Nimegundua akaunti nyingi benki hazina kitu

Hardlife

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2021
Posts
2,758
Reaction score
6,299
Mara nyingi ninapoenda ATM hukuta risiti watu wamesahau pale pakuchukulia risiti. Inasahaulika sana kwakuwa ndiyo ya mwisho.

Pengine kadi nazo zingekuwa za mwisho zingesahaulika sana na ndiyo maana waliset uchukue kadi then pesa.

Sasa nina tabia ya kuangalia salio la ile risiti iliyobaki. Nikiri imekuwa kama tabia yangu na nikijumlisha tangu nianze kuangalia risiti zinazosahaulika tangu nianze kutumia ATM zaidi ya miaka 15 sasa.

Nilizoona ni zaidi ya 300 na kwa hii niliyoiona leo ndiyo nimekuta ina salio kubwa ambalo ni Tsh 1.2m.

Mara nyingi nakuta kati ya 50k mpaka 500k. Watu wengi hatuweki akiba labda kama tunatumia akaunti nyingine.
 
Benki inakitanisha wenye hela hawajui watazitumiaje na wasio na pesa Ila wanajua wanazitumiaje kuzalisha .

Ukiwapa 100M fixed kwa mwaka watakupa riba ikienda Sana Ni 6-7% kwa mwaka. So hapo utaambulia ngapi hapo.

Wanamkopesha mjanja mzalishaji ama anayejua kucheza money's game kwa riba ya 17% kwa mwaka. So bank net yao Ni 10%.

Bank ana act like a middle man. Sijui Kama unanielewa. So hakuna ujanja kujisifia kuwa mie Nina hela nyingi kwenye akaunti.

Banks zinamheshimu mno yaani mno a man ambaye akaunti yake Ina mishe mishe Yani haitulii.

Mara 200M zimeingia kwa akaunti Mara Kuna zero balansi. Mara zimeingia 300 Mara zometoka 240M ,Mara zimeingia 150 zometoka 200.

Hiyo frequency uwe nayo kwa zaidi ya miaka kadhaa utashangaa watakuita wanakuambia wakupe hela uzalishe uwapelekee riba kidogo tu.

Sasa wewe ingiza tu wanajua u mwoga wa kushika hela.
 
Sahihi kabisa.
 
Mualimu mshahara wake ni 350k hadi 900k anapokea hizo hera kupitia benki baada ya siku 30, akiweka Atm kutoa hera anakatwa 3000, sasa unataka huo mualimu abakize shilling ngapi hapo benki?
 
Upo sahihi 100% tangu mwaka jana nilikua nawakopa sana voda halafu kabla mambo hayaja haribika na rudisha pesa yao yote kwa wakat.

Videni kama 50k, 100k nilikua na kopa sana mpaka leo jamaa wameamua kunipandishia dau la kukopa wana weza kunikopesha mpaka 425k kwahiyo nilipata ka shida cha chap na weza vuta tu kama akiba then na warudishia baadae [emoji4][emoji117] na tolea mfano kama bank tu wanakuwaga na records za mteja mizunguko yake yote ya hela.
 
Inawezekana ukawavuta mpaka 10M baadaye you dumb yor sh1t into @ssaн0le
 
Watu wengi mishara ni less than a milion, sasa mtu ana familia yaani mke na watoto plus familia za kiafrika ukiwa na kakazi unawatunza hadi watoto wa shangazi hivyo akaunti inakuwa ni njia ya kupitisha pesa ukaitoe uitumie uanze subiri tena mwezi ujao
 
Unachosema ni ukweli.
 
Sina cha kuongeza
 
Wengi ni wakombozi wa familia
 
Majembe,Yono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…