Nimegundua shemeji yangu ana mwanaume mwingine. Je, nimwambie rafiki yangu kabla ndoa haijafungwa?

Nimegundua shemeji yangu ana mwanaume mwingine. Je, nimwambie rafiki yangu kabla ndoa haijafungwa?

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Stori iko hivi, weekend moja jamaa yangu wa karibu sana akanialika kwenye mazungumzo ya faragha kipindi tuko chuo. Alitaka kunitambulisha kwa mpenzi wake ambaye wamekubaliana kuanza mchakato wa kuoana. Nikawapongeza na kuwaahidi ushirikiano kutoka kwangu.

Siku nyingine rafiki yangu huyu akawa anamwelezea jinsi anavyofaa kuwa mke wake yule binti, moja ya sifa ni kwamba anaweza kuongea kisukuma, pili ni wa nyumbani, na ni mtiifu kwa hiyo jamaa aliwaambia wazazi waanze maandalizi ya mchakato.

Baada ya kama wiki 3 hivi tangu siku nimetambulishwa, rafiki yangu mwingine alikuwa anasoma Muhimbili akaniomba niende kwake computer yake inasumbua nikairekebishe, tikapanga siku siku yenyewe nikiwa nashughulikia computer huku tunapiga story, kama kawaida Yetu kipindi hicho.

Akaanza kunisimulia habari za mahusiano yake na mdada mmoja hivi akasema alikuwa hajawahi kutongozwa na mdada lakini mwaka ule imetokea alikuwa nyumbani Maswa ndipo alipokutana na hiyo request kutoka kwa mdada na wamekuwa wakiendelea na mapenzi kwa takribani miezi 2.

Mdada aliyekuwa anamsemea ndiye yule niliyetambulishwa kwake jana kuwa anataka kuanza mchakato wa kufungandoa na rafiki yangu yule mwingine huu ulikuwa mtihani wangu mkubwa sana sikumwonyesha ishara yoyote ya kushtuka niliendelea kumsikiliza na kumdodosa zaidi.

Unaweza ukafikiri ni movie vile kwa maana haikupita nusu saa yule dada akapiga simu kuwa anakuja hapo room kwa jamaa, jamaa akafurahi sana akasema njoo dakika 20 nyingi dada akafungua mlango uso kwa uso na mimi akiwa hajui kama tumemwongelea ilibidi ajifanya kushangaa akaonyesha mshangao fake, huku akiuliza.

"Kumbe na wewe huwa unafika huku?" Lakini hakutaja neno shem, kama ilivyo kawaida yake rafiki yangu akauliza, "ina maana mnafahamiana?" Nikawahi kujibu "Ndiyo, huyo ni wa Maswa." Sikusema kitu kingine zaidi, nikakaa kimya kama sijui chochote.

Basi mle chumbani tukawa watatu, basi rafiki yangu akawa yuko busy akimpetipeti mpenzi wake, lakini mpenzi mwenye haonekani kuwa tayari hata kukumbatiwa kimahaba basi mimi nikamaliza kazi yangu nikawaaga, nikawatakia kazi njema kilichofuata baada ya hapo ni mimi kuwaza nifanyeje next

Option ya kwanza ni kukaa kimya kama sijaona chochote, yaani niwaambie marafiki zangu wote hawa juu upande wa pili wa shiringi kuhusu huyu mpenzi wao wote ni marafiki zangu na tumetoka Maswa pamoja, na wao ni marafiki pia, tena wamesoma shule moja A level ile waliachana mwaka mmoja tu, na wanaheshimiana sana.

Option nyingine niliyoifikiria ni kumweleza yule ambaye anataka kuoa ili atambue kwa sababu nilijiuliza vipi akifunga ndoa halafu baadae katika maisha wakashindana tabia and then akaja kugundua kuwa mimi nilishuhudia kitu kama kile lakini niliamua kuaa kimya kama sijui na kumuacha aangamie nikiwa naona, je huo ndiyo urafiki wa kweli?
 
Waambie tuu washikaji kuwa wanataka kuoa kimeo, tena kama ana tabia ya kutongoza wanaume basi atakuwa na msururu Huyo.

Uzuri wanaume hatunaga noma mbele ya mwanamke, naamini hao jamaa urafiki utaongezeka na watatengeneza umoja wao wa kummega kwa zamu, au ikibidi wanammega kwa pamoja chumba kimoja!
 
Kuongea kisukuma ni kigezo cha kuolea [emoji23][emoji23][emoji23] we waache hayakuhusu..
 
Muombe anaetaka kuoa awatambulishe mchumba mkiwa wewe na huyi rafiki yako wa muhimbili, mbona simple tuuu, hapo huyo rafiki wa muhimbili atajionea laivu nila chenga jinsi wanavyochanganywa, then kama ana akili atampotezea

Kwa kufanya hivo utakua umetatua mgogoro wako wa nafsi kuliko kumwambia laivu muoaji kuhusu mabaya ya demu wake, anaweza akakuona unamsinichia
 
Waweke wazi marafiki zako wajipange nani anamwachia mwenziwe wao watapatana watamshirikisha mpendwa wao ingawa aliye tongozwa ana nafasi kubwa
 
Muombe anaetaka kuoa awatambulishe mchumba mkiwa wewe na huyi rafiki yako wa muhimbili, mbona simple tuuu, hapo huyo rafiki wa muhimbili atajionea laivu nila chenga jinsi wanavyochanganywa , then kama ana akili atampotezea

Kwa kufanya hivo utakua umetatua mgogoro wako wa nafsi kuliko kumwambia laivu muoaji kuhusu mabaya ya demu wake, anaweza akakuona unamsinichia
Umenena mkuu
 
Ndoa ni kiapo baina ya wawili mbele za Mungu kukivunja si rahisi muokoe huyo jamaa yaka kabla hayajamfika uaminifu ni nguzo kuu sana katika mahusiano na hasa ndoa Unapokosekana na vilio na majuto kwa wapendanao.
 
Funguka tu mkuu kuondoa utata, bora hivyo kuliko waje kujuta hapo baadae

Naamini mkisolve kiutu uzima mambo yatakaa poa
 
Bro kwanza hapo unatakiwa kuwa makini sana mkuu ili usije ukajenga ugomvi na mmoja kati ya hao marafiki zako kumbuka huyo shemeji yako tayari kashajua kuwa umemshtukia so atakachokifanya sasa ni kutengeneza mazingira ya wewe kuonekana muongo na mchonganishi.

Na huenda akawa yupo tayari kumkana mmoja kati ya hao wawili Kingine kukaa kimya kwa inshu kama hiyo ni jambo baya sana kumbuka kuchagua mke ndio kuchagua maisha utakayo ishi chamsingi tafuta njia nzuri ya kumthibitishia huyo anaetaka kuoa pasipo wewe kuonekana snich.

Waite washkaji wote wawili bila kuwaambia chochote kaanao chini Then wape mkanda full ulivyo Then mmoja kati yao ampigie simu huyo mwanamke aje hapo.
 
Nina majibu mawili yote sahihi kufanya ila moja ni sahihi zaidi (a)kaa kimya, (b)funguka chagua mwenyewe jibu sahihi zaidi.
 
'Sifa ya kwanza anajua kuongea kisukuma' asingejua kisukuma' asingefaa kuwa mke??
 
Back
Top Bottom