Pole sana Mkuu,hiyo inabidi utoe taarifa polisi pamoja na maelezo uliyopewa bank.Polisi kuna kitengo kinachoshughulika na wizi wa pesa kwa njia ya mtandao watakusaidia.
NMB ni wezi haijapata kutokea? Ukitumia ATM Machine umekwisha. Na hao watu wa claim wana majibu ya kunya haijawahi kutokea.
mkuu muone branch meneja fasta! Customer care zetu ovyo, utapoteza muda mwingi na hela hutaipata kama huja muona meneja! Ila Tembo card ni nbc kweli? Sio crdb?
usikubali benki wana namna ya kujua nani ametoa hata kama imetolewa kupitia exim mtu aliyetoa anajulikana mwone meneja wa benki waexpose kwenye vyombo vya habari ili watu wote wajue hiyo benki haiaminiki tena kutunza pesa za wateja hakikisha unafatilia hadi mwisho lazima pesa yako irudi
Fuatilia hela yako kwa kuweka kumbukumbu za maandishi, hizi ndiyo kesi ambazo tunazisubiri sisi wanasheria ili kuziwajibisha benki mahakamani...wakiendelea kukuzingua wasiliana na wakili yeyote aliyejirani akusaidie kufungua kesi ya madai watakulipa na usumbufu woote, pesa ikiibiwa kwenye akaunti aliyeibiwa ni benki wala sio mteja.Jumamosi nimetoa pesa kny ACC yangu kupitia ATM NBC kwa kutumia TEMBOCARD VISA yangu, jana nataka tena kutoa pesa kwenye Akaunti ATM ikasema sina hela kwenye ACCOUNT wakati nina hela za kutosha, leo nimedamkia kwenye tawi langu la CRDB, Counter wanadai hiyo hela iliyopotea imetolewa kupitia Bank ya EXIM, wanadai itakuwa imeibiwa wakaniambia nijaze Claim form alafu nifuatilie, but hawajui kama nitalipwa. Jamani hii imekaaje?