pesakilakitu
JF-Expert Member
- Aug 17, 2024
- 1,618
- 2,861
Katika kampeni iliyoanzishwa na Benki ya NBC ambaye ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu, mimi kama mdau wa mpira nimeshangazwa kama si kuchekeshwa na kusikitishwa na Kauli za Mwigulu, kwanza ametoa tuhuma kuwa uwanja tena eti wenye jina maalum kwamba pametolewa penati tatu, yeye anaujua mpira ama anaongea kisiasa na kishabiki ,,kwamba zile penati zilitolewa Bure?
Kwamba mchezaji akiangushwa kwenye eneo la hatari refa acheke akenue meno mpira uendelee kwa sababu uwanja unaitwa jina la Waziri mkuu? Siasa hazitakiwi kwenye mpira na ushabiki usio na mantiki sababu ni shabiki wa timu mmojawapo isikufanye uwe shabiki usiejielewa na unayeongozwa na mihemko.
Wewe kama Waziri unatakiwa ku deal na Hali ya uchumi wa nchi, Kuna matatizo mengi, wananchi ni masikini, deni la taifa linazidi kukua kila kukichwa, unapata wapi muda wa kuongelea mambo ya Simba na Yanga, unapata wapi muda wa ushabiki maandazi?