Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Hivi hawa wenye maduka siku hizi mnawaelewa kweli? Nazungumzia hawa wauza maduka ya vyakula Kwa rejareja kina Mangi na Muha hapo mtaani kwenu mnawaelewa? Labda ni Mimi pekee ndio siwaelewi.
Anyway, mwanzoni wakati naanza maisha ya ubachela, Kigheto ghetto nilikuwa napatana nao Sana hawa wauza maduka.
Sikuwa na tabia ya kuhama Duka Mimi. Nilikuwa ninaduka moja tuu ambalo ndilo nililokuwa nachukua bidhaa muhimu za nyumbani kama Unga, Mafuta, maharage, mchele, sabuni n.k.
Mimi napenda kuchukua vitu Kwa jumlajumla, yaani kama ni mchele ni kilo kumi, Mafuta Lita tatu, sukari kilo moja n.k Waswahili wanasema Mimi mwoga wa Maisha. Wao wamezoea kuchukua vitu roborobo vidogo kama viroboto.
Mimi Mafuta ya Mia tatu nitatumiaje, Unga Robo nitabebaje mimi, yaani kila siku niwe naenda Kwa Mangi au Muha Mimi, thubutu! Acha waniite muoga wa maisha kwani shilingi ngapi.
Mimi furaha yangu nikikaa kwenye Ghetto langu la kisela nione Stoo ya chakula imesheheni. Uhakika wa kwenda chooni ndio Jambo la Kwanza kwangu. Masuala ya kufikiri kesho itakuwaje na nitakula nini hayo nilimuachia rafiki yangu Kiboboso, yeye ndiye mambo yake hayo ya kununua mpaka Mafuta ya Mia mbili. Atajua na maisha yake lakini mbona yeye haishi kunipangia Maisha, aaargrrrrrrrhii! Naona natoka kwenye Stori kisa huyu mwehu Kiboboso.
Wahenga walinitungia Methali mahususi isemayo; masikini akipata matako Hulia Mbwata. Ndivyo nilivyo Mimi Bwana Taikon. Kwanza sina KAZI maalumu, Leo huku kesho Kule. Kote unikute pote unione nipo.
Nikiseti puzzle zangu zikatiki mbona mtaa mzima utajua.
Siku nimebeti alafu mkeka ukatiki, kibindoni nikitoka mawindoni niliweka kama laki mbili mfukoni. Mbona Majirani wananikomaga. Kwanza naenda kuoga, kisha navaa Suti yangu Fulani hivi ya kitasha, hii niliinua kipindi nasimamia ndoa ya rafiki yangu mmoja wa kishua huko Kwa walamba Asali. Hii suti ukiona nimevaa basi jua Taikon leo anapewa. Hata Hapa mtaani wameshanijua.
Naoga zangu wakati huo nimeacha muziki unapiga ungedhani kuna tamasha la muziki. Kelele mwanzo mwisho. Narudi kutoka bafuni na taulo likiwa kiuno nikiwa kifua wazi huku nikiwapita wapangaji wenzangu kama vile siwajui huku nikiimba wimbo kufuatisha muziki niliouweka ghetto.
"Hee thee do... Ooh my aaa. Ooh" Hapo ninaimba wimbo wa kingereza ambao siujui vizuri Ila nadandia na kurukia tulia maneno basi ilimradi nami nijitutumue .Mfukoni si ipo laki mbili. Nani Kama Mimi Bhana.
Nitaivaa Ile Suti yangu, labda unataka kujua ikoje. Ni nzuri Sana. Nikiivaa unaweza kusema ni Bwana Harusi, rangi yake ni kahawia iliyokolea, imenishika vizuri, chini imening'inia karibu na viwiko vya mguu Kule chini. Viatu vya vyeusi vya maana. Tai ikiwa shingoni licha ya kuwa kuna joto.
Hapo nitajiangalia kwenye kioo na kutengeneza nywele zangu huku bado nikiufukuzia ule wimbo nisioujua wa kingereza, alafu zile sehemu zinazojirudia za ule wimbo ambazo tayari zimekaa kichwani zikifika huwa natoa sauti kubwa kuziiimba mpaka Wapangaji wenzangu waliokaa hapo nje wananisikia.
Alafu kipande hicho kikipita ninakuwa Ninaimba " iii iiinn ninini" alafu nachanganya na Mlunzi kufuata instrumental ya muziki.
Tayari nitakuwa nimemaliza, nitazima Sabufa, kisha nikaichukua Ile laki mbili, na kuikagua tena Kwa kuihesabu ungedhani humo ndani tunaishi wawili. Zipo Sawa. Nazitia kibindoni natoka.
Nikishafunga mlango, najiweka tena vizuri alafu Mkono mmoja mfukoni kisha natembea Kwa madaha kufuatiana na Suti yangu nzuri yaheshima.
Sitowaongelesha majirani Hilo hata wao wanajua kuwa nikiivaa hiyo Suti ninapandwa na kiburi cha ajabu. Ninavyotembea, ninavyoweka USO na macho yangu, na kuna muda nabetua midomo huku kila mara nikipandisha mabega.
Alafu nikawa nawatazama, hapo nawaona wakiwa na hofu Ila kuna mwanamke mmoja akawa ananiangalia Kwa jicho la "Hilo nalo vipi" huku ameubetua mdomo wake. Lakini sijali wala nini.
Huyo mpaka dukani Kwa mangi. Wateja wenzangu wote wananiachia njia ungedhani ni Mheshimiwa, lakini Kwa hii Suti Acha wanipishe tuu. Hapo nitanunua bidhaa Kwa matambo huku nikitoa kejeli za rejareja Kwa wateja wengine. Nikijifanya ati Mimi ndio mteja wa thamani na tegemeo Kwa biashara ya mangi.
Nachukua vitu Kwa jumla bila hata kumuangalia Mangi akinihudumia. Sina hofu wala wasiwasi. Natoa laki mbili naanza kuzihesabu na kumpa mangi Hesabu yake.
Miaka ikaenda, mambo yanabadilika jamani. Nilikugundua Kwa nini watu huchukua mpaka Mafuta ya Mia tatu licha ya kuwa hakuna kipimo cha kiwango hicho.
Mdogo mdogo nikaanza kuona utofauti wakati nahudumiwa na dukani Kwa mangi.
Awali sikuwa mtu wa kumzingatia Sana Mangi wakati ananipimia labda ni Unga au mchele.
Sijui ni kitu gani kilichonifanya nione kama Mangi ananipunja.
Yaani nikimuambia naomba mchele Kilo moja. Akinipimia na kunipa naona kama sio kilo Moja. Naona ni ndogo.
Nikahama Duka lake, nikaenda Duka la pili, nalo vivyohivyo, nikaenda latatu huyu ndio Kabisa nikaona kama ananiibia kabisa. Yaani hiyo kilo ukiiangalia ni Kama vile nusu kilo.
Nikahama mtaa huo nikaenda mitaa mingine kununua mahitaji ya nyumbani nako vivyo hivyo. Nikasema hapa nisipoangalia nitahama Mpaka Kaya, wilaya na Mkoa mpaka nchi.
Siku moja nikiwa dukani, Mangi akanipimia mchele Kilo moja. Ndugu zangun, nusura tuzichape, yaani ilikuwa kanipunja haswa.
Nikamuuliza Mzee moja nikamwambia; Hivi Mzee wangu ulipokuwa na umri Kama Mimi ulikuwa unaona kadiri unavyokua mkubwa ndivyo unaona Bidhaa au vitu unavyopimiwa vinapungua ujazo na ukubwa?"
Mzee akacheka Sana, akaniuliza; " Kijana umeoa?" Nikamjibu ndio.
Mzee akasema, tena hapo bado. Ngoja uone siku zinavyoenda unaweza kugombana na wauza maduka.
Nikaondoka zangu,
Kumbe kadiri unavyokua mkubwa na familia inavyoongezeka ndivyo unavyoona vitu unavyovileta nyumbani havitoshi.
Unatakiwa kuongeza zaidi na zaidi.
Ulikuwa mwenyewe sasa mpo wawili. Mnakula nusu kilo.
Mlikuwa wawili sasa mmepata mtoto, mpo watatu na mnaongeza wengine familia inakuwa kubwa. Bajeti na kiwango cha chakula kinatakiwa kiongezeke.
Hapo macho yako sio ajabu yakaona kama unapunjwa ukiwa Dukani.Macho yote yatakuwa makini Kama Refa anayeangalia VAR, ukimtazama Muuza Duka kwenye Mzani.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Kadiri unavyokua inapaswa uongeze juhudi na uzalishaji ili kukidhi Mahitaji yako na familia yako.
Zamani 200,000/= niliiona ni nyingi Kwa sababu sikuwa nategemewa na yeyote. Lakini siku hizi wazazi wananitazama, mke wangu ananitazama, watoto wangu wananitazama, Wakwe zangu wananitazama, mashemeji na wadogo zangu wote wananitazama.
Bado hiyo 200,000/= nitaiona Kubwa?
Ile Suti yangu ilishapauka, mbwembwe zote zimekwisha. Hapa nilipo na babaika.
Kadiri unavyokua ndivyo unavyoishiwa mbwembwe na majigambo. Taikon leo akifika dukani Kwa mangi sio Yule wa kupiga makelele hovyohovyo.
Ninafika Kwa adabu nikitembea kama mtawa akiwa hekaluni. Hapo nitasubiri wengine wahudumiwe Kwanza niliowakuta. Na hata akija mwingine akanikuta huwaga namuambia Mangi amuhudumie tuu.
Hapo nimekuja kukopa.
Sio Mimi tena niliokuwa nawakejeli kina Kiboboso kuwa wananunua Mafuta ya Mia tatu na Unga chini ya Robo. Leo sina hata hiyo miatatu. Dooh!
Nipumzike sasa.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.