Nimegundua haya

🤝👏👍
 
Mkuu nimesema ukifa una kuwa wiped memory na unakuja kuanza moja katika mwili mwingine na huwa huwa unakuwa na trait zilezile mfano kama doctor unapenda tena uwe doctor automatically bila kujua kumbe ulishapitiaga hayo over and over
Mkuu unaulizwa ulisha wahi kufa ukarejeshewa kumbukumbu zako kwenye mwili mpya???

Au kuna mtu unayemfahamu aliye wahi kufanyiwa hayo?? Ukatushuhudia hapa kwa vielelezo na ushahidi??

Tuambie hao roho wanakuwaje hai?? Wanaumbwaje? Wamehifadhiwa wapi wakisubiri mtu afe? Wanaishije kabla ya kupandikizwa kwenye mwili mpya?
 
unahitaji msaada wa kisaikolojia mapema sana, akili yako inamhitaji Mungu pia. moto upo, na kama hautaokoka hapa duniani, utaenda kuungua. kuhusu binadamu, ni kweli mwanadamu ni roho wala sio mwili, huu mwili ni nguo tu tunavaa, ukifa roho inaenda aidha motoni au sehemu salama, mwili huku duniani unaoza.

Luka 20:34 - 36, Yesu akawaambia, wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwasababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

LUKA 16:19 - 31 YESU ALISEMA: "Palikuwa na mtu mmoja tajiri, ambaye alikuwa anavaa mavazi ya bei kubwa sana ya rangi ya zambarau na kitani safi, na kufanya sherehe kila siku. Na mlangoni pa huyo tajiri kulikuwa na maskini mmoja jina lake Lazaro, ambaye alikuwa amejaa vidonda. Lazaro alitamani kupewa makombo yaliyoanguka kutoka mezani pa huyo tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kuramba vidonda vyale! Basi, huyo maskini akafa, nao malaika wakamchukua wakamweka karibuna Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa. Huyo tajiri akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye. Basi akaita kwa sauti: Baba Ibrahimu, nionee huruma, umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu. Lakini Ibrahimu akamjibu; kumbuka mwanangu kwamba ulipoea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini yeye anatulizwa, na we unateseka. Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, na wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze. Huyo aliyekuwa tajiri akasema; basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso. Lakini Ibrahimu akamwambi; ndugu zako wanao Musa na manabii, waache wawasikilize hao. Lakini yeye akasema, sivyo baba Ibrahimu, ila kama mtu atafufuka kutoka kwa wafu na kuwaendea watatubu. Naye Ibrahimu akasema; kama hawatawasikiliza Musa na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka kwa watu".
 
hivi kuna ushaidi gani kwamba binadamu ana roho na nafsi .? usikute ubongo nando nafsi na roho 🤔🤔
 
hizi. nazo story zahovyo tu.! ivi Leo afufuke babu yangu anambie kuna moto. niache zambi kweli nitakataa na nisiamini.? nilipofikia now siamini kilakitu kwenye huu ulimwengu hadi nione nakusikia au kihisi kwa kutumia ngozi
 
Unataka maarifa yanayopaswa kuelezwa na maiti?yaani mambo inabidi aje leo hapa babu wa babu yako aliyekufa 50s huko akueleze unategemea uelezwe na mtu mpo hapa mna-share pumzi moja?

Dude,you must be kidding!
sio hayo tu hata yakwenye vitabu vya dini pia. ivi kwamfano ikitokea Nyerere kambalage afufuke Leo aseme jaman kuna moto kuna mbingu na kuna mungu.! ivi kunu watu wangekataa.?
 
umewahi kukutana na mtu wahivyo anaekumbuka maisha yake ya kabla hajafa nakuzaliwa upya.?
 
Hiyo.no.5 hasa kuhusu kituo Cha luwenzory naomba ufafa nuzi mkuu
 
Hiyo.no.5 hasa kuhusu kituo Cha luwenzory naomba ufafa nuzi mkuu
 
Namba 3,na namba 13 zimenijulisha kuwa wewe ni mgonjwa wa akili kabisa,Shigongo alikuwa sahihi aliposema Bungeni kuwa Watanzania wengi wanaumwa ugonjwa wa akili kwa sababu ya maisha magumu
 
hizi. nazo story zahovyo tu.! ivi Leo afufuke babu yangu anambie kuna moto. niache zambi kweli nitakataa na nisiamini.? nilipofikia now siamini kilakitu kwenye huu ulimwengu hadi nione nakusikia au kihisi kwa kutumia ngozi
unajitoa tu ufahamu, ila unajua moto upo, na utakuja kuungua.
 
life is nothing but an experience and we are the experiencers, everyone is experiencing their own realities and its these experiences which give life the meaning

Kuhusu maisha baada ya kifo,majibu sahihi anayo yule aliye experience kifo
Nyingi ni stori za binadamu hai kwa binadamu hai mwenzake.
 
ni kwasababu unaishi kimwili, ndio maana unafikiri kimwili, shetani ameushika ufahamu wako, amekutwika kiburi, kiwe cha elimu au pesa au exposure au vyovyote, ndio maana hauamini kwamba kuna maisha baada ya kifo. Laiti ungalijua kwamba hata hapahapa duniani wapo watu wengi sana pamoja na kuishi kimwili, wanaishi kiroho na kuoperate kiroho pia, sasaivi wewe umelala wapo watu wanaoperate spiritually kabisa kwa kusafiri na kufanay shughuli mbalimbali ila miili yao imelala kwenye kitanda kwao.

zaidi ya yote, Biblia imeeleza wazi, Yesu mwenyewe alieleza kwamba kuna maisha baada ya kufa. na kwa kudhihirisha zaidi, yeye alikufa na siku ya tatu akafufuka, hivyo aliongea kulingana na experience, hizi sio story za abunuasi, ni vitu halisi ambavyo unatakiwa kuvitafakari usiku na mchana. Uelewe kuna maisha mengine baada ya haya ambayo unaweza aidha kwenda uzimani au motoni, uchaguzi ni wako.

Ili upone, unatakiwa kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, utapata uzima wa milele hapa duniani na baada ya maisha haya, huu ni ushauri wangu kwako kabla haujaburutwa siku moja uokoke kwa nguvu, though wapo watu ambao unawezafikiri pengine waliandikiwa mauti kwasababu hata uwahubirie vipi hawaamini, wabishi tu, ila ni kwasababu ya kiburi cha uzima ambao Mungu mwenyewe ndio amewapa. Mungu akurehemu.
 
ivi kwani watu walio okoka hawafi.? alafu wew umewahi kuishi kiroho.? sema mtupanga mtupige visadaka tu hakuna lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…