Niliamka saa kumi usiku baada ya kuona hizi wiki mbili naumwa Kila siku kichwa, nahara, kitambi chote kwishaaa mkanda nimetoboa matundu sita mpya mpaka sasa
Nikaona kabisa huu ni ukimwi, kuchukua simu nikaingia gugo nikaandika dalili za ukimwi. Nimesoma naona zote ninazo mpaka kijipu upande wa paja karibu na korodani ninayo wanaita groin nodes
Wakuu kupima naogopa Vibaya mno, nakumbuka mwaka 2010 niliwahi kupata mkanda wa jeshi naona hili Tena limekuja. Hii ngoma nimekuwa na stress Sana hata kazini kwenda nahisi uvivu
Mda wote kichwa na misuri inauma nahisi kuchokaaa
Pole sana ni Vema kupima ndugu yangu ukimwi sio mwisho WA maisha Ila tambua kwamba moja ya kitu hatari ni kujipima Kwa hisia ambapo uleta hatari ya msongo wa mawazo ambao uleta upungufu wa Kinga ambapo uleta magonjwa yadhaniwayo yanasababishwa na ukimwi kumbe Ni hofu ndio imekufikisha hapo.
Nakushauri kitu ndugu yangu nenda kapime huku ukiwa umemwachia mungu kila kitu Kwa kuwa ikitokea umekuwa nao jipe imani ya kuishi na ikitokea huna basi badili mtindo Wa maisha, huu ugonjwa tunauchukulia poa ukiwa hujapata lakini ukiupata inaitajika imani kubwa sana ya kiroho kuishi nao.
Nakushauri tena nenda kapime achana na maelezo ya google kuhusu kujitambua kama unavyo au huna, magonjwa mengi yanaingiliana mfano: kuharisha ,kukonda linaweza kuwa zao la hofu, mkanda wa jeshi umpata mtu yeyote japo Kwa mtu ambaye anaukimwi pia anaweza kupata lakini akiwa amekaanao huo ukimwi Kwa kipindi kirefu.
Mimi nakupa ushuhuda wangu kwamba mwaka fulani nilikwenda kozi, kule kozi Kuna bwana nilikuwa nalala naye kitanda cha karibu na alikuwa anameza dawa ambazo yeye alisema za joint lakini zinafanana na za ARV kuanzia kopo hadi muhundo.
Tulishea vitu vingi sana kabla ya Mimi kujua zile dawa,Mimi nilikuwa natumia sindano kutolea uchafu kwenye Meno alafu naiweka sindano kwenye Meza, nilikuta anaitumia sindano kama ambavyo Mimi hufanya nilihisi kuchanganyikiwa baada ya yangu kuikosa nilijua wazi kumbe siku zote tunashea.
Kimbembe niliporudi kutoka kozi wiki moja mbele nikaanza kuharisha, jasho usiku,vipele mgongo wote,kuokoa na mafua, nikaingia google na YouTube kucheki dalili za awali za ukimwi Braza nikajiwekea tiki tayari na nikabaki na Siri kwamba nitaishi navyo mpaka nitakapokuwa mahututi.
Siku zinaenda nikawa na mawazo lakini Ile Hali ikaisha Ila kuumwa kupo mwezi huu napitisha mwezi ujao naumwa ikawa ni mawazo juu ya mawazo, siku fulani hivi nikawa naumwa sana kichwa na mafua karibia wiki mbili mfulululizo na homa zingine ikiwemo na malenge lenge mikononi nikaona hapana nikamuita mke wangu nakumuambia kwamba Mimi najiisi ni magonjwa wa ukimwi nakuomba ATA nikigundulika husinikimbie.
Wife akanipa moyo na kuniambia huwezi niacha atanibeba mwanzo mwisho, asubuhi hao hospitalini mpaka Kwa wahusika nikawaelezea na baadaye akatuchukua vipimo na kuanza upimaji, Mimi wakati huo nishamuambia Yule Dada kwamba Mimi najua ni mgonjwa TU Ila nimekuja kuthibitisha ili nianze dozi nilikaa tayari kuanza dozi nilikubali yote.
Baada kama dakika kadhaa muhudumu anauliza muko tayari kupokea majibu yenu Mimi nimelalia Meza namwambia Yuko tayari ,muhudumu wa afya akasema wote ninyi ni WAZIMA endeleeni kujilinda huwezi amini nililia sana tena sana na kuapa kwamba nitaanza kuswali.
Hivyo nakuomba husijihukumu nenda kapime afya ni mtaji wako iwe utakutwa nao au hutokutwa nao Ila ukishajitambua utaishi kulingana na ilivyo na utashauriwa kuwa maisha lazima yaendelee na kuumwa sio kufa.