Nimegundua haya Mawili tu yangefanyika katika Vichwa vya Watanzania wote wala hizi 'Kelele' za 'Chura' tusingezisikia kabisa

Nimegundua haya Mawili tu yangefanyika katika Vichwa vya Watanzania wote wala hizi 'Kelele' za 'Chura' tusingezisikia kabisa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Nguvu yao kubwa Watanzania kupenda ( kushadadia ) sana Umbea na Mambo ya Kingumbaru ( Kijinga ) na Kipopoma ( Kipumbavu ) wangeiwekeza zaidi katika Kupenda kulipa Kodi Vizazi kwa Vizazi wala lawama hizi zisingekuwepo.

2. Ule muda mrefu ambao Watanzania waliutumia Kumjadili sana Diamond na Tuzo yake ya BET Kisha Mzee Mpili wa Yanga SC wangeutumia katika Kupitia Bajeti ya nchi, Kuichambua kila Kipengele na Kuielewa vyema Wala hizi lawama tusingezisikia leo Siku ya Tatu ( 3 ) sasa.

Hata katika Vitabu vya Kidini ( Imani ) Suala la ulipaji Kodi limehimizwa mno tu na ni Wajibu wa kila Binadamu ( Mtu ) anayepumua ili Maendeleo yaweze kupatikana.

Mnataka Tanzania iwe kama Marekani, Uingereza na Dubai Kimaendeleo halafu mkiwekewa Kodi mbalimbali mnaanza Kulalama tu wakati ukweli ni kwamba Watanzania wengi tunajuana kwa Matumizi mabaya ya Pesa zetu kwa Mambo ya Kipuuzi Kipuuzi tu ila tukiwekewa Kodi tunaona tunaonewa.

Mmeshaambiwa kuwa hii ni Tozo ya Kodi ya Kizalendo ambapo Serikali imebuni chanzo chake cha Mapato zaidi na hatimaye imekipata katika Mitandao ya Simu tatizo liko wapi?

Kuna Watu mnataka mwakani muongezewe Mishahara ( na mmeshahaidiwa mtaongezewa ) hivi mnadhani bila 'Mama' kuja na Ubunifu wake huu hizo Pesa za Mishahara yenu mnataka azitoe Kijijini Kwake Unguja?

Wakati akina GENTAMYCINE na wengineo ( wenye Akili na Maono ) kila Siku tunawaambieni kuwa Meli ya aina Moja inayoongozwa na Manahodha tofauti tofauti tokea iundwe mwaka 1977 sasa inaenda 'Kutuzamisha' katika Mkondo wa Nungwi si mlikuwa hamtuelewi? Sasa tutaelewana tu Kudadadeki zenu.

Lipeni ( tulipeni ) Kodi tuacheni 'blah blah' japo nailaumu sana Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Kiwango kidogo hiki cha Tozo kwani Mimi GENTAMYCINE nilitamani ili Watanzania tunyooke na tunyooshwe vizuri ingekuwa ukitoa Tsh 10,000/ Basi ukatwe Tsh 6,000/ na ukitoa Tsh 100,000/ ukatwe Tsh 75,000/ huku ikiwezekana ungekuwa ukitoa Tsh 1,000,000/ Basi ukatwe Tsh 800,000/ naamini hapa Akili zetu Watanzania zingeamka na kutukaa sawa kabisa.

Katika hili nina Furaha kubwa sana tu.
 
Hatukatai kodi ila kiwango kikubwa mno
Mimi naona ni Kiwango kidogo sana hivyo naiomba Serikali ya CCM ya Rais Samia waiongeze iwe Maradufu yake labda Ungumbaru na Upopoma wa Wananchi wa kila baada ya miaka Mitano Mitano utapungua na Akili zitaturudia baada ya Kuathiriwa na Moshi mzito wa Mwenge wa Uhuru.
 
Halafu utasikia kesho sijui nani amekula pesa za umma halafu aliyeiba hizo hela yupo halipi wala hastakiwi sasa si tatizo hilo
Ndio hivyo unapotakiwa kulipia uzalendo kwa kimakua tunasema "solidaliti"
 
Kuna mambo mengi mkuu hii ni nchi kubwa. kiuchumi tulalamika ela hatuna serikali inaona imechapisha ela nyingi na hazionekani mtaani.
Kuna mawili kurudisha ela kwenye mizunguko wa bank na kuzitoa kwenye miamala ya simu serikali inaamini bank ni salama itapata takwimu sahihi.
Na hii hatujazoea. Tulizoea serikali ikihisi kitu kwenye mzunguko wa pesa kiuchumi sio sahihi wanachapisha pesa mpya ili kuondoa sintofahamu.
Hii hata magu alishafanya kwa bureu change ikionekana dola zipo mtaani nyingi anafunga bureu change dola zinarudi bank wanapata takwimu sahihi za fedha za kigeni.
Hivyo mambo ni mengi kwenye usalama wa taifa lolote.
Pesa inaweza kuondoa hadi serikali iliyopo madarakani.
Hii mpaka kwenye magari magu alitumia aliona magari used yananuniliwa mengi toka nje akapunguza miaka ya used car na kupunguza uingizaji wa magari chakavu.
 
Hapa nilipo toka asubuhi sijaona mtu anaulizia kutoa au kutuma mtandao wowote ule
 
Back
Top Bottom