KERO Nimeibiwa kamera Tabata, sikupata msaada stahiki Kituo cha Polisi Stakishari. Mwizi anajulikana maeneo yale, amefanya tukio jingine na bado anapeta tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nachukia sana wezi, nenda ofc ya LHRC kawaeleze wanasaidia watu maskini km wewe buree
 
Pole sana bro ingekuwa enzi ya Magufuli hapo kituoni kuanzia mkuu wa kituo , mkuu wa upelezi na sijui wale masajenti wanao andika andika hapo wote wangekuwa hawana kazi

Kwa kuwa RB unayo hata wewe mwenyewe unaweza kumkamata tafuta tu marafiki 2 wakusaidie ukisha mmpata utampeleka polisi
 
Walioshauri vibuyu wezi wengi wapo fiti sikuhizi wanatumia vibuyu vya bei mbaya kuhakikisha kazi zao zinaenda na utahitaji kibuyu premium kumfikia😀 maana yake ukienda upande huo utaishia kupigwa tu pesa na wataalmu wa kweli wanahesabika wengi ni kama jamaa huyo

Ndio maana sikuhizi vijana wengi wanaingiliwa kama huyo na wengine wakishikwa watu wanamalizana nao juu kwa juu maana polisi hainaga msaada siku zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…