Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Mkulima harudishi gharama zake kwa mahindi debe kufika 25000. Mnashindwa kutofautisha Kati ya soko lilivyo na inflation.Mkuli.ma hawezi kutolewa kafala ili wengine wzpate chakula kwa bei nafuu. Wakati mkulima huyo huyo akiuziwa mbolea bei juu hakukuwa na makelele ya kumtetea.
Mvua ilipokata wakati kisha ingia gharama za kulima, kupanda na kupalilia watu wzlikaa kimya, basi endeleeni kukaa kimya wakati mkulima anarudisha gharama zake.
Hakuna mkulima analima kila aina ya mazao. Mahindi yakifika 25000 kwa debe hiyo sio dalili nzuri kwa maana mkulima huyo huyo atalazimia na yeye kununua maharage au mafuta au bidhaa nyingine kwa bei kubwa. Usije ukafikiri mahindi debe likiwa 25000 basi mkulima kazi yake yeye ni kukupata faida tu, kumbuka ana mahitaji mengine nayo yanapanda.
Kikubwa serikali kudhibiti mfumuko wa bei(inflation), haina maana kabisa mkulima anauza mahindi gunia 150000, aalafu yote hiyo anaitumia kununua bidhaa nyingine zilizopanda bei.
Ni bora mkulima auze gunia 70000, alafu mbolea anunue 40000, kuliko kuuza gunia 150000 alafu mbolea ainunue kwa 170000. Bado hajaenda kweye mahitaji ya kawaida ya nyumbani, mwisho kauza kwa pesa nyingi alafu yote anaimalizia kwenye mahitaji na haitoshi.
Usikariri bei kubwa ni muuzaji kunufaika bila kufikiria pia muuzaji atahitaji mahitaji mengine kwa bei kubwa.