na wewe
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 231
- 398
Za jioni wadau wa hapa.
Leo nimemsindikiza rafiki yangu kuja kujitambulisha kwa mara ya kwanza. Kwa lengo la kutaka kuoa. Hivyo kwa vile tulikuwa wachache na mimi huwa sipendi kuvua viatu mara kwa mara.
Tulipofika mlangoni nikaona niulize swali la kichokozi kwa mwenyeji wetu aliyetupokea, "kuwa kama kuna ulazima wa kuvua viatu."(nilijua lazima watazunga kuwa tuingie tu bila kuvua) ukweli mwenyeji alikubali lakini mzee kiongozi wetu wa msafara alitaka tuvue ila nililazimisha tuingie na viatu.
Ukweli nyumba ni safi sana na iko vizuri. Lakini baada ya kukaa nikama nimejishtukia kuwa hapa ni ukweni na ni sisi tu watatu ndio tumevaa viatu.
Sasa nauliza kwa wale wanaojua utaratibu kuwa kama inachukuliwaje pale unapoingia na viatu ukweni?
Mwanza Jijini