Nimeikumbuka TP Lindanda Pamba Football Club

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kwa wale vijana waliozaliwa miaka ya 2000 nawakumbusha tu kuwa Pamba ya Mwanza ambayo kesho inacheza robo fainali na Simba ilikuwa sio ya kawaida.

Golini alikuwa Madata Lubigisa, kulia David Mwakalebela, kushoto Deo Mkuki, Nne Abdallah Bori, sentahafu George Masatu, six Mao Mkami Ball Dancer, Winga Hamza Mponda, Nane Dan Mhoja, Tina Kitwana Suleiman, Kumi Juma Amiri Maftah Pele wa Mwanza na Kushoto ni Fumo Felician
Kulikuwa na Nico Bambaga marehemu, Hussein Masha, John Makelele Zig zag,.Alphoce Modest, Nteze John. James Washokera, Bitta John, marehemu Rajab Msoma.

Aisee, kesho Pamba wanaingia uwanjani nikikumbuka enzi hizo, nakumbuka mbali sana.

Sasa hivi hatuna tena wachezaji wa aina hiyo.
 
Huwa ananisisimua sana Bin Subery Sport A.M akiwachambua wakongwe wana TP Lindanda
 
Kipindi hicho walikuwa wamoto kweli.

Sema ndo wachezaji karibu wote walienda kariakoo na jangwani.

Huko nako walikiwasha kinoma
 
Timu ya kwanza na ya mwisho kuitandika timu ya ushelisheli magoli mengi
 
Wana Kawekamo TP Lindanda Pamba Ya Mwanza. Enzi za akina Mang’ombe aka baiskeli pikipiki mhamasishaji na shabiki wa mpira Tanzania ambaye sijawahi ona mfano wake. Sijui bado yuko mitaa yake Igoma pale kwa watu wazito Jiji la miamba
 
Mtangazaji wa soka aliyebase Mwanza enzi hizo marehemu Dominick chirambo alipokua akitangaza mechi ya Pamba ilikua burudani sana.
 
Naipenda sana hii timu.

Leo niko njia panda, nishangilie Simba au Pamba.
 
Golini Paul Rwechungura halafu kuna mtu anaitwa ITUTU KIGI alikuwa anakimbia balaa,FUMO FELICIAN alikuwa anachana nyavu kila mara na mashuti yake makali
 
Tp lindanda Wana KAWEKAMO😊😊
 
Wana Kawekamo TP Lindanda Pamba Ya Mwanza. Enzi za akina Mang’ombe aka baiskeli pikipiki mhamasishaji na shabiki wa mpira Tanzania ambaye sijawahi ona mfano wake. Sijui bado yuko mitaa yake Igoma pale kwa watu wazito Jiji la miamba
Yupo kishili siku hizi na baiskeli yake haiachi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…