Nimegundua mpenzi wangu akiwa na marafiki zake, huwa ananiita mimi kimburu

Nimegundua mpenzi wangu akiwa na marafiki zake, huwa ananiita mimi kimburu

Katika pitapita kwenye maeneo ya ofisi ya mpenzi wangu, nikasikia wananiteta, ''kimburu wangu ananivuruga kweli, hataki kutulia na mimi, kila wakati ni migogoro tu''

Wenzie wakamuuliza, kimburu ndio nani; ndipo aliponitaja equation x.

Baada ya kusikia hayo maneno, hata sikuingia ofisini kwake, ikabidi niendelee na mihangaiko yangu.

Hapa bado natafakari, kwa nini ananiita mimi kimburu?

Nipeni ushauri wakuu, au na nyie wapenzi wenu wanawaita majina ya ajabu ajabu wakiwa na marafiki zao?​
Huo muda wakufanya hayo yote ulipatia wapi? Ulitakiwa uwe bize kwa kutengeneza mazingira ya kupata pesa
 
Kimburu kwa kiswahili cha mtaani ni paka asie na makazi maalum na asie na tabia nzuri na kazi yake kubwa ni kuvizia na kupora chakula kwa mfano kuvizia kuku akiwaona na kuwashambulia kwa ajili ya kula pia huvizia majumbani akiingia na kufunua masufuria na vyungu kutafuta chakula na muda wote utamuona hatulii anatazama kule na huko aidha anatafuta mawindo au akiogopa asije kudhuriwa kutoka na tabia zake mbovu alizonazo.Huyo ndo Kimburu.Mtu akikwita kimburu ni dharau kubwa sana !
Hapo ni sawa kabisa!
 
Kimburu= Ni mnyama mla nyama hutembea usiku na ni mwizi wa kuku, kimo chake ni chini ya ule wa paka ila ni mrefu kumzidi paka yaani miguu ya mbele ipo mbali na miguu ya nyuma anaweza kuwa mweusi au wa kijivu anatisha kwa ukali
 
Back
Top Bottom