. Nimesoma naona zote ninazo mpaka kijipu upande wa paja karibu na korodani ninayo wanaita groin nodes.

Wakuu kupima naogopa Vibaya mno, nakumbuka mwaka 2010 niliwahi kupata mkanda wa jeshi naona hili Tena limekuja. Hii ngoma nimekuwa na stress Sana hata kazini kwenda nahisi uvivu.

Muda wote kichwa na misuli inauma nahisi kuchokaaa.
 
Nishawahi kupata dalili kama hizo kwa muda mrefu, mafua yasiokata, kikohozi homa na kupungua uzito
watu wakawa wanasema nikapime labda nimeukwaa

Dawa nyingi nikatumia hapo naogopa kwenda kupima,
Maza akaingia room akasafisha feni yangu vizuri sana, baada ya siku chache nikawa mzima.
 
Ulipata Mkanda wa jeshi??😳😳
Au uligugo pia na wenyewe?
Nenda kapima achana na Gugo..
Ulipopata Mkanda wa jeshi ulitibiwaje na ulitibiwa wapi?
Maana nina amini kama uliambiwa Hospitali kuwa una mkanda wa Jeshi basi lazma walikupima..
Sikwenda kupima, mm mambo ya kupima Pima hapana, Ila ulikuwa ni mkanda ule maana upele uliwasha mgongoni mpaka kwa babu
 
Niliamka saa kumi usiku baada ya kuona hizi wiki mbili naumwa Kila siku kichwa, nahara, kitambi chote kwishaaa mkanda nimetoboa matundu sita mpya mpaka sasa

Nikaona kabisa huu ni ukimwi, kuchukua simu nikaingia gugo nikaandika dalili za ukimwi. Nimesoma naona zote ninazo mpaka kijipu upande wa paja karibu na korodani ninayo wanaita groin nodes

Wakuu kupima naogopa Vibaya mno, nakumbuka mwaka 2010 niliwahi kupata mkanda wa jeshi naona hili Tena limekuja. Hii ngoma nimekuwa na stress Sana hata kazini kwenda nahisi uvivu

Mda wote kichwa na misuri inauma nahisi kuchokaaa
Nakumbuka Miaka ya 2008 mpaka miaka ya 2014 hivi ujana ulinizidia sana 😀😀

Sasa kuna kipindi nikaanza kuumwa kutokana na kielimu cha afya nilichokuwa nacho nikaona hichi kimo mzee..

Ila kwa bahati mbaya nilikuwa nahisi Inaweza kuwa HIV au Hepatitis B Nilichokua naomba Mungu kipindi Hicho bora iwe HIV..😀😀..

Nikapiga moyo konde sasa siku moja nimekaa kaa zangu ifisini nikajipima nikakuta HIV haipo..
Nikavuta Pumzi..

Sasa miaka hiyo serikali wakaja na chanjo ya bure ya hepatitis kwa watumishi Kimbembe kikawa kupima 😀😀😀..

Ila nikakaza moyo nikapima na nikalambwa chanjo zote za Hepatitis..

Sasa ninachokushauri kuna Desturi ya Akili kutengeneza Illusion kutokana na majanga ya nyuma na kukutisha ila ukipima unakuta Hola hauna kitu..
 
Sikwenda kupima, mm mambo ya kupima Pima hapana, Ila ulikuwa ni mkanda ule maana upele uliwasha mgongoni mpaka kwa babu
Shida iko Hapa!😀😀
Mkanda wa Jeshi mkuu una dalili zake na una Signs zake na una KANUNI zake za kiutambuzi unaotofautisha na Rashes zingine..

Ndo maana nikakuuliza au na wenyewe uligoogle?
Maana mkanda wa jeshi una sheria zake za kuujua na sio wote wanaojua Shingles inakuwaje
 
Back
Top Bottom