Nimegundua Bashe hajui maana ya Food Security

Hawana ushawishi Wala akili,toka lini chawa akawa na akili? Hao wameendekeza njaa ikapanda hadi kichwani.Kwa Sasa hivi Kuna mtu mmoja Kenya hapo anaitwa William Samoe Ruto,huyo alikataa uchawa na amefanikiwa.Hao wengine ni Fleas tu.
 
Kama kuna kenge ni pamoja na watu kama hii kenge hapa.

Wanaosafirisha mazao nje ni wa wachuuzi na si wakulima.Wakulima wanauza kwa bei ya kunyonywa sana.Ila kwa vile ni kenge haitanielewa

Waambie hao wakulima wasiuze kwa bei ya kunyonywa. Hilo liko ndani ya uwezo wao. Kama wamekubali kuuza kwa bei chee ni kosa lao sio la wanunuzi. Mbaya ni hao wakulima kulazimishwa kuuza kwa bei chee.
 
Sawa Mkuu, Mchumi wetu. Tushauri sisi Wakulima tukiwaona wanunuzi wa bei ya juu (nzuri) tuwakimbie? tukimbilie wale wa bei ya chini eeh!!! Uchumi ni demand and supply basi.
 
Mm nimekuelewa, concept yangu ni kuwa bidhaa zikipanda bei kwa sababu yoyote ile, na ww huduma zako pandisha bei. Kuwa sehemu ya inflation mpaka mfike optimal point recession ianze na ww shuka nayo. Gharama za maisha ziamishe kwa mwingine, usikubali ziishie kwako. No one cares about individual linapokuja suala la macro economy. Kama ni mwajiriwa wa serikali tafuta namna sababu mshahara utakulazimisha machungu ya inflation yaiishie kwako
 
Waambie hao wakulima wasiuze kwa bei ya kunyonywa. Hilo liko ndani ya uwezo wao. Kama wamekubali kuuza kwa bei chee ni kosa lao sio la wanunuzi. Mbaya ni hao wakulima kulazimishwa kuuza kwa bei chee.
Bei haipangwi na mkulima, soko(mnunuzi) ndio hupanga Bei. Mkulima hata afanyaje Kama soko kwa wakati huo linataka debe Kuuzwa elfu 3, atauza tu. Labda akatae kuuza abaki nayo, na hapo yatamuozea na hata namna nyingine ya kupata pesa.

Ndio maana hata mazao ya biashara unaona wanunuzi hupanga bei kabla hata ya kilimo kuanza.
 
Sawa Mkuu, Mchumi wetu. Tushauri sisi Wakulima tukiwaona wanunuzi wa bei ya juu (nzuri) tuwakimbie? tukimbilie wale wa bei ya chini eeh!!! Uchumi ni demand and supply basi.
Kwa sasa huyo mnunuzi wa bei ya chini anatoka wapi? Hii Hali ya Sasa hivi ni dunia nzima na ndio maana nchi zote zinahnagaika kuicontrol.

Nilichikueleza huwezi kupiga pesa katikati ya inflation. Ni sawa na muuza duja ajisifie sasa hivi anapiga pesa kisa sabuni anauza 3500 kutoka 1500.

Au Ni sawa na kondakta ajisifie anapiga pesa kisa nauli imeongezeka wakati mafuta ananunua litre 1 kwa 3500.

Mkulima unauza gunia 150000, hapohapo pembejeo ulinunua mara 3 ya bei ya awali. Hapohapo ukienda dukani mahitaji yote yamepanda Bei. Au hizo pesa mnazopata hamtumii kwenye kitu chochote? Mnazitunza tu?
 
Unapandishaje huduma ikiwa wewe huamui bei? Ndio maana nimekutolea mfano Kama una duka unaweza kuamka asubuhi na kuuza mkate elfu 10??

Bei inapanda kutokana na mnyororo wa uzalishaji hiyo bidhaa. Ukiona mkate unauzwa 2000 na wenye bakery basi jua nao wamenunua unga wa ngano kwa bei kubwa. Na wanaozalisha unga wa ngano nao wamezalisha kwa Bei kubwa.
 
Reactions: Tsh
Huamui bei kivipi boss? Kwani dukani kwako pale anayekuuzia mkate akikupandishia bei si na ww unaupandisha bei ili margin yako ibaki pale pale?

Kama huduma zako demand hairuhusu ww kuongeza bei na unanunua kwa bei ya juu basi unafanya biashara kichaa.
 
Una shida uko upstairs
 
Reactions: Tsh
Na wewe kanunie
Wakati tunawauzia Wakenya Watanzania wanakuwa wananunua bia na t-shirts za CCM kwenda kwenye mikutano ya Kinana.
 
Umeandika kinadharia zaidi kuliko kiuhalisia. Msimu huu mbolea zilipanda, beii sana je zilisababushwaa na mkulima kuuza mahindi bei juu? Mafuta yalipanda bei sana je ilichochewa na mkulima kuuza mazao yake bei juu?

Kama mkulima akiuza sasa mazao yake kwax bei juu inampunguzia mzigo wa kununua bidhaa zingine ambazo zimepanda sana hivi karibuni. Ni sawa na wewe mfanyakazi ulivyodai nyongeza ya mshahara kwa kigezo kuwa bei za vitu zimepanda sana..

Suala la inflation hilo ni somo lingine ambalo usliifunganishe na haki ya mkulima kupata fair return kwa investment aliyofanya. Inflation ina source kuu mbili cost push na demand inapokuwa kubva kuliko supply. Hata wewe ukilipwa,mshahara mkubwa bila tija inachangia inflation kwa sababu gharama za utoaji wa huduma au uzalishaji wako itakuwa ghali. Kudhibiti inflation hiyo ni kazi ya serikali na benki kuu kupitia,fiscal na monetary policies mtawalia.

NB: Hakuna mtu mwenye uchungu na mkulima kuliko mkulima mwenyewe.
 
Katika mwaka tuliopiga hela wakulima basi ni huu wa 2021/2022. Nimeuza mchele kwa shilingi 2,500 kwa kilo na viazi shilingi 90,000 kwa gunia huko huko shambani. Wachuuzi watawaletea kwa bei wanayoijua wao! Sisi tumeshamalizana nao.
Halafu baadhi ya watu wa mijini wanawachukulia wakulima kama watu wasio na akili kumbe kuna watu wanaishi hapa DSM lakini ukifika msimu wa kilimo wanaenda kulima hadi wanavuna kisha wanarejea mjini kula maisha.
 
Go to hell
 
Kama kuna kenge ni pamoja na watu kama hii kenge hapa.

Wanaosafirisha mazao nje ni wa wachuuzi na si wakulima.Wakulima wanauza kwa bei ya kunyonywa sana.Ila kwa vile ni kenge haitanielewa


Kama ni rahisi ingia ufanye halafu utajirike
 
Ninyi mnaosema mahindi yasiuzwe nje eti wanaopeleka nje sio wakulima. Mkulima yamhusu nini? Mkulima ana furahia bei nzuri kurudisha gharama na ustawi wa kaya yake.

Iambieni serikali inunue mahindi kwa bei nzuri sio kuwageuza wakulima kuwa wahisani wanaodumu katika umaskini.

Nimelima mahindi kwa adha nimepata gunia 100. Anatokea mtu ananipangia wa kumuuzia palikuwa na mkataba?

Pesa ambayo ningeipata huenda nami ninge boresha makazi na maendeleo mengine. Anatokea mtu anayazuiya na bado anatamani niendelee kulima mwakani.

Kuna mantiki hapo?

Nini itakuwa motisha ya kurudia kulima zaidi hayo mahindi iwapo ntapata hasara au faida kiduchu?

Mnataka kuwaonea wakulima kwa sababu bado hawaja pata ujasiri wa kujitetea. Walio wengi wanapata gunia zisizo zidi 10 kwa ekari na wanalima ekari 1 hadi 3.

Lakini ikitokea fursa kidogo haohao wanatumika kama kundi la kuwabeba wengine wasio lima. Hii sio haki
 
Ulitaka mkulima kila mwaka awe wa kulia machozi tu? Ulitaka wakulima kila mwaka wauze kwa Bei ya hasara ili wewe ufurahi? Ulitaka kuona kila mwaka wakulima Ni wakuteseka na kuvuja jasho huku nyinyi mkilia kimvulini, Nenda na wewe ukalimee ujuwe uchungu wake, Nenda ukalime uje uuze hiyo Bei ndogo unayoitaka, Nenda ukalime ujuwe adha ya kilimo, nenda ukalime ujuwe mkulima anahangaika vipi juani na kwenye mvua, nenda na wewe ukalimee ujuwe ugumu wake,


Msitake kuwafanya wakulima wa nchi hii kuwa daraja lenu ninyi wanyonyaji wakubwa, Tunamshukuru Sana mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kutujali sisi wakulima wanyonge, Sasa tunaona faida ya kilimo chetu, Sasa tunafaidi jasho letu

Mh Bashe songa mbele fanya kazi uliyooaminiwa na mh Rais wetu mpendwa, Msaidie kwa nguvu zako zote, usimuuangushe Rais wetu tunayempenda kwa dhati ya mioyo yetu, Fanya kazi chapa kazi Leta matumaini kwa watanzania Kama ambavyo mh Rais wetu ameongoza njia hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…