Mtu anitajie IBARA ya Katiba inayosema kwamba Rais ndiye mwenye MAMLAKA ya KUKUBALI au KUKATAA uanzishwaji wa mchakato wa Katiba ya nchi! Kwa uelewa wangu, Katiba ni mali ya wananchi, inayotoa ULINZI kwa raia dhidi ya Watawala. Sasa, mtawala hatakiwi kuamua lini Katiba ifanyiwe maboresho. Hayo MAMLAKA yako kwa wananchi.
NINI KIFANYIKE!
Tunaweza kuanzia mahakamani (no guarantee). Kifungu 81 ya Sheria ya Tafsiri za Sheria (The Interpretation of Laws Act) kinasema kwamba kama kuna jambo limetungiwa sheria ili likamike, jambo hilo ni LAZIMA likamilishwe. Kushindwa kukamilisha jambo hilo ni KOSA LA JINAI. Hata kama sheria mahususi imesha muda wake, jambo hilo ni LAZIMA likamilishwe.
Suala la mchakato wa Katiba lina sheria yake, mchakato ulikwamishwa, lakini sheria inalazisha mchakato UKAMILIKE mpaka tupate Katiba mpya. Kwa tafsiri hii ya sheria, jambo la kufanyika ni kufungua kesi mahakama Kuu, ili mahakama itamke wazi kwamba sheria imevunjwa, halafu itoe ODA kwa Serikali mchakato uendelee.
Pia, kwakuwa Serikali inaweza kusema haina Bajeti, sisi wananchi tuieleze mahakama kwamba tuko tayari kuchangia bajeti ya Katiba ila tunachokitaka ni Katiba mpya tu. Hapa tutakuwa tumeipiku Serikali.
Isipokuwa tutabaki na kizingiti kinginge, Bunge! Tusiogope. Approach hii itasaidia wananchi kujua ni chombo gani kati ya SERIKALI, BUNGE & MAHAKAMA kiko upande wa wananchi. Kuna mambo tunafanya sio ili tu kupata ushindi, bali KUWEKA REKODI.
Narudia, Rais wa nchi hana mamlaka KIKATIBA kuamua ni lini Katiba ifanyiwe marekebisho, Katiba imemnyima mamlaka hayo kwa sababu Rais ni mtawala na Katiba hulinda wananchi dhidi yake na walio chini yake.
MAMLAKA YA KUAMUA MABADILIKO YA KATIBA YAWE LINI NI YA WANANCHI WENYEWE.
[emoji1013] #BabaMwita
Sent using
Jamii Forums mobile app