msumeno
JF-Expert Member
- Aug 3, 2009
- 2,826
- 1,734
Waungwana mimi kaka yenu nimezaliwa kijijini kwetu hukoooo Tabora,, mimi ni mtoto pekee kwa wazazi wangu... wazazi wangu kwa kweli hali yao ni kama ya wengi wetu hapa Tanzania hasa sisi wa Bush... ila faraja ni kwamba baba ana mashamba makubwa na mengi saaana kule kijijini... yaani kifupi yoooote yangu. sasa mikakati niliyo nayo ni kuyaendeleza kwa kufanya yafuatayo
TURUDI VIJIJINI TUKAVUNE UTAJIRI WALIOTUACHIA WAZAZI WETU... KILIMO NA UFUGAJI NDO MPANGO MZIMA
- Kufuga..... kianzio kipo
- kilimo cha cha mazao ya kudumu kama michikichi .. korosho... na mengine ... mtaji naweza upata Insha Allah
- Kuyasajiri yoote ili nisije nikavamiwa na wajanja kwa kigezo cha uwekezaji
TURUDI VIJIJINI TUKAVUNE UTAJIRI WALIOTUACHIA WAZAZI WETU... KILIMO NA UFUGAJI NDO MPANGO MZIMA