Nimegundua 'KITI' na watendaji karibu wote hawaijui Katiba

Nimegundua 'KITI' na watendaji karibu wote hawaijui Katiba

Binafsi nina mashaka uelewa wa mambo wa namba moja au anafanya makusudi. Juzi juzi alisema katiba ni ya wananchi na si wanasiasa pekee. Nikajiuliza:

1. Kwani ile tume ya WARIOBA si ilizunguka Tanzania nzima, tena vijijini ndani ndani walikusanya maoni. Nina uhakika hakuna tume ya katiba mpya itakayoundwa na kufanya kazi kwa uweledi kama tume ya Warioba kwa sababu ile tume ilipewa uhuru wa kufanya kazi, na maoni yale yalikuwa ni ya wananchi kabisa.
Ndio maana mzee wa watu alishika tama siku ile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo Wapemba wenzake ndio wanajuwa katiba ndio maana wana katiba mpya?
20230914_100820.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anitajie IBARA ya Katiba inayosema kwamba Rais ndiye mwenye MAMLAKA ya KUKUBALI au KUKATAA uanzishwaji wa mchakato wa Katiba ya nchi! Kwa uelewa wangu, Katiba ni mali ya wananchi, inayotoa ULINZI kwa raia dhidi ya Watawala. Sasa, mtawala hatakiwi kuamua lini Katiba ifanyiwe maboresho. Hayo MAMLAKA yako kwa wananchi.

NINI KIFANYIKE!
Tunaweza kuanzia mahakamani (no guarantee). Kifungu 81 ya Sheria ya Tafsiri za Sheria (The Interpretation of Laws Act) kinasema kwamba kama kuna jambo limetungiwa sheria ili likamike, jambo hilo ni LAZIMA likamilishwe. Kushindwa kukamilisha jambo hilo ni KOSA LA JINAI. Hata kama sheria mahususi imesha muda wake, jambo hilo ni LAZIMA likamilishwe.

Suala la mchakato wa Katiba lina sheria yake, mchakato ulikwamishwa, lakini sheria inalazisha mchakato UKAMILIKE mpaka tupate Katiba mpya. Kwa tafsiri hii ya sheria, jambo la kufanyika ni kufungua kesi mahakama Kuu, ili mahakama itamke wazi kwamba sheria imevunjwa, halafu itoe ODA kwa Serikali mchakato uendelee.

Pia, kwakuwa Serikali inaweza kusema haina Bajeti, sisi wananchi tuieleze mahakama kwamba tuko tayari kuchangia bajeti ya Katiba ila tunachokitaka ni Katiba mpya tu. Hapa tutakuwa tumeipiku Serikali.

Isipokuwa tutabaki na kizingiti kinginge, Bunge! Tusiogope. Approach hii itasaidia wananchi kujua ni chombo gani kati ya SERIKALI, BUNGE & MAHAKAMA kiko upande wa wananchi. Kuna mambo tunafanya sio ili tu kupata ushindi, bali KUWEKA REKODI.

Narudia, Rais wa nchi hana mamlaka KIKATIBA kuamua ni lini Katiba ifanyiwe marekebisho, Katiba imemnyima mamlaka hayo kwa sababu Rais ni mtawala na Katiba hulinda wananchi dhidi yake na walio chini yake.

MAMLAKA YA KUAMUA MABADILIKO YA KATIBA YAWE LINI NI YA WANANCHI WENYEWE.

[emoji1013] #BabaMwita
20230915_041848.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni muhimu kuielewa HISTORIA ya KATIBA ya Tanzania:
1961 (Katiba ya Uhuru)
1962 (Katiba ya Jamhuri)
1965 (Katiba ya Mpito)
1977 (Katiba ya Muungano)
Hakuna popote kwenye HISTORIA hii ELIMU ilitolewa kwanza kama SHARTI la KUANDIKA KATIBA. Wananchi WANATAKA KATIBA MPYA SASA.
20230917_055502.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kangi Lugola aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya ndani, alikuwa anaonesha uzalendo wake kwa kuvaa shati lililonakshiwa kwenye mifuko na bendera ya Taifa! Huku akitembea muda wote na kitabu cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwingine alijinasibu uzalendo kwa kuvaa tai yenye rangi za Bendera ya Taifa karibia muda wote.

Nina hakika wawili hawa hawajawahi kukutana na maswali ya moja kwa moja yanayohitaji majibu ya kikatiba, nukuu na vifungu vyake! Walijinasibu uzalendo kwa sababu ya tumbo!

Asilimia 95 ya watendaji kwenye mamlaka zetu hawajawahi kuisoma Katiba, hawaijui, na hawaifuati na hapa ni pamoja na Kiti chenyewe. Wanaweza na kujua ni wakati tu ule wa kukishika kitabu kidogo cha Katiba wakati wa kuapa.

Wanaoijua Katiba, kuisoma, kuichambua na kuitumia katika maisha ya kila siku ni wananchi wachache walioko nje ya mfumo wa kaliba mbalimbali, wasomi na wanasheria pamoja na wazee wachache wastaafu waliobaki.

Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji karibia wote wakusanye leo uwape mtihani rahisi wa maswali machache ya Katiba ujionee maajabu ya Dunia kwa alama watakazopata, na hii ni pamoja na kiti chenyewe!

Matamshi ya kuita Katiba ni makaratasi tu yanaangazia tatizo kubwa mbleni kuliko tunavyodhani.
Eeh Mungu isaidie Tanganyika iweze kuvuka salama
Tunategemea makubwa sana kutoka katika kile kiti. That kiti is not equiped to handle these inordinately massive national issues. Kile kiti hakijui hata kazi za kiti.

Fupa limetushinda vichwa milioni 60, miaka 60 ya uhuru, haliwezi fupa hili kutafunwa na kiti.

Not that kiti anyway....

Kila mstari wa Katiba ya Marekani umeshitakiwa mahakamani na tafsiri zake kutolewa.
Sasa mahakama za Tanzania zinapelekewa kesi ya kikatiba zinasema hawawezi kuingilia muhimili mwingine.

Kile kiti hakiwezi kuwa na majawabu ya mambo ya kikatiba ambayo hata majaji hawana upeo wa kuyatafsiri. Unahitaji kiti very very exceptionally special. Hatujapata bado mnyamwezi wa kubeba mizigo kama hiyo.
 
Tunategemea makubwa sana kutoka katika kile kiti. That kiti is not equiped to handle these inordinately massive national issues. Kile kiti hakijui hata kazi za kiti.

Fupa limetushinda vichwa milioni 60, miaka 60 ya uhuru, haliwezi fupa hili kutafunwa na kiti.

Not that kiti anyway....

Kila mstari wa Katiba ya Marekani umeshitakiwa mahakamani na tafsiri zake kutolewa.
Sasa mahakama za Tanzania zinapelekewa kesi ya kikatiba zinasema hawawezi kuingilia muhimili mwingine.

Kile kiti hakiwezi kuwa na majawabu ya mambo ya kikatiba ambayo hata majaji hawana upeo wa kuyatafsiri. Unahitaji kiti very very exceptionally special. Hatujapata bado mnyamwezi wa kubeba mizigo kama hiyo.
Kila mstari wa Katiba ya Marekani umeshitakiwa mahakamani na tafsiri zake kutolewa.
Sasa mahakama za Tanzania zinapelekewa kesi ya kikatiba zinasema hawawezi kuingilia muhimili mwingine.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom